Wagombea wa UVCCM mkoa wa Iringa waingia mitini kuthibitisha umri wao

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,617
WAGOMBEA WA UVCCM MKOA WA IRINGA WAINGIA MITINI KUTHIBITISHA UMRI WAO , KAMANDA WAO NA KATIBU WA CCM MKOA WATOA YA MOYONI ......




Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiwaomba wajumbe wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea kutenda haki katika kupendekeza majina



Mwanahabari na Mwanachama wa UVCCM Bi Tumain Msowoya ambaye ni mgombea nafasi ya kiti UVCCM mkoa wa Iringa




Mwanachama Geofrey Lukuvi anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa wa Iringa




Mwanachama Fauzia Jemedari anayegombea kiti




Mwanachama Gaudence Kabwabwalika anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa




Hawa ndio wagombea wa nafai ya UVCCM na ndio vijana wenyewe wa CCM


SAKATA la kashfa nzito kwa wana chama wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kutuhumiwa kudanganya umri wao wa kuzaliwa limechukua sura mpya baada ya idadi kubwa ya vijana waliojaza fomu za kuomba nafasi mbali mbali katika UVCCM kukimbia kikao cha usaili kwa wagombea hao.

Huku kamanda wa umoja wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emmanuel Mteming'ombe wakipigilia msumari kwa kutaka haki itendeke katika kuchuja majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali bila kuwepo upendeleo wowote na wale waliochakachua miaka kuwajibishwa .

Hatua hiyo imekuja baada ya mtandao huu kuibua siri nzito ya robo tatu ya vijana hao kujaza umri wa uongo ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma miaka ya kuzaliwa ili iweze kuendena na kanuni ya UVCCM inayomtaka mgombea kuanzia miaka 14-30. Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu juzi wakati wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya UVCCM mkoa wa Iringa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa chini ya mgeni rasmi kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas.

Sehemu kubwa ya wanachama hao walioojaza fomu hizo kushindwa kutokea katika kikao hicho nyeti cha kuhakiki taarifa walizojaza katika fomu zao za kuomba nafasi mbali mbali.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wanachama zinadai kuwa walioshindwa kutokea katika kikao hicho ni baadhi ya wale wanaodaiwa kufanya uchakachuaji wa umri katika zoezi la ujazaji wa fomu hizo . habari kamili tafuta gazeti la Tanzania Daima kesho ama hapa



 
Back
Top Bottom