Bila Tanganyika (Tanzania|) yetu, sisi ni nani?

Apr 11, 2011
5
70
Na Ezekiel Kamwaga

KWA mujibu wa wanasayansi, dunia yetu ina umri wa takribani miaka bilioni nne na nusu. Katika miaka hiyo, nchi iitwayo Tanganyika imedumu kwa muda wa takribani karne moja tu – katika hiyo, angalau miaka 61 kama taifa huru. Kwa vyovyote vile, kama taifa, Tanganyika ni mtoto mchanga.

Taifa linajengwa na vitu vingi. Katika kitabu chake maarufu cha Sapiens, mwandishi Yuval Noah Harari, anatueleza namna mataifa yanavyojengwa kwa hadithi. Hii ni kwa sababu, Tanganyika – na kwa muktadha wa makala haya nitakuwa nikiichanganya na Tanzania kwa sababu zilizo wazi, si kitu unachoweza kukishika au kukiona kwa macho.

Tanganyika ni hadithi tamu. Hadithi ya ushujaa wa Mtwa Mkwawa na Chifu Songea. Tanganyika ni hadithi ya hadaa ya Karl Peters kwa Chifu Mangungo wa Msowero. Hadithi ya mapambano ya kudai Uhuru ya Julius Nyerere na Abdul Sykes. Hadithi ya ujasiri wa Bi Titi Mohamed na Lucy Lameck. Umahiri wa Shaaban Robert na Kaluta Amri Abeid. Ushabiki wa Simba na Yanga na ushawishi wa lugha ya Kiswahili. Hadithi ya Mapambano ya Ukombozi wa Mwafrika na Vita ya Kagera.

Kwa bahati mbaya, nchi nyingi za Kiafrika – na Tanzania ikiwamo, zimekosa mwendelezo wa hadithi nzuri kuhusu nchi zao. Mara nyingi, shughuli pekee ambayo huunganisha watu kama taifa ni sherehe za Siku ya Uhuru au Mapinduzi kwa wengine. Mara zote changamoto yangu na sherehe za namna hii ni kuwa nyingi hufanywa kwa kuwaenzi viongozi au daraja la walio madarakani wakati huo.

Nini hufanyika Siku ya Uhuru? Mara nyingi ni kwa kiongozi wa nchi kukagua gwaride na kutembea kwa msafara mkubwa wa magari. Pengine ataachia huru wafungwa kadhaa na kufanya dhifa kwa wageni Ikulu. Baada ya hapo Uhuru unakuwa umeadhimishwa!!

Hakuna kitu kingine chochote kinachofanyika majumbani kwetu na mitaani kwetu kuadhimisha siku hii. Sijawahi kusikia mtu anatamani kurudi nchini kwake (Afrika) kuwahi maadhimisho ya siku ya Uhuru. Kwa wale walio kwenye ajira, walau hupata siku moja ya mapumziko.

Kwa Watanzania wengi, maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi, Idi na Mwaka Mpya pengine vina maana kubwa kuliko Uhuru au Mapinduzi ya Zanzibar. Kuna makabila ambayo hutumia wakati huo kujuliana hali na kwenda makwao. Nafahamu watu ambão tarehe kama hizi wanawaza tu ni lini siku itafika ya kwenda kula Krismasi na watu wao.

Hata hivyo, huwezi kujenga Utaifa kwa Krismasi, Idi au Mwaka Mpya. Hizi zote ni sikukuu ambazo hazina uhusiano na taifa letu. Krismasi imejengwa katika misingi ya Ukristo ambayo si dini yetu. Idi imejengwa katika misingi ya Uislamu ambayo si dini. Mwaka mpya unatokana na kalenda ya Julian ambaye hana uhusiano wowote na Tanzania.

Kwenye nchi zilizodumu kwa miaka miaka mingi mingi zaidi yetu, kuna shughuli ambazo raia wake wamezipa umuhimu na zina maana kubwa kwao. India wana sikukuu ya Diwali ambayo sasa taratibu inaanza kuheshimiwa hata katika mataifa makubwa. Msingi wa sikukuu hii ni India na dini yao ya Kihindu.

China wana mwaka mpya wao wenyewe ambão hauna uhusiano wowote na mwaka huu wa kalenda ya Julian. Siku ya mwaka huu wa Kichina ni siku kubwa kwao na huadhimishwa na kila mtu anayeitwa Mchina.

Mataifa ya hivi karibuni kama Marekani kuna sherehe kama ya Thanksgiving ambayo ni kama ya kila Mmarekani. Wana siku yao ya Uhuru ya Julai 4 ambayo nadhani tunaweza kuiga kitu kutoka kwao. Hata hivyo, siku yao ya shukurani ni ya kipekee sana kwa watu wake.

Nilikuwa Uingereza katikati ya mwaka huu wakati Waingereza walipokuwa wakisherehekea miaka 75 ya Malkia Elizabeth kuwa madarakani. Familia zilikuwa zinakaa nje kula na kunywa pamoja. Ingawa mwishowe iliishia kwa Malkia na família yake kuungana não pale Kasri ya Buckingham, lakini niliona watu kwenye nyumba zao wakifurahia tukio. Uingereza ni Dola ya Kifalme na una mila na desturi zake na mojawapo ni kuenzi Ufalme.

Uhuru na kujenga taifa

Kwa wanaoangalia Kombe la Dunia, bila shaka watakuwa wanaona hisia tofauti za utaifa miongoni mwa wachezaji na wananchi wa timu zinazoshiriki. Kuna wale ambão nyimbo zao za taifa zikipigwa huwa wanatafuna banzoka na kutingisha shingo na kuna wale wanaotoa machozi. Kuna wale wanaolia wakifungwa na wale wanaokimbilia kupiga ‘selfie’ na masupastaa wengine baada ya kufungwa.

Kama hujui historia ya taifa lako, kama hujui ugumu ambão waliokutangulia walipigana mpaka kufanya mkasimama kama taifa, huwezi kuwa na uchungu na nchi yako. Uchungu kwa nchi yako hauji hivihivi. Unajengwa na kinachojenga ni zile hadithi ambazo tumezizungumzia mwanzoni mwa makala haya.

Nilishtuka wakati hayati Rais John Magufuli alipoanza kufanya uamuzi wa kusitisha maadhimisho ya siku za Uhuru na Muungano ili kuokoa matumizi ya fedha. Kelele hazikupigwa sana kwa sababu ukweli ni kwamba kwa mwananchi wa kawaida kule vijijini, mbwembwe za kwenye Uwanja wa Uhuru hazimsaidii chochote.

Tumeambiwa tena hivi karibuni kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameamua pia kutofanyika kwa sherehe za maadhimisho mwaka huu ili kuokoa fedha na ziende kwenye matumizi mengine ya ujenzi wa vituo vya afya. Hakuna kelele inayopigwa kwa sababu, kwa mara nyingine, wananchi wa kawaida wanakosa nini kwa kutofanyika kwa sherehe za Uhuru?

Pamoja na ukweli huo mchungu, swali ambalo nilijiuliza wakati ule wa Magufuli na najiuliza sasa ni hili; bila maadhimisho ya Uhuru au Mapinduzi yetu, sisi ni nani hasa? Kama taifa, tunaamini katika nini na ndoto yetu ni ipi hasa?

Huko tulikotoka, sisi wengine tulisoma na kutibiwa kwenye hospitali na watoto wa viongozi wakubwa wakiwamo marais, mawaziri na vigogo wengine. Michezo yetu ya utotoni ilifanana, hadithi zetu za shule zilikuwa zilezile na ukubwani kuna walioenda kupata mafunzo kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Ilifika wakati Watanzania walianza kufahamika kama watu fulani hivi waungwana, wanaopendana, makini na weledi. Mmoja wa walimu wangu Chuo Kikuu cha SOAS hapa London, Profesa Stephen Chan, alipata kuniambia kwamba ingawa yeye alikuwa New Zealand mwanzoni mwa miaka ya 1970, aliwahi kuwa na ndoto za kuja kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sababu ubora wake ulianza kufahamika duniani kwenye aina fulani ya kada ya masomo ya juu.

Kila nikiitazama Tanzania ya sasa, sioni kama tunajenga utambulisho wa aina yoyote. Watoto wetu hawasomi tena shule zinazofanana – kuna wa shule za kata, daraja la juu kidogo ya kata, za watu wa uwezo wa kati na zile za matajiri na viongozi wakubwa.

Sasa hivi, wala si ajabu kukutana na mtoto wa Kitanzania aliyezaliwa na kukulia Tanzania akiwa hazungumzi kabisa Kiswahili ambayo ni lugha yetu ya taifa. Siamini kama kuna mtoto wa Kihindi, Kichina au Kiarabu ambaye amekulia kwenye taifa lake lakini baada ya miaka 15, hawezi kuzungumza lugha ya taifa lake bali Kiingereza, Kifaransa au Kihispania. Sina uhakika.

Hata hospitali zetu zinazotuhudumia zina madaraja. Hata vyuo wanavyosoma watoto na jamaa zetu sasa hivi vina madaraja. Kwenda jeshini kupata mafunzo ya uzalendo na ukakamavu kwa sasa ni bahati nasibu. Wala si siri tena kuwa sasa tumeanza safari ya kumaliza mradi wetu wa kujenga taifa letu walilotaka waasisi wetu.

Kila nitazamapo, naona fursa kubwa ya kujenga nchi yetu tena na tena kama tunataka. Kwa mfano, badala ya kutumia mamilioni kufanya gwaride, kwa nini tusitumie maadhimisho ya siku ya Uhuru wetu kufanya vitu vingine?

Nakumbuka kauli mbiu moja mashuhuri mara baada ya kupata Uhuru ilikuwa ni Uhuru ni Kazi. Kwamba hatukupata Uhuru ili kukaa majumbani kwetu bila kufanya kazi. Kwa tafsiri hiyo, tunaweza kuendeleza kauli mbiu hiyo hata sasa kwa kufanya tukio moja kubwa.

Kwa mfano, katika wakati huu mgumu wa uzalishaji, tunaweza kutumia siku hiyo kutoa zawadi kwa mkoa ambao umezalisha kiwango kikubwa cha mazao ya chakula na ule wa biashara na kutoa zawadi kwa wakulima wake. Inaweza kuwa kwa kuongeza ruzuku kwa wakulima na wataalamu zaidi.

Tunaweza kutumia siku hiyo tena kutoa zawadi na kutambua vijana wanaofanya makubwa kupitia teknolojia za kisasa. Ukiwa Uingereza kwenye treni, utakutana na matangazo ya kampuni ya NALA ambayo inatoa huduma ya kutuma fedha kutoka Uingereza kwenda nchi kadhaa za Afrika na imekuwa na mchango mkubwa.

Lakini ni nani anamjua Benjamin Fernades na wenzake wa namna hiyo walioibua ubunifu wa namna hiyo. Siku kama ya Uhuru, ilikuwa ni siku ya kutambua alichofanya na kueleza ilikuwaje akafanya alichofanya na kipi kikifanyika tunaweza kuibua wengi wa aina yake na kutengeneza wajasiriamali watakaoongeza ajira na kuzimua uchumi wetu.

Kama kuna ubunifu ambao utatatua kero au mojawapo ya matatizo ambayo tayari tumeyatambua kama maadui wa taifa, siku ya Uhuru ilitakiwa kuwa ya kutambua waliohusika na hilo na kuwaenzi.

Tunaweza kuamua kuwa Siku ya Uhuru iwe ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wetu mahiri wa ngazi zote na kuwatambua. Kama kuna utafiti muhimu umefanyika kuhusu dawa au mbegu mpya za mazao mashambani ambao utaongeza tija na ufanisi shambani na kazini, hiyo ndiyo siku ya kutambua.

Na mnaweza kuamua kuupa kila mwaka jina la mmoja wa wahenga wetu. Kwa mfano mkaamua mwaka 2023 uwe Mwaka wa Mkwawa. Mnachofanya ni walimu wa ngazi zote kufundisha angalau mara moja kila wiki kuhusu Mtwa Mkwawa na yale aliyoyafanya kwa Tanganyika. Aliamini nini, alipigania nini na kwa nini alishindwa na Wajerumani waliokuwa wachache? Ilikuwaje makabila yaliyomzunguka yalimwacha mwenyewe apigane na Wajerumani? Haya ni mafunzo ambayo yatatujengea viongozi imara wa baadaye.

Kwenye muktadha huo, tunaweza kutengeneza filamu ya Mkwawa kama hizi zinazotengenezwa kwenye Netflix na watoto wetu wakaigiza shuleni na wakubwa wakafanya tamthilia kwenye redio, kumbi na luninga. Uingereza bado wanaonyesha michezo ya William Shakespeare hadi leo na binafsi wiki mbili zilizopita nimetoka kutazama tamthilia ya Othello iliyofanyika jukwaani hapa London.

Waigizaji mashuhuri wa miaka ya karibuni hapa Tanzania kama Vincent Kigosi (Ray) na marehemu Steven Kanumba (Kanumba), walianzia vipaji vyao kwenye sana aza maonyesho majukwaani na wakaja kuwa nyota waigizaji kwenye luninga. Kama hatuigizi tena kwenye shule zetu na majukwaani, tunategemea tasnia ya filamu – ambayo nadhani ina fursa kubwa kwetu kwa sababu kuna kipindi tulikuwa tunashindana na Nollywood ya Nigeria, itapata wapi watu mahiri.

Tamthilia na filamu ni mojawapo ya nyenzo muhimu kwenye kujenga utaifa. Mojawapo ya nyenzo kubwa ya utawala wa Marekani duniani hivi sasa ni Hollywood ambako filamu na tamthilia zake zimeteka dunia nzima. Si kwamba wanatengeneza fedha na ajira nyingi duniani kupitia sekta hiyo lakini wanasambaza utamaduni wao duniani na kuusimika zaidi miongoni mwa raia wake.

Vipi kama tukitumia maadhimisho ya Siku ya Uhuru kuzitaka família kutumia siku hiyo kwa wananchi kula pamoja na jirani zao na kujali wenye shida walio miongoni mwao? Kwamba walio na nguo, viatu na vingine wasivyohitaji wanapeleka kusaidia wenye uhitaji?

Kwa maoni yangu, kufufua Utaifa wetu maana yake ni kuifanya sherehe ya Uhuru kuwa ya wananchi na si wenye madaraka na majeshi yao. Tunahitaji kuifanya sherehe iweke mizizi yake kwa wananchi wake. Ikifika mahali watu wanasherehekea Siku ya Uhuru kama wanavyofanya kwa Krismasi na Idi, nina uhakika Tanzania haitakuwa tena miongoni mwa nchi masikini duniani.

Mawazo yangu ni finyu sana na naamini kuna mawazo mengine mapana zaidi lakini jambo la msingi kwenye makala haya ni kuweka msingi wa namna Uhuru wetu uwe Uhuru wa wananchi.

Kwa kasi hii ninayoiona ya kupoteza utambulisho na Utanzania wetu, unaweza kujenga hospitali na shule kila mahali lakini ukaja kuishia kusikia watu wameiba microscope na wametumia viti vya darasani kama kuni za kupikia. Na kama elimu yenyewe inayotolewa itakuwa ni ya kufanya wakichukie Kiswahili au kumjua zaidi Shakespeare kuliko Shaaban Robert na hospitali yenyewe inapima malaria na haina hata dawa, tutavuna mabua.

Tanzania ni Mama yetu. Na kama tunaamini hakuna kama mama, tunahitaji kuamka kutoka kwenye usingizi wetu. Sasa.
 
Hatukupigania uhuru kama walivyopigania Wamarekani dhidi ya Ufalme wa Uingereza au WaSouth dhidi ya makaburu
 
Kuna mwanasiasa wa zamani Italy alisema, "Tumeiunda Italy, sasa lazima tuwatengeneze Wataliana ". Tafsiri isiyo rasmi.
Nahisi na sisi bado hatujawapata Watanzania. Tunajiona zaidi Wazanzibari, Wapemba, waislamu, wakristo, wa wa kila kabila lililopo.
 
Kweli aisee angalau hii siku tungeuziana vitu kwa mfumo wa ujamaa kila mtu apate,iwe siku ya aman mtaani watu wajuliane Hali lakin kwa sasa hii sherehe inamaana tu ya kua siku ya off kazini
 
Shida kwa nchi zote za Africa ni kuwa historia zao zinaanza kwenye Utumwa and going forward and not before. Ukiacha Ethiopia...... Turudi nyuma tuandike historia yetu ndio mdogo mdogo tutasogea.
 
Hongera sana mkuu! Andiko lako linathibitisha kuwa wewe ni msomi mwerevu mnyenyekevu. Fikra za sampuli hii ni malighafi adhimu kwa ujenzi wa Taifa.
 
Hatukupigania uhuru kama walivyopigania Wamarekani dhidi ya Ufalme wa Uingereza au WaSouth dhidi ya makaburu
Wewe unaewaaabudu Wamarekani...huwezi elewa Vita ya majimaji ilikuwa ni kupigania Uhuru....
Vita vyote walivyokuwa wanapigania babu zetu vilihusu uhuru
 
hayo Mapinduzi kule Zanzibar yalishakataliwa, wenyewe hawataki hata kuyasikia wewe bado unayapiga promo tu
 
Kungali kuna mkanganyiko! Kuna wanaoyaita MAPINDUZI TUKUFU hivyo wako tayari kuyalinda kwa gharama yoyote, na kuna wanaoyachukulia kuwa yalikuwa MAUAJI KATILI hivyo kila yanapoadhimishwa hukumbuka wapendwa wao waliopoteza maisha kipindi hicho.
 
hakuna anelinda mapinduzi zaidi ya wanufaika wa mfumo wa utawala, wanchokilinda na maslahi yao na familia zao tu.
 
Back
Top Bottom