Wadada Mpo?

Stephano

Member
Dec 30, 2008
27
4
Wanajamii nimezungukaaaaa na kutumika sanaaaaa sasa naamua kutulia. tatizo langu ni wadada waliotulia wanapatikana wapi?
 
Una uhakika kwamba unataka kutulia kweli au umeamua kubadilisha njia ya kuchezea dada zetu,au unataka kubadilsha ladha ili uone ladha ya hao wanaosemekana kutulia ikoje,kwa sababu mabinti waliotulia wapo kila mahali hata hapo ulipo wapo kibao
 
kaka sio kazi rahisi unavyodhania, hawa jamaa wamebadilika sana hawapatikani, waliotulia wamekuwa bidhaa adimu
 
Wanajamii nimezungukaaaaa na kutumika sanaaaaa sasa naamua kutulia. tatizo langu ni wadada waliotulia wanapatikana wapi?

Angalia nyumba za jirani yako hapo,hiyo ya mbele,ya kushoto na ya kulia kwa nyumba yenu mojawapo ya nyumba hizo ina binti mzuri tu kwa tabia,umbo na sura,nadhani atakufaa,sasa sijui kama wewe utamfaa ama la...Be blessed mkuu
 
Ulimwengu wa sasa utulivu sifuri mdada jmosi anafunga ndoa alhamis unashangaa jamaa kala.
Si angalau ungemueshimu mwenzio angalau ata baada ya harusi,yaaani nilichoka.
Watulivu wapo ila ni nadra sana kuwapata.
Mtegemee mungu ktk ilo
 
Wanajamii nimezungukaaaaa na kutumika sanaaaaa sasa naamua kutulia. tatizo langu ni wadada waliotulia wanapatikana wapi?

Stephano;

Waliotulia wanapatikana hukohuko walipotulia, nenda utawakuta na wao wametumika sanaaa kama wewe na wakamua kutulia
 
Wanajamii nimezungukaaaaa na kutumika sanaaaaa sasa naamua kutulia. tatizo langu ni wadada waliotulia wanapatikana wapi?

Ndugu waliotulia walishapanda usafiri wa kaburi na kwa sasa wapo mbinguni, hapa duniani tulipo ni sehemu ya changamoto, misukosuko, matatizo, makasheshe n.k. ambayo sisi sote tunatakiwa kukumbana nayo na kuyatafutia suluhu; na pale ambapo suluhu inapatikana ndipo tunafurahia matunda japo hata ni kwa muda fulani tu. Hata hao ambao wanaweza kuwa wanafikiria kuwa wamewapata waliotulia huenda ni kwa sababu siyo rahisi kubaini vile vyote avitendavyo mwenzi wako, na laiti kungekuwa na uwezekano wa kubainika, basi wangejikuta wanahukumu kuwa hajatulia; na ndiyo maana kuna wakati unasikia kwnye mahusiano mtu anakuja kusema -SIKUTEGEMEA KAMA UKO HIVYO-. Cha msingi katika mahusiano ni uwepo wa staha/uvumilivu na kusameheana ndiko haswa kunafanya kuwa na mwonekano wa kwamba fulani amempata aliyetulia. Vinginevyo kidume na wewe kwea usafiri uende huko kwenye utulivu, Mbinguniiii kwa Baba
 
Mh... Shukran sana kwa i'lmu kubwa
 
waliotulia hawapatikani kwa matangazo hayo uliyofanya,wanapatikana kiutulivu pia.Utakayempata kwa mtindo huu naye inawezekana hajatulia pia.mwombe mungu
 
Una maana gani ya KUTULIA? Maana kwangu suala sio utulivu bali 'COMMITMENT'. Bila kujitoa kabisa kwa mwenzako kwa mapenzi ya dhati basi tegemea maumivu mbele ya safari
 
waliotulia WAPO wengi SAAAAAAAAAAANA! La msingi ni kwamba inabidi USITULIE hili uweza kupata WALOTULIA!!! Ukitulia utapa ambao hawajatulia. Reasoning ni rahisi "unlike charges.... and like charges....."

Siku Njema
 
unaweza kuwapata pale AMBIANCE au JOLYS CLUB, tembelea siku moja utawapata
 
Alietulia hutampata labda aliyeweza kujibadilisha kufuatana na mazingira ya mahali na hali husika. Kazi kwako.
 
Kwa kweli MTM umenivunja mbavu na jibu lako, nahisi ndilo limfaalo bro Stephano.

Sasa bro Stephano, wewe umetumikaaaaaa weee, halafu unamtafuta dada wa watu aliyetulia? Ili yeye ukamhadithie nini? Nafikiri angalia ushauri wa MTM mara mbili mbili manake nina hakika utakayempata huko, ndio mtaongea lugha moja....
 
Back
Top Bottom