Wahanga wa vyeti fake ni wakati wa kutuliza akili sana na kushikamana kwa Pamoja wana familia wote

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Baada tu ya Tangazo la Rais Magufuli kuondolewa na kutangaza ktk vyombo vya habari watumishi wenye vyeti fake nadhani ni muda pia muafaka kwa kuwatia moyo kwa msamaha huo wa Rais.

Kwanza mpo nje na mko huru kuendelea na maisha kama wanainchi wengine wa kawaida.

Silaha yenu kubwa ni mshikamano ktk familia ili msije mkatengana hata Mara moja kwasababu tu ajira imekoma

Kumbukeni huyo Baba, Mama au kaka,Dada ndiye alikuwa anafanya ikaitwa siku nyumbani sasa sio tena dharau zinaanza za wana familia.

MTU Unapoenda vitani unabeba silaha yoyote ile ili ushinde vita lakini ikitokea ukashindwa vita basi unarudi nyumbani kimya kimya lakini lazima upokelewe.

Mashirika,Taasisi,NGOs,n.k hawa walioondolewa ni wataalam wa Fani tofauti tunaweza kuwatumia.

Na wao wanaweza kujiorganize na kuanzisha chochote kile cha kufanya kazi.

Wana psychology muwe Karibu na kundi hili ni watu wengi sana.
 
Kuna watu wana ROHO ngumu Na mbaya Nchi hii sijapata kuona,mbaya zaidi tumewapa dhamana ya kutuongoza!Mungu muumba mbingu Na Nchi Simama Na sisi Na Utuguse,ww tu ndie tunaekuabudu Na ww tu ndie tunaekuomba Msaada!Ameen
 
Hilo dua la kuku. Nawe umo?
 
Mungu majibu yake hayawagi mbali .Usiudharau ushauri anaoutoa binadamu mwenzako kumbuka imani zinadumu milele na hizo imani tunaziishi kupitia rohoni ,vichwani mwa wenye hizo imani na vinywani kwa ajili kufikisha ujumbe
 
wakati wa richmond kampuni ilikuwa feki lakini ililipwa kutokana umeme uliozalishwa licha ya kampuni kuwa feki,
hawa wenye vyeti feki hawana budi kuondoka, ila ni muhimu wakalipwa stahili zao.
 
Umetoa mawazo mazuri, sema jamii nayo ni tatizo kuanza kuchekana mkuu.
Hilo ni tatizo kubwa la Tanzania, unaweza kumsaidia kwa moyo mmoja kabisa Leo lakini kesho ukakwama hata kama hujamwomba msaada yeye lakini anaweza asiwe na habari na wewe na kukupikia na majungu pia.
 
Plan B ilitakiwa iwepo tangu zamani maana ukiwa na cheti feki unajua ni 50/50 mambo yanaweza kubuma

Huu ni muda wa kupata ushauri na kupewa moyo na wanafamilia...ili kuikubali hali.

Then unaanza upya, kama ulikuwa jasiri kuwasilisha cheti fake pia kuwa jasiri kuanza upya.

Kila la kheri.
 
Hilo ni tatizo kubwa la Tanzania, unaweza kumsaidia kwa moyo mmoja kabisa Leo lakini kesho ukakwama hata kama hujamwomba msaada yeye lakini anaweza asiwe na habari na wewe na kukupikia na majungu pia.
Wakae watafakari njia zao.
 
Kuna watu wana ROHO ngumu Na mbaya Nchi hii sijapata kuona,mbaya zaidi tumewapa dhamana ya kutuongoza!Mungu muumba mbingu Na Nchi Simama Na sisi Na Utuguse,ww tu ndie tunaekuabudu Na ww tu ndie tunaekuomba Msaada!Ameen
Hakuna mwenyewe roho mbaya aliyepewa dhamani ya kuongoza nchi.Viongozi wote wanaofuta sheria kwa dhati huwa hawapendwi na jamii isiyopenda kufuata sheria
Kuna watu wana ROHO ngumu Na mbaya Nchi hii sijapata kuona,mbaya zaidi tumewapa dhamana ya kutuongoza!Mungu muumba mbingu Na Nchi Simama Na sisi Na Utuguse,ww tu ndie tunaekuabudu Na ww tu ndie tunaekuomba Msaada!Ameen
Hakuna wenye roho mbaya bali jamii isiyopenda kufuata sheria ndiyo utaona hivyo.

MUNGU humlinda kiongozi anayemtii na kutimiza Neno lake.Kiongozi anayeifundisha jamii kuwa hili ni Jema na hili si jema humpendeza MUNGU

Hata MUNGU aliwaadhibu wote waliokwenda kinyume na maagizo yake someni maandiko.

Rais Magufuli anajaribu kwa kadri awezavyo kutukumbusha u muhimu wa kufuata sheria
 
Kuna watu wana ROHO ngumu Na mbaya Nchi hii sijapata kuona,mbaya zaidi tumewapa dhamana ya kutuongoza!Mungu muumba mbingu Na Nchi Simama Na sisi Na Utuguse,ww tu ndie tunaekuabudu Na ww tu ndie tunaekuomba Msaada!Ameen
Acha kulalamika wewe wakati unafoji cheti unaona ulikuwa sahihi? Saivi ndo unamkumbuka Mungu?
 
Back
Top Bottom