Wahadhiri, wanafunzi OUT kujitetea mara mbili

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Wahadhiri, wanafunzi OUT kujitetea mara mbili
Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 17th November 2009 @ 22:00 Imesomwa na watu: 31; Jumla ya maoni: 0






WAHADHIRI wanne na wanafunzi takribani 50 wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) wanaotuhumiwa kudanganya katika matokeo watajitetea mara mbili kwa namna tofauti.

Uongozi wa chuo hicho, umesema, watuhumiwa hao wanajitetea wiki hii kwa maandishi kupitia kamati maalum inayofuatilia tuhuma hizo, Baraza la chuo hicho limetoa idhini kwa kamati hiyo kushughulikia utetezi huo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette, amesema, licha ya kuanza kujitetea kwa maandishi, watuhumiwa watajitetea pia kwa mdomo (ana kwa ana) ili kuwapa nafasi nyingine na pia chuo kijiridhishe.

“Hii itasaidia kila mmoja kujiridhisha kwamba ametendewa haki kabla ya uamuzi kutolewa, hatua hii siwezi kusema itachukua muda gani kwa kuwa muda mrefu unahitajika maana wanafunzi wanatoka sehemu mbalimbali za nchi si Dar es Salaam pekee,” amesema Prof. Mbwette.

Alisema katika kipindi cha wiki chache zinazo, hatua kubwa ya kutoa utetezi itakuwa imefikiwa.

Kwa mujibu wa Profesa Mbette,kila mtuhumiwa atapata nafasi ya kutosha kujieleza katika aina hizo mbili kwa kuwa suala hilo linagusa mustakabali wa maisha
 
Back
Top Bottom