Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

Theme ni albamu, ila umetupeleka chumbani, sebuleni yaani ilimradi basi tu.
 
Kumbukumbu nzuri enzi hizo mpira wa makaratasi sodo anayo mtu mmoja, huyo uwanjani hamtakiwi kumkanyaga na yeye ndio anapanga nani acheze au asicheze na mkimkanyaga mpira anaweka kwapani na mchezo unaishia hapo, au ilikua lazima mkamsaidie kazi kama kuteka maji au kuosha vyombo ili muwahi kwenda kucheza
Maudhui ni album na TV zamani
 
Daaaah! Basi enzi hizo mambo yalikuwa ni fire najaribu kuvuta picha vijana na watoto wa enzi sijui mlikuwa na muonekano wa Aina gani? Naipenda sana historia ya Tanzania Kuna kitu najifunza.Bila kusahau redio Tanzania RTD.daaah kweli ya kale ni dhahabu ngoja nivute kiti nikae ndio Kwanza mjadala umepamba moto
 
Jamani tuacheni tupumue!
Uzi una mambo ya zamani tunajikumbusha mnauharibu kwa ulimbukeni wenu!
Yaan utaona Uzi unabadilikia hewan sasa hivi tabia inakera sana hii kwnn MTU asianzishe Uzi wake wa nireeten gwajima na tulia inakera sana mkuu
Kitu kinaongelewa hata hakihusiani.
 
nakumbuka mzee alikua na video tapes za enrique iglesias kulikua na videos kama bilamooooooos, sad eyes, maria maria za kina santana,kina britney spears, mzee alikua anamkubali sana enrique mpaka akaniambukiza na mimi! kipindi hicho pierce bosnan ndo alikua james bond!!!!! mpaka leo hii hizo ngona naskiliza! i realy miss me
We umezaliwa elf mbili na ngp?? Maana huyo nwrique naye kijana tu
 
Mpiga picha ktk eneo letu (maana Ni zaidi ya mtaa ingekuwa kijijini tungesema Kijiji kizima) alikuwa anaitwa Said,ili umpate siku ya sikukuu uweke booking almost mwezi kabla, na akija anapiga dakika chache anaondoka, pozi uliloweka ndo hilohilo utakuja kuhakiki Kama ulikaa vzr au ulifumba macho picha ikitoka, haina take 2, alikuwa na baiskeli Yake, akikupiga Leo picha analeta baada ya wiki, na ikitokea unamghasi anakwambia mkanda haujajaa, mpaka mkanda ujae ndo akasafishe, akiona KERO zinazidi anakwambia zimeungua huna pa kushtaki, walikuwa ni masupastaaa sana. Wametafuna sana mademu
 
Miaka ya themani karibia na tisini tulikuwa tunaenda kucheck movie kwa mwasi pale kinondoni studio na pia tulikuwa wakati mwingine tunaenda kucheck movie za charlie chaplin kwa wafrika kusini wao walikuwa wako bongo kama wakimbiz (freedom fighters)
Wao sasa walikuwa wanatonesha sinema kwenye ule mdude kama projector
Infantry Soldier enzi hizo watoto wa uswaz tulikuwa tunaonekana wajanja kuazimana mikanda ya sinema lkn cha ajabu tv hatuna
Jiulize sasa hizo tape tulikuwa tunapata wapi?


Ova
 
Namkumbuka mpiga picha maarufu aliyekuwa anatupiga hizo picha enzi hizo miaka yote akiwa na bicycle yake ya Swala, kwa sasa ni Afisa Elimu wa mkoa fulani.. baada ya kujiendeleza, alikuwa na juhudi sana yule mheshimiwa
 
Hahahahaaaa noma sana mkuu. Ukitaka kuiangalia "nega" unaielekeza kwenye mwaga wa jua hivi aisee...
Nlikuwa na kikamera unachomeka picha unangalia hku unabonyeza picha zinasogea
Kuangalia pesa nlikuwa sikosi hela ....alinipaga baharia mmja zamani vitu vizuri na nadra watu kuwa navyo walikuwa navyo mabaharia wa melini

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom