WAFANYAKAZI wa migodi wametaka Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) irudishwe bungeni kwenye mkutano ujao ili kipengele cha fao la kujitoa kiondolewe mara moja.
Mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jana, wafanyakazi hao walisema kuwa kupelekwa sheria katika Bunge lijalo kutasaidia kupata haki na si kusubiri miaka 55 wakati migodi mingine imeanza kufungwa.
Mwakilishi wa Katibu wa Chama Wafanyakazi wa Migodi na Viwanda Tanzania (Tamiko), Benjamin Dotto, alisema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa wafanyakazi wa migodi huku fedha yao ikitumika kutekeleza miradi ya serikali ambayo haina faida kwa wafanyakazi.
Dotto alisema kuwa wafanyakazi wa migodi wanafanya katika mazingira magumu hali ambayo fedha zinaweza kuwasaidia katika maisha kutokana na athari zinazotokana na sumu ya migodi, kwamba hawana uwezo wa kufika miaka hiyo kama sheria inavyosema.
Aliongeza kuwa msimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii atokane na wafanyakazi ili aweze kusimamia haki na sheria zinazomnufaisha mfanyakazi.
Wafanyakazi wa migodi wako katika mazingira magumu kutokana na kazi wanazofanya ambapo hawawezi kusubiri miaka hiyo ambayo sheria hiyo inataka huku wakiwa wameathirika na migodi, alisema Dotto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wachimba Migodi, Joseph Mgire, alisema kuwa amani itatoweka kama sheria hiyo haitatekelezwa katika wakati muafaka.
Mgire alisema kuwa wafanyakazi wa migodi wako katika mikataba ambayo haieleweki kutokana na makampuni hayo wakati wowote yanaweza kufungwa na kulazimika kusubiri miaka 55 kuweza kupata mafao yao.