Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2008
- 15,323
- 10,063
Kila kukicha tunasikia malalamiko ya wafungwa nchini mwetu kuhusiana na lishe mbovu. Mimi nina wazo na wadau wa JF naomba tulijadili:
Kwa kuwa bajeti ya serikali inatengwa kwa ajili ya kila mfungwa kwa mlo wake wa siku,na kwa kuwa kiwango hicho kinajulikana,basi ni bora uwekwe utaratatibu wa kupata makandarasi wa nje (catering outsourcing) ambao watakua wanapika chakula nje ya magereza lakini chini ya usimamizi wa askari magereza na baadae kubeba hicho chakula na kuwagawia wafungwa. Kwa utaratibu huu itajulikana kabisa gereza lina wafungwa kadhaa hivyo zipelekwe sahani kadhaa za chakula ambacho kitakuwa ni kwa mujibu wa official ration ya mfungwa,mathalan wali,maharage,mchicha,kipande cha tunda etc. Nashauri hivi kwa sababu inasemekena on paper wafungwa huwa wanapewa vyakula vyote hivi ingawa physically hawavioni. Wadau mnaonaje wazo hili,si litasaidia kuondoa udokozi na kuwaongezea lishe wafungwa wetu?