Wafanyakazi wengi serikalini kumpigia kura JP Magufuli

Njanga Tz

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
843
653
Habari wakuu,
Leo nimehitimisha kufanya utafiti wangu binafsi usio rasmi.

Katika research yangu hii nilikua na maswali madogo mawili,
I. Je utampigia kura nani?
II. Kwanini utampigia kura?

Utafiti huu usio rasmi ulihusisha watumishi waserikali tu haswa waalimu na wafanyakazi wa halmashauri.

Siweki graph piechart wala lines ila kwa swali la kwanza asilimia kubwa walijibu watamchagua JP Magufuli.

Kwanini watamchagua Magufuli? Jibu la wengi lilifanana, ni kwamba akiingia Lowasa hawatakua huru ataturudisha 2006/2007.

Swala la sera za chama na maslahi ya taifa havikugusiwa ila ishu kubwa jamaa ni pilipili sana. TAFAKARI CHUKUA HATUA.

# Magufuli 2015
# Lowasa 2015
 
Ngojea waje hao wafanyakazi wajibu ili huo utafiti uuendeleze na majibu ya hapa
 
hao wafanyakazi wapo wangapi??
alafu wasio waajiriwa au watumishi wa serekali wako wangapi?
angalia usijekua kama twaweza?
subirini25oct
 
Wewe unazungumzia wafanyakazi gani? Ambao watampigia Magufuli ni Wakurugenzi, maafisa waliopewa vyeo ambao hawazidi 15% ya idadi ya watumishi wote, kama ndio uliowahoji in sawa lakini hakuna watumishi wengine watakaomchagua Magufuli.
 
Wewe jidanganye tu. Unawatafuta mahousegirl wa wafanyakazi unadai ndio wafanyakazi wa serikali. Makufuri yataishia milangoni kuzuia pombe za Joni na Josefu, lakini Safari hii ukweli utakuuma sana maana Lowasa ndiye rais wako kuanzia 26 Octoba. Sawasawa?
 
mhhh wameogopa tu kusema ukweli kwa kuhofia vibarua vyao mioyoni mwao wanaujua ukweli
 
Watanzania wenye akiri wote na tunaojituma kazini tunapenda wachapa kazi ..ila kama vipi subirini Oktoba tukapige kura
 
Habari wakuu,
Leo nimehitimisha kufanya utafiti wangu binafsi usio rasmi.

Katika research yangu hii nilikua na maswali madogo mawili,
I. Je utampigia kura nani?
II. Kwanini utampigia kura?

Utafiti huu usio rasmi ulihusisha watumishi waserikali tu haswa waalimu na wafanyakazi wa halmashauri.

Siweki graph piechart wala lines ila kwa swali la kwanza asilimia kubwa walijibu watamchagua JP Magufuli.

Kwanini watamchagua Magufuli? Jibu la wengi lilifanana, ni kwamba akiingia Lowasa hawatakua huru ataturudisha 2006/2007.

Swala la sera za chama na maslahi ya taifa havikugusiwa ila ishu kubwa jamaa ni pilipili sana. TAFAKARI CHUKUA HATUA.

# Magufuli 2015
# Lowasa 2015

Hebu jifunzeni kufanya propaganda zenye mashiko na uhalisia
 
Back
Top Bottom