JF Toons
Digital Art by JF
- Feb 19, 2024
- 32
- 66
Serikali imeweka utaratibu wa kuhakikisha huduma muhimu ya chakula na lishe inapatikana kwa Wanafunzi wa elimu ya msingi.
Kulingana na Mwongozo wa Kitaifa wa Utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe kwa Elimumsingi, wazazi na Wadau wanatakiwa kuchangia vitu mbalimbali ikiwemo;
- Chakula
- Mafuta
- Sukari
- Chumvi pamoja na mahitaji mengine ya kupikia
- Posho ya mtunza stoo
Hii yote ni katika kuhakikisha Wanafunzi wanapata huduma hiyo muhimu wawapo Shuleni.
Je, ulikuwa unafahamu kuhusu hilo? Kwa kiasi gani wewe Mzazi/Mlezi unatekeleza wajibu huu?