Wafuasi wa Lowassa na CHADEMA, hawajui wanafuata nini

Nimefikiria akili za hawa wafuasi wa huyu mtu aliekatwa nimegundua ni kama nyumbu tu wale wa serengeti ambao hufuata mkumbo tu bila hata kujua wanakwenda wapi na kwa nini wavuke mto sehemu ya hatari wakati sehemu salama ya kuvuka ipo

mbona 2010 ccm ilimteuwa kugombea ubunge monduli na rais alipita monduli akamnyanyua mkono kwamba ni jembe?

logically ccm wote ni manyumbu yale ya serengeti,rwaha,mikumi,ngorongoro,na kwingineko
 
nimefikiria akili za hawa wafuasi wa huyu mtu aliekatwa nimegundua ni kama nyumbu tu wale wa serengeti ambao hufuata mkumbo tu bila hata kujua wanakwenda wapi na kwa nini wavuke mto sehemu ya hatari wakati sehemu salama ya kuvuka ipo

mlitegemea nini mlivyomkata jina bila kumsikiliza?hamkujua yeye ana wafusi wengi ndani na nje ya ccm?mtakoma sasa
 
Nimefikiria akili za hawa wafuasi wa huyu mtu aliekatwa nimegundua ni kama nyumbu tu wale wa serengeti ambao hufuata mkumbo tu bila hata kujua wanakwenda wapi na kwa nini wavuke mto sehemu ya hatari wakati sehemu salama ya kuvuka ipo

Low thinking capacity! Unashindwa kujenga hoja unaonesha ulivyo na IQ ya chini mno kuweza kujadili mambo ya siasa better stay quiet
 
Lowasa Rais kama hutaki utataka na utaungana nasi ni suala la Muda tuu
 
Kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi juu ya jambo Fulani kama alivyofanya Lowassa kwani sisiem siyo chama cha mama yake wala bibiyake.Sioni kwanini ahukumiwe kwa maamuzi yao mbona wap wengi wamehamatioka chama kimoja kwenda kingine mf.Letecia Nyerere-CDM-CCM,Lembeli-CCM-CDM n.k kwanini wao hawajadiliwi au hawana madhara kwenye mchakato ama kweli kweli sisiem wamechelewa kujenga woga badala yae watulie watumikie maamuzi magumu waliyoyafanya Dodoma siku chache zilizoisha!!!!!!!!!!!
 
Nimefikiria za hawa wafuasi wa huyu mtu aliekatwa nimegundua ni kama nyumbu tu wale wa serengeti ambao hufuata mkumbo tu bila hata kujua wanakwenda wapi na kwa nini wavuke mto sehemu ya hatari wakati sehemu salama ya kuvuka ipo

Je unayaamini hayo unayoyasema????? mbona umesahau kutuambia hao wa chama cha zamani akili zao nao ni za wanyama gani wakule mbuga za saanane au ni za mikumi
 
Je unayaamini hayo unayoyasema????? mbona umesahau kutuambia hao wa chama cha zamani akili zao nao ni za wanyama gani wakule mbuga za saanane au ni za mikumi

Unamkumbuka kibwetere
 
Umeona eeh, jamaa hawajitambuı na n wakurupukajı.Niliamını CDM ila nimeachana nao kwa upuuzi wa Mbowe.Nabaki kuwa mtu huru sıtakı kuwa na chama cha siasa mpaka kıtokee chama chenye watu wakwelı.
haujawai kuwa mwanachadema usituzuge hapa
 
Were uko upande gani mpaka ujue wafuasi hao wanachotaka?Umekuwa Mungu kujua fikra za watu,period!
 
Khaa.. Unafanananisha kuvuka kwa nyumbu..! Wao ndo wameona kivuko kizuri ni hapo, haijalishi kuna maji mengi au laa.. Kwa kuwa hawana vipimo.. We ulitaka wakavukie wapi? Basi kamwambie maufunguo akawajengee daraja...
Khaa.. Hebu niache kuchangia maada ya mtu aliyetukana wenzake, kifuatacho ni kurudishiana, ngoja tuone upepo tayari, karibuni tu hapa, tutaziona #Nyeti
 
Acha Matusi ya namna hiyo weka hoja tukuelewe.
hakuna hoja inayowafaa, NYIE NI KAMA NYUMBU KWELI. mngekuwa na hoja msingekuwa mnahama kwa makundi bila kujua mnakoelekea. Tanzania haiwezi kufikia mageuzi ya maana ikiwa na kundi kubwa la wajinga kama nyie. Hakuna cha hoja kwa watu wapumbavu kama nyie. Mnakuwa kama mnacheza ule mchezo wa nyama nyama nyamaa, ya kuku nyama, ya ng'ombe nyama ya fisi nyama. Mpaka msituke mlishatoka wote ktk mchezo
 
Jana alikuwa anagombea CCM, kesho yake anagombea UKAWA. Hivi kweli miaka takriban 15 sasa ya upinzani nchini, hajapatikana mgombea mwenye credebility ya upinzani, na sio mamluki kama tunavyoshuhudia sasa? Kweli kabisa Dr. Slaa namwelewa vizuri kama kweli kasusia. Yaani haiingii akilini, eti wasomi kama ma profesa wa ukawa, madaktari wa sheria na kadhalika. Wanampokea mamluki na kumfanya kiongozi wao. Si ataiuza hata nchi huyu???
 
ningewashangaa Sana ccm kama mngemshabikia lowasa kuamia UKAWA! Najua upo kazini, ila watanzania tumeshahamka hatuitaki ccm tumewachoka majizi nyinyi, sumu yako kamwage baharini hapa hupati mtu! Upo we panyaroad??

Kaka acha matusi ndugu yangu, nimesoma quotes zako nyingi sana zimetawaliwa na matusi. Hapa kwenye hii forum kila mtu yuko huru kuandika mawazo yake, lakini siamini kama kila mtu yuko huru kutukana wengine. Mimi na wewe tunaweza kuwa na itikadi tofauti za kisiasa, lakini huna ruhusa ya kunitukana. Ongea hoja za msingi lakini sio matusi. Hata mimi najua sana kutukana lakini sioni sababu ya kufanya hivyo hasa ikizingatiwa kuwa hili sio jukwaa la MATUSI.
 
Lowasa kawahi sasa hawa wengine kula za maoni za chadema watakuwemo? maana chadema walisha jipanga
 
attachment.php
 
Back
Top Bottom