Mbunge Salim Atoa Onyo kwa Polisi Ulanga/Mahenge

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham ameliomba jeshi la Polisi wilayani humo kuacha kuwaonea wananchi jamii ya wakulima pindi wanapopeleka kesi za wafugaji kulisha mifugo katika mashamba yao badala yake wawasaidie kupata haki zao ili kupunguza mvutano kati ya jamii hizo mbili.

Mbunge Salim ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata za Ketaketa na Ilonga alipofika kusikiliza kero za wananchi waliolilalamikia jeshi la polisi kuwa halitendi haki katika kesi zao hata kama wakikamata ushahidi na badala yake watuhumiwa wanaachiliwa huru na kupelekea changamoto hiyo ya wafugaji kuendelea kufanya uharibifu huo mara kwa mara na wakulima kupata hasara kila mwaka.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Ulanga Imani Mlyapatali amesema ni kweli jeshi hilo limekuwa likilalamikiwa sana na wananchi hivyo ameagiza wajitathimini kabla ya uongozi wa juu haujaingilia kati kuwachukulia hatu kwani kumnyima haki mwananchi ni uvunjifu wa sheria na inawezakupelekea machafuko katika jamii hizo mbili.

Wilaya ya Ulanga inakabiliwa na changamoto ya wakulima na wafigaji katika vijiji kadhaa kutoka na mifugo kuwa mingi kuliko maeneo rasmi ya malisho ambayo yametengwa hivyo kupelekea wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.

WhatsApp Image 2023-11-17 at 18.34.32(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 18.34.31.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 18.34.32.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 18.34.32(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-17 at 18.34.34.jpeg
 
Back
Top Bottom