Wahenga ni akina nani hawa?

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Maranyingi naona watu wanatumia hili neno 'Wahenga' hasa wanapotaka kutumia misemo yenye Busara.
Je Wahenga ni akina Chifu Mangungo au Mkwawa?
Au ni akina Nyerere au Sokoine?
Na kwa nini tusitumie Jina na Mhusika aliyesema maneno hayo, kama tunavyofanya tunapoongelea maneno ya akina Martin Luther King au Gandhi?

Je kwa kama hatuwajui majina yao halisi ina maana hata misemo hiyo pia ni ya kizushi au uongo?

Nifafanulieni tafadhari
 
Wahenga hao walisema lini??
Na walimwambia nani??
Kwanza sidhani hata Kama hao wahenga walijijua kuwa wanaitwa wahenga!!!
 
Ndo hapo ninapopata maswali mengi Sir. Burn, tusijekuwa tunatumia 'umbea' kwa kisingizio kuwa ni maneno ya Busara ya 'wahenga'


Wahenga hao walisema lini??
Na walimwambia nani??
Kwanza sidhani hata Kama hao wahenga walijijua kua wanaitwa wahenga!!!
 
Mimi nadhani wahenga ni wazee waliotutangulia, ukiangalia wazee wa zamani kuna misemo yao mpaka leo tunatumia, haijulikani hao wazee ni kina nani ila wanaongelewa kwa ujumla.
 
Mkuu kama hatuna uhakika nani kasema nini kwa maana ya credibility, then kwa nini tukiamini walichosema? Ndiyo hao hao walisema pole pole ndiyo mwendo?

Mi nadhani wahenga ni wazee waliotutangulia,ukiangalia wazee wa zamani kuna misemo yao mpaka leo tunatumia,haijulikani hao wazee ni kina nani ila wanaongelewa kwa ujumla.
 
Wahenga inabeba ujumla wa mapokeo ya misemo ya zamani kwa njia ya methali ama ya moja kwa moja. wahenga si mtu/ watu ama mzee/ wazee la hasha hili neno wahenga linabeba jumla yao wale watu wazamani.
yaani maneno ya kimafunzo toka kwa wazee wetu tangu enzi na enzi.
 
Mimi nadhani muulizaji alikuwa anataka kujua "Wahenga" ni wakina nani na kwanini waliitwa hivyo, kama nimemsoma vizuri.
 
Mi nadhani wahenga ni wazee waliotutangulia,ukiangalia wazee wa zamani kuna misemo yao mpaka leo tunatumia,haijulikani hao wazee ni kina nani ila wanaongelewa kwa ujumla.


Agree with you 100%.

Wahenga ni 'ancestors'. Unajua zamani kabla ya development of technology watu walikuwa wanajifunza mambo mbalimbali ya kimaisha kuanzia afya, ulinzi etc kutokana na matukio yanayowakuta. Mfano mama Mjamzito anapokula sana aina fulani ya chakula na matokeo yake kufanya mtoto kuwa mkubwa kiasi kwamba njia ya kawaida ya kujifungua ilikuwa haiwezekani na hivyo kupoteza maisha, basi wazee walikuwa wanakusanya matukio kama haya na kuangalia sababu wakigundua wanakaa chini na kuona jinsi ya kuzuia matukio hayo kwa kutumia taarifa tu. Unakuta wanaanzisha misemo kama 'Mama mjamzito akila mayai, mtoto atazaliwa bila nywele' - ujumbe huu ulikuwa na nguvu sana katika kuzuia excessive eating of eggs kwa wajawazito.

Misemo mingi ilikuwa ikiwekwa na wazee kwa ajili ya kuzuia matukio mabaya waliyokumbana nao katika jamii. Wazee hawa walikuwa wanaaminika sana na jamii. Hivyo basi vizazi vijavyo navyo vinachukua maneno hayo na kuyaendeleza indirectly wanakuwa wanajikinga na majanga ambayo wazee waliisha yafanyia obervation research.

Mfano tu ni 'Bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi' - ina maana kubwa sana, kama mtu ameepuka janga fulani basi usidhani kuwa ni guaranteed, ndiyo maana katika ajali kuna wanaopoteza maisha na kupona, kwenye UKIMWI kuna wanaosahau kutumia condom na kujikuta hawajaambukizwa kwa hiyo usichukukulie kuwa ni kawaida kutokea hivyo, Inawezekana methali hii ,enzi za mababu ikawa ilitokana na 'mwanajamii kusahahu kufunga mlango na usiku swala akaingia ndani na kujipatia kitoweo, ila wakati huohuo kuna mwingine alisahau akaingiliwa na simba na kuliwa'. Haya yote yalitokana na Observation za wazee hao waliokuwa wakiishi enzi hizo.

'Noun

wahenga

  1. ancestors (ancestors)

'
 
Kuuliza sio ujinga,

Toka nimeanza kusoma darasa la kwanza mpaka namaliza elimu ya juu sijui wahenga ni akina nani, mara utasikia mtu akisema wahenga walisema asiyesikia la mkuu…, wahenga walisema mwenda pole...

Na mimi naomba kujuzwa hivi wahenga ni akina nani?
 
Wahenga ni watu wenye hekima, busara na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.

Tatizo langu na mimi lipo hapo kwamba ni kama vile walikuwepo zamani tu na siku hizi hawapo. Wahenga walisema....kwa nini hatusemi wahenga wanasema?
 
Wahenga ni watu wenye hekima, busara na uwezo wa kufanya mamuzi sahihi. Tatizo langu na mimi lipo hapo kwamba ni kama vile walikuwepo zamani tu na siku hizi hawapo. Wahenga walisema....kwa nini hatusemi wahenga wanasema?

asante, uko sahihi, na mimi naona walikuwepo zamani tu kwakweli, siku hizi ni majanga tu hakuna wahenga tena labda

kama kuna wahangwa.
 
Kuuliza sio ujinga,

Toka nimeanza kusama darasa la kwanza mpaka namaliza elimu ya juu sijui wahenga ni akina nani, mara utasikia mtu akisema wahenga walisema asiyesikia la mku…, wahenga walisema mwenda pole...

Wanajanvi naomba kujuzwa hivi wahenga ni akina nani?
Elders !! akina babu na akina bibi !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom