Tetesi: Wafanyakazi Shule Maarufu Tabata- Dar es Salaam Kugoma Muda Wowote

DolphinT

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
1,308
1,828
Hizi ni tetesi zilifika hivi punde kwamba wafanyakazi katika shule maarufu huko Tabata Dar es Salaam kugoma muda wowote kuanzia sasa hali inayotishia kuhatarisha zoezi linaloendlea la mitihani ya kitaifa wakitaka kuushinikiza Ungozi wa shule na menejiment kusikiliza kero zao za muda mrefu ambazo zinawaathiri wafanyakazi, wanafunzi na kuathiri pia matarajio ya wazazi.

Shule hiyo maarufu ambayo kwa historia imehudhuriwa na watoto wa vigogo na watu maarufu nchini inalamikiwa kushindwa kulipa mishahara na stahiki za wafanyakazi kwa wakati wakiwemo waalimu, madereva, wapishi walinzi na wafagizi huku wamiliki wakendelea kuogolea katika ukwasi uliotopea na kushindwa kujitokeza kutoa taarifa au kauli juu ya hali hiyo ambayo imekua ikijitokeza mara mara kwa mara kwa maiak miwili sasa.

Huku hayo yakiendelea taarifa zilizofikia chanzo cha kuaminika cha habari ni kwamba shule hiyo ambayo inatoza kiwango kikubwa cha ada kwa wanafunzi kuanzia chekechekechea shule ya msingi na sekondari , huduma zake haziendani kabisa na kiwango cha ada hiyo ikujumuisha huduma mbovu za chakula, sehemu ya kulia chakula pamoja na maswala ya michezo na buriudani kwa wanafunzi kwani shule hiyo haina kabisa viwanja vya michezo na hakuna utaratibu wa kuwapeleka wanafunzi katika shule za michezo hali ambayo imezua taharuki pia kwa wazazi wanaosomesha wanafunzi katika shule hiyo.

Hali kadhalika jambo la kustukiza ni kwamba Aliyekua mkuu wa shule ameondolewa katika mazingira ya kutatanisha na shule kukabidhiwa kwa kijana mdogo ambaye kwa historia yake anazidi kuongeza wasi wasi kwa wazazi na walimu kwa kuzingatia kwamba hana uzoefu katika uendeshaji wa shule na amekua akiwatishia walimu waliopo kuwafukuza kazi au kuwapangia kazi za usafi na usimamizi wa mabweni hali inayotishia kumtia Mmiliki wa shule hiyo katika mgogoro wa kiutumishi kwa musjibu wa sheria za kazi na ajira na mahusiano kazini.

Imeelezwa kwamba shule hiyo kwa sasa imekua chaka la kupitishia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na tassisi hiyo ikiwemo kandarasi za ujenzi wa miradi ya serikali hivyo kuifanya kushidwa kulipa mishahara kwa wakati hali kadhalika kushindwa kutopeleka michango ya hifadhi ya jamii (NSSF) NA Bodi ya Mikopo pamoja na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.

Wakati Mmiliki wa shule hiyo akilalamikia upungufu wa wanafunzi kuwa chanzo cha kupungua kwa mapato imeelezwa kwamba anaendelea kajiri walimu kwa gharama kubwa bila kuzingatia mahitaji, ufanisi na ubora pamoja nagharama, hivyo kumlazimisha mkuu wa shule mpya aliyepo kutaka kuwapunguza wafanyakazi na walimu waliopo bila kuzingatia sheria na kanunu za utumishi.

Mzazi mmoja amabaye ana watoto takribani watano katika shule hiyo analalamikia utaratibu usio rafuki uliowekwa na Mkuu mpya wa shule ambaye amekua na kauli tata kwa wazazi, walimu na wanafunzi, anaaeleza kwamba wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne mwaka huu hawana nia ya kurudi shuleni hapo mwakani kwa ajili ya kidato cha tano, huku walioko kidato cha tano, cha tatu na cha nne wakihama kwa visingizio mbalimbali.

Licha ya mmiliki wa shule kuitisha vikao ili kutuliza taharuki hiyo miongoni mwa wafanyakazi, walimu na wanafunzi hali imeendelea kuwa mbaya huku kukiwa hakuna hatua mahususi zinachokuliwa na menejiment kutuliza hali hiyo ya hewa inayovuma kwa sasa. Wafanyakazi walimu na wazazi wanatoa wito kwa menejimenti na Bodi ya shule kuangalia swala hilo kwa upana na kwa haraka kabla hali haijawa mbaya hasa katika kipindi hiki cha mitihani ya taifa kwani wamefika kiwango cha mwisho cha uvumilivu huku wao wakikaa kimya bila kutoa taarifa huku wakitaka mkuu wa shule aliyepo aondolewe mapema iwezekanavyo.
Jina la shule limehifadhiwa kwa sababu maalumu kwa kuwa hizi bado ni tetesi.
 
Hilo neno itaathiri mtihani ya kidato Cha 4,sio kweli, kwani hao walimu ndio wanasimamia huo mtihani ?,mtihani ni kitu sensitive sana ukijaribu kuleta vurugu au kitu chochote kitakachoathiri mtihani kutofanyika lazima uishie jela utashtakiwa kwa Sheria ya uhujumu uchumi na Sheria namba 3 ya mwaka 1970 ya usalama wa Taifa pamoja na Sheria ya Baraza la mitihani ya mwaka 1973.
 
Back
Top Bottom