Wagonjwa Muhimbili walia adha ya mgomo

Kwani madaktari wasipokuwa kwenye mgomo wagonjwa hawapotezi maisha? Ujauzito ni stress kwa mwili, ikiongezewa na pneumonia complications tena, na ukizingatia miundobinu iliyopo unapata jibu.
Poleni na msiba.
 
Wakuu niko hapa muhimbili, na mkuu wa mkoa wa dsm yupo hakuna Dr hata mmoja na gari la wagonjwa aka ambulance likija na mgonjwa linaambiwa rudi naye ulipotoka mana hakuna dr. Kazi ipo, JK haelewi kinachoendelea yuko kimya.
Source mdau niliyeko mhmbili hosp
 
JK haelewi kinachoendelea yuko kimya. Source mdau niliyeko mhmbili hosp[/QUOTE said:
Wale mapapalazi wa TBC wapo wapi wanatakiwa wafike hapo ili kurusha taarifa kama hii???

JK na Serikali yake LEGELEGE hata hawashituki; mtoto wake akiumwa anampeleka nje ya nji.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!!
 
Yeah hiyo ndiyo hal i halisi hapa. Leo tumeamua kufunga kabisa hata emergency zote. Sasa majeruhi wakipokelewa wapelekwe wapi? Wakati MOI hakina kazi?
Wahudumu Wa afya nao wameingia kwenye mgomo sasa hapo ni mpaka kieleweke.
 
Tusubirri tuone mtoto wa mkulima atatoa cv ya nani leo baada ya kutoa ya Dr. Ulimboka jana
 
Pinda alikua anabweka jana weeeeeee akidhani anaongea na watoto asijue ananena na watu wenye si tu akili bali taaluma zao which are deadly needed everywhere in the world. Sasa amelikoroga ni lazzima alinywe.

Muhimbili hali ni mbaya balaaa na leo hakuna cha huduma ya dharura. Madaktari hakikisheni serikali inalicheza dhumari lenu na si nyinyi kuimba nyimbo za serikali! I wishi na walimu wangekua kama nyinyi coz nao wanasumbuliwa na utii wa woga.
 
Nataka kuona picha jamani mlioko huko maana tunapata taarifa nyingi tu humu ila hazina uhalisia wa kile kinachosemwa.
 
Huu ni uongo, nipo Muhimbili na huduma zinaendelea vizuri.
Madaktari wanawajibika kama kawaida.
Wale walioandaliwa iwapo mgomo ungeendelea wameombwa wasubiri kwanza.

Tuwe na ustaarabu wa kuweka ukweli kwenye jamvi.
 
Yeah hiyo ndiyo hal i halisi hapa. Leo tumeamua kufunga kabisa hata emergency zote. Sasa majeruhi wakipokelewa wapelekwe wapi? Wakati MOI hakina kazi? Wahudumu Wa afya nao wameingia kwenye mgomo sasa hapo ni mpaka kieleweke.
Mimi ninaunga mkono, lakini ikiwa ni kweli hospitali zimefunga sehemu za dharura, nadhani maadili ya mgomo kwenye sekta ya umma yatakuwa yamekiukwa.

Ninavyoelewa, wafanyakazi wa sekta za umma wakigoma, huwa wanapanga kuwepo na asilimia fulani ya huduma. Sasa ikiwa madaktari mmeweka huduma zero, mtakuwa mnakiuka maadili ya kazi yenu.
 
Back
Top Bottom