Wahadhiri waeneza siasa za chuki vyuoni

Sasa kama Wahadhiri hao wanafundisha siasa na wanahitaji kutoa mifano kutoka Serikalini wafanyeje? Wawaambie wanafunzi uongo? Mulugo huyu si yule wa Songea Boys.........amebadilika sana,ameisha kabisa.Pole kaka,Mwalimu Mulugo.
 
zipo coz ambazo huwezi kuacha kuzungumzia siasa mfano Political Science au hata sheria kwa mfano Constitutional lw, Human Rights, Administrative law na zingine.

Serikali iseme kuwa imeshndwa kazi na wanatafuta mbaya wao wakat wanamjua aka ufisadi.

Nadhani ni muhimu kwa wahadhiri kulitolea kauli hili ili kuwakemea mawazir wa JK kuwa makini na kauli zao.

Serikali inataka kumfunga mdomo kila mtu sasa, mwishowe watatuambia wananchi tusizungumze chochote mpaka kwenye vikao.

this is to be done MAPEMA IVEZEKANAVYO
 
'Wahadhiri ni watu OBJECTIVE wanajua nini cha kufanya kwa wakati na mahali gani
ukiona lecturer analeta siasa kwenye theatre ni ZUZU' - Dr. Mkumbo

Asante kwa habari.
Itakuwa bora zaidi na utakuwa umemtendea haki uliyemnukuu kama utaonyesha wapi,lini na kwa watu gani kauli hiyo ilitolewa.Hii itatupa mwanga wa mwanataluma huyu kuwa ni mtu wa namna gani!.Lakini pia atatusaidia kufafanua kauli yake,maana kwa mtazamo wangu kauli inajikanganya.
 
Labda waseme vyou vinavyofundisha Sayansi ya Siasa, Demokrasia, utawala bora, uchumi na maswala ya jamii vifute kozi hizo.

Usalama wataifa feki unawadanganya. Kwa vile CCM ina uvivu wa kufikiri inaona wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kutokiunga mkono ni inasababishwa na wahadhiri!
 
Asante kwa habari.
Itakuwa bora zaidi na utakuwa umemtendea haki uliyemnukuu kama utaonyesha wapi,lini na kwa watu gani kauli hiyo ilitolewa.Hii itatupa mwanga wa mwanataluma huyu kuwa ni mtu wa namna gani!.Lakini pia atatusaidia kufafanua kauli yake,maana kwa mtazamo wangu kauli inajikanganya.

KALIX2 MBONA hiyo iki straight? nadhani dr hapo kusema siasa alikuwa na maana kujaribu kudanganya danganya wanafunzi ilikila kitu kionekane swaafi ilihali mambo yameharibika
 
hili jambo liangaliwe kwa umakini kwani unaweza kuta mhadhiri wa ualimu aananza chambua viongozi wa serikali na kupandikiza chuki miongoni mwa wanachuo.
kama wanapenda siasa basi wajiunge na vyama wanavyovipenda na kupanda majukwaani.
mwanafunzi wa chuo ni mtu mzima na ana uwezo wa kuchambua lipi la kweli na ni lipi la uongo,katika hatua hii ya elimu mwanafunzi anajifunza na kufundishwa mambo mengi ya kijamii ambayo ni kwa ajili ya kumjenga uelewa wake,masomo kama principles of management,development studies,principles of economics pamoja na mihadhara mbalimbali ya kielimu sitegemei mhadhiri afundishe kwa kutolea mfano wa mambo ya marekani au ulaya badala ya haya ya nchini,linapofanyika hili serikali hii inaona ni uchochezi hii haiingii akilini na wala haikubaliki
 
Vyuo vikuu ni chemchem ya mabadiliko wanafunzi hao wanapaswa kufahamu kwa undani namna serikali inavyoteleleza majukumu yake na namna pesa za umma zinavyotumika na kwa maslahi ya nani.

Vyuo vikuu wanafundishwa watu wa kada mbalimbali hivyo ni vema wakaelewa mapungufu na mazuri ya serikali yao.

Isitoshe kuna masomo vyuo vikuu ambayo yakifundishwa mtu hawezi kukwepa kuzungumzia siasa e.g. Public administration, political science, public resource management, human resource management etc..

Serikali itimize wajibu wake ipasavyo wala haitasikia harufu ya migomo.

Masomo yote ya social science, Science na welfare hayafundishiki bila kuangalia governance na policies sasa hapo mhadhiri ataachaje kuongelea government? I thinkwhere these people are heading siko kabisa! Ndiyo maana ikaitwa Reasearch and Development (R & D). Waache uvivu wa kufikiri wafanye kazi kikamilifu, its only because they dont use effectivel the Academia except for political purposes ndiyo maana wana fail katika policies zao.
 
Labda waseme vyou vinavyofundisha Sayansi ya Siasa, Demokrasia, utawala bora, uchumi na maswala ya jamii vifute kozi hizo.

Usalama wataifa feki unawadanganya. Kwa vile CCM ina uvivu wa kufikiri inaona wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kutokiunga mkono ni inasababishwa na wahadhiri!

Si wezi shangaa wakitamka kuvifuta; kwani si walisha wahi kusitisha field practicals kwa kisingizio cha kwamba theory tu inatosha?
 
Huku sasa ni kuweweseka kwa mchana, sijawahi sikia tokea nizaliwe kuwa serikali inachunguza wataalam wa vyuo vikuu jinsi wanavyofundisha. Wapige marufuku vyuo vikuu.

Chuo kikuu wanaohudhuria ni watu wazima wenye kuelewa na kujielewa huwezi kuwaingizia mawazo yako. Serikali ianze kwenye kuchunguza mitihani kama ni ya kisiasa. Huwezi kaa darasani three hours unazungumzia mada tu watu watalala lazima uingize stori mojamoja ya kuwafanya wawe active.

Mi wakati nasoma nilikuwa ninampenda sana mwalimu mmoja kwa kuwa jamaa alikuwa akituchekesha sana darasani hasa kuhusu viongozi wa nchi vilaza wanaotoa maamuzi bila kufikiri, kama yule aliyewahisema Daresalaam ina maji ya shida sasa akikuta mlima mchicha ana mchicha wa kijani atamueleza maji ya kumwagilia kayapata wapi?, wakati halisi ni kuwa mchicha ni lazima uwe wa kijani kwa sababu ya kuwepo kwa chlorophyll which helps in photosynthesis.

wafanye kama SARAFINA

 
Last edited by a moderator:
CCM wasijaribu kuwatonesha vidonda wasomi wetu kwa kuanza kuwaingilia kwenye kazi zao huo ni ujinga kabisa walimu wanafanya kazi kwenye mazingira magumu, na kwa uzalendo kabisa halafu leo anatokea mtu hana mbele wala nyuma anasema wanawasaka wanawatishia nyau mbona pale UDOM walipoweka tools down walikuwa wanababaika, nadhani vyama vya wahadhiri watakutana waoombe ufafanuzi maana yake nini manake nadhani kuna watu wao wanaotaka kuwafukuza ili wajustify wanayosema.
 
Hao akina Kawambwa wanashindwa kusoma alama za nyakati! Hata kama wahadhiri hawatasema chochote, bado hao wanachuo watapata taarifa kuhusu erikali yao kupitia vijiwe, magazeti TV nk.

Halafu waalimu wa shule za sekondari, shule za msingi ambao ndio wengi na wanaidai serikali, na bado wako kwenye mazingira yenye changamoto wao wataisemaje serikali yao!
 
I cannot understand the teacher/trainer/lecturer who does delivery/presentation on corporate governance for instance fails to cite relevant lessons students may get from EPA, KIWIRA, Richmond etc. The cases are cited to instill them analytical skills no more no less, i guess. For brilliant lecturer who is not brain washed he/she can not continue citing cases such as Enron scandal, etc from abroad while we have our own-made cases in Tanzania.

I suggest all scams such as EPA, Richmond, Dowans need to be well documented in good faith as case studies by different specialists in various fields to help in teaching our students. By so doing, it will help the existing managers/ decision-makers and future generations to know what when wrong and how can they avoid them.

A good question I always ask when I argue about ward schools for example what needed to start between "building of schools vs training of sec-teachers"? this is not an easy question at all. However it evoke inquisitive and analytical mind when one tries to answer such simple question.

The generalization will fail us and do us no good - I think politics does affect people' lives so man-kind has a number of lessons from politics depending ones field.

Just a caution!
 
Ni ujinga na upuuzi kuona kuwa siasa au kusema kutumia kuongea siasa vyuo vikuu n Je kama Lecture anafundisha soma la Political katika vyuo hivi asiseme kitu juu ya siasa, Je kwa sasa tunasoma Political Science kama Government and Politics in Tanzania hakuna siasa hapa?

Je kama mtu anasoma Political and Public Administration PSPA degree hakuna siasa hapa?? Je kama mtu anachukua au anasoma soma la Uraia au Siasa hakuna siasa hapa, hali kama hii bila shaka kuna haja ya kukemewa vikali maana hawa jamaa wanabaki uhuru wa vyuo katika kufundisha hata kutoa mawazo, na ni ujinga kusema kuwa hakuna siasa lakini wao CCM ndio wa watu wa kwanza kugawa kadi za CCM usiku katika vyuo vingi Tanzania.

Bila shaka Tanzania lazima tuamke sasa na tusema Vyuoni ndio viongozi wanapikwa na kuongea siasa ni sehemu yake na siasa ni maisha yako na inanzia nyumbani na jinsi ya maisha yako ya kila siku yanavyokwenda
 
Kama wahadhiri wote chuo kizima wanafanya hivyo ili kuwaelemisha wanafunzi wao utafanyaje? Fukuza wahadhiri chuo kizima halafu serikali iende ikafundishe.....best strategy ya CCM government.

Yaani mnashindwa kutafuta njia ya kupunguza makali ya maisha ya watanzania............mnataka mjibanze kwenye madarasa vyuo vikuu kusikiliza wahadhiri wanachoongea. That's genius.
 
Kazi kweli ipo.

Kama mimi ni mwalimu namwaga pindi halafu naona kwamba nchi imeenda siko lazima na ni wajibu wangu kuwaeleza wanafunzi kwamba jamani ninyi mkienda huko jaribuni kubadilisha hii hali kwani sio nzuri.

Badala ya serikali kuangalia jinsi ya kuendeleza elimu Tz, wao wanakuja na sera zao mbovu. Hivi kwanza huyo jamaa kweli amefikiria au wanataka kuwafurahisha mafisadi wenzao? Tz hakuna kurudi nyuma wahadhiri komaeni hapa kwani ukombozi unakuja mbele yetu.

Elimu mbovu lkn serikali hakuna kitu wanachofanya kusaidia elimu kaz yao ni kupeleka watoto wao Ulaya/Asia kusoma halafu wanarudi nchini kuchukua hizo kazi, kweli hii sio haki. Inabidi tupambane mpaka dakika ya mwisho. Najua hata wewe unayesoma huu ujumbe kama umetumwa na hao mafisadi kawaambie kwamba Tz ya leo sio ya kipindi kile.

Natamani tupate wahadhiri kama Prof. Chachage/Othman kila chuo hapa Tz ili vijana waweze kupata kujua mambo mbalimbali na umuhimu wa kuwa mtu wa kupambana na kusaidia wananchi wa hali ya chini.

Ninayo mengi sana ya kusema ila muda hapa unakaba. Ngoja nikatafute mlo kwanza nikirudi tutaongea vizuri.
 
Huko ni kutaka kuwafundisha namna ya kufundisha. Sasa mhadhiri wa DS atatoa wapi mifano hai na relevant kwa society ya Tanzania kama vile bad governance, non free and unfair election? China?
 
Kwani wahadhiri vyuo vikuuu wanafundisha au wanafahamisha mambo? Nijuavyo lecturer wa chuo kikuu si mwalimu bali ni mhadhiri kwasababu anachokifanya ni kufahamisha na kutoa mifano halisi kwa jamii.

Sasa kama vyuo vikuu imekuwa kama primary school au secondary school basi hili tamko ni sahihi ila kama ni vyuo vikuu vya taaluma wanaomaliza vyuo vikuu ni decision makers (sio wanafunzi) hivyo basi kama hawawezi kutatua matatizo ya jamii basi hawafai kuitwa wahitimu wa vyuo vikuu!!!
 
hili jambo liangaliwe kwa umakini kwani unaweza kuta mhadhiri wa ualimu aananza chambua viongozi wa serikali na kupandikiza chuki miongoni mwa wanachuo.
kama wanapenda siasa basi wajiunge na vyama wanavyovipenda na kupanda majukwaani.
chuki wanapandikiza wenyewe ccm wewe unamwambia mtu tutakupa mkopo woote tena unabadilika huu ni ujinga!
 
Back
Top Bottom