Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,752
Unategemea Mkulo alivyo kilaza atazingatia yote hayo???Serikali inajidanganya katika suala hili la kodi kwa mashirika ya kidini, yawe ya Kikristo ,Kiislamu au Bohora.
Inaelekea Serikali haijafanya utafiti katika hili na italijutia katika muda si mrefu ujao.
Viongozi wetu wengi wamesoma BURE katika hizi shule. Sasa tujiulize biashara iliyopo pale.
Kikwete kasoma nafikiri Lugoba Seminary,Nyerere ndo kabisa ikiwa ni pamoja na kufundisha shule ya Pugu Seminary.Siyo siri kuwa watakao athirika zaidi na msimamo huu wa kodi ni Kanisa la Katoliki ambalo lina miradi mingi zaidi ya kijamii.
Kwa hili basi serikali inbidi ikubali ya fuatayo-
1)Kanisa libadili msimamo wake wa jadi wa kutoa huduma za kijamii kwa bei nafuu na kufanya kibiashara
2)Kufunga huduma zote zisizoweza kujiendesha kibiashara
3)Hospitali kama KCMC,Bugando sasa ziwe private
4)Shule kama St Francis-Mbeya, Mazinde Juu,Kifungilo Girls,St Marian Bagamoyo ziwe private schools na zitoze ada istahiliyo kama hizi "International Schools " za Dar es salaam
Ni wazi kuwa msimamo wa madhebu yote ya dini ni kinyume na kufanya mambo kibiashara hivyo ufinyu wa mawazo ya kutakiwa kufanya shughuli zake kibiashara utaonekana muda si mrefu
ila hapa nahisi pia kuna kitu nyuma ya pazia na sasa wanajaribu kublow the horn