Wafanyabiashara wataka umeme wa Buzwagi............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Wafanyabiashara wataka umeme wa Buzwagi

Imeandikwa na Raymond Mihayo, Kahama; Tarehe: 13th December 2010 @ 23:20

WAFANYABIASHARA wa viwanda na mashine za kukoboa mpunga, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wameiomba serikali kuharakisha mazungumzo yake na uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi ili wilaya iweze kupata umeme wa uhakika kupitia katika mgodi huo.

Wafanyabiashara hao waliyaeleza hayo katika kikao chao na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bahati Matala.

Walisema pamoja na kilio chao hicho cha muda mrefu, uongozi wa juu ukiwemo ule wa Shirika la Umeme nchini(Tanesco) Wilayani hapa umekuwa ukifumbia macho.

Akisoma risala kwa niaba ya wafanyabiasahara hao , Hamis Makune alisema kwa sasa kumekuwa na ukatikaji wa umeme kiasi cha mara tano kwa siku hali ambayo inaathiri utendaji wao wa kazi katika mashine za kukoboa mpunga na hivyo kupunguza kipato chao.

Makune alisema kuwa ukatikaji wa umeme huo ambao hutokea bila ya kupewa taarifa na Tanesco kunaweza kusababisha uharibifu wa mashine zao na kuleta hasara kwa wamiliki wa viwanda.

Hata hivyo Makune alisema pindi wanapopata umeme wakati wa usiku Polisi huwakamata wafanyabiashara hao na kuwazuia kufanya kazi hali ambayo inawatia hasara katika biashara yao hiyo.

“Tunaomba Mkuu wa Wilaya kama kuna uwezekano ujaribu kuzungumza na uongozi wa Mgodi wa Buzwagi ili kuona kama kuna uwezekano wa kuunganisha umeme katika mgodi huo hadi kwa wananchi wa wilaya hiyo ili kupunguza tatizo hilo”, alisema Makune.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Matala alilitaka shirika la umeme , Tanesco, kuangalia jinsi ya kuliondoa tatizo hilo ili wafanyabiashara waweze kufanya kazi zao kama ilivyokuwa awali.

Nae Kaimu Meneja Tanesco Wilaya ya Kahama, Kitila Brayson alisema kwa sasa shirika lake linafanya jitihada kuondoa tatizo hilo ambalo linasababishwa na baadhi ya transfoma tatu
katika maeneo ya Mwendakulima, Kagongwa na katika eneo la Wachina .
 
Upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya ukapa wa umeme na ufisadi ndani ya Tanesco..............
 
Back
Top Bottom