Wafugaji ‘wampigia magoti’ Waziri Mkuu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
pindaloliondo.jpg
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda​



Esther Mwimbula, Kilosa
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ameombwa kusitisha operesheni ya uhamishaji wa mifugo inayodaiwa kuingizwa na wafugaji kiholela katika mikoa mbalimbali nchini ili kupisha msimu wa kilimo na kuepusha migogoro baina ya wafugaji na wakulima wakati wa kuhamisha mifugo hiyo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji Kanda ya Mashariki (uwakama), Shema Jiji alitoa ombi hilo alipozungumza na wafugaji wa jamii mbalimbali wakiwamo wamasai, wamang’ati na wasukuma iliofanyika Wilaya Kilosa.

Mkutano mkuu wa wafugaji hao uliwashirikisha wajumbe kutoka Mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga.
Jiji alisema utekelezaji wa zoezi hilo utawapa ugumu wafugaji kutokana na maeneo mengi ya kupitisha mifugo kujaa maji katika kipindi hiki ambacho mvua zimekuwa zikinyesha nchini.

Alisema kuwa mbali na barabara nyingi wanazozitumia kwa ajili ya kusafirisha mifugo yao kujaa maji, lakini pia wakulima katika maeneo mengi tayari wameanza msimu wa kilimo kwa kupanda mazao yao mbalimbali ya chakula na biashara kwa ajili ya msimu wa kilimo hivyo upitishaji mifugo katika maeneo hayo utachochea vurugu na kutoelewana baina ya wakulima na wafugaji kutokana na mifugo hiyo kula na kuharibu mazao yao .

Aidha alisema kuwa chama hicho cha Umoja wa Wafugaji Kanda ya Afrika Mashariki chenye jumla ya wanachama wafugaji zaidi ya 300 kiliamua kuitisha mkutano huo mkuu kwa ajili ya kujadili matatizo mbalimbali yanayowakabiliwa wanachama wa umoja huo.

Alisema wafungaji kwa pamoja wanamwomba Waziri Mkuu kusitisha zoezi hilo kwa sasa ili kupisha kipindi cha msimu wa kilimo kipite kwani pia itawasaidia baadhi ya wafugaji waliojikita katika kilimo kuendelea na kukamilisha shughuli mbalimbali.

Jiji alisema Serikali inapaswa kutumia busara zaidi ili iweze kutekeleza agizo hilo la kuirudisha mifugo ilikotoka kwa kupisha msimu wa kilimo (masika) ambao wakulima nchini wamekuwa wakiutumia kwa ajili ya kuandaa mashamba kwa kupanda mazao yao mbalimbali ya chakula na biashara ili kuepusha uharibifu unaoweza kutokea kwa kupitisha mifugo katika maeneo hayo ambayo kwa sasa wamekuwa wakiyatumia kama mashamba yao.
chanzo.
Wafugaji ?wampigia magoti? Waziri Mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom