Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

Ni kweli MF1, tena cha kusikitisha hata watu wa nje wanakuja kutajirikia kupitia taasisi za kidini, wanakuja kwa gear ya kutoa misaada na kuendesha biashara zao wakifanikiwa wanaondoka na kuuza taasisi kwa watu wengine wakidai kuwa wamefanya mabadiliko, taasisi nyingi zinaendeshwa kibiashara, ni magari mangapi yanayoagizwa na taasisi zetu za kidini na ya nasamehewa kodi kumbe ni kwa ajili ya matumizi ya watu binafsi,

hata wafanyabishara wanatumia taasisi za dini kuingiza vitu bila ushuru,

I think it is sheer short sighteedness kwa mtu kuiona miradi mingi ya kidini na kijamii kwa mtindo huu wa jumla ya magari yaliyoingizwa na kodi iliyokosekana.Long term scope ya miradi hii ya kijamii ambayo inatekelezwa na mashirika haya ya kidini ina far reaching impact kuliko kodi inayoweza kupatikana.
Kwa hii leo, kwa level of governance tuliyonayo (na si miaka hii tu ya karibuni) miradi mingi ya kiserikali siyo endelevu ukilinganisha na ile ya kidini, hii ni pamoja na ukweli kuwa wote wanafaidika na misamaha ya kodi.
 
Last edited:
Ati leo wanatishia kuandamana kwa sababu wataondolewa misamaha ya kodi! Leo wamecharuka na kugundua kuwa serikali inaweza kuwafanyizia wakiendelea kupiga kelele. Ati, kwa vile sasa misamaha ya kodi itafutwa kwa taasisi za kidini ukiondoa vitu vya ibada (Biblia, Qurani, tasbihi n.k) ndio wachungaji na mashehe wetu wamecharuka!

Niliwaandikia karibu mara mbili kuwa wamelala kitanda kimoja na watawala na wamefurahia mahaba ya ufisadi. Ni wao wamekuwa wakiwaalika kila kukicha kwenye tafrija zao na kwenye matembezi yao hawakosi. Sasa leo wameanza kupiga kelele dhidi ya ufisadi na dhidi ya uongozi wanatarajia watawala wacheze chioda?

Leo wachungaji na mashehe wanaanza kusimama na kunyoshea kidole ufisadi waziwazi wanatarajia kweli misamaha ya kodi iendelee?

Walichofanya watawala ni kuwabeep hawa! Kwamba wakiendelea na kelele zao dhidi ya viongozi na kunyoshea kidole watawala wajue serikali ina uwezo na ubavu wa kuwafanya walipe!

Sasa uchaguzi ni wao:

a. Wapige magoti kwa viongozi wa serikali na kuwaahidi kuwa wakirudishiwa misamaha ya kodi hawatapiga kelele dhidi ya viongozi (a.k.a kujihusisha na siasa)

b. Waamue kupandisha gharama za huduma zao za kijamii ili waanze kutengeneza faida kama taasisi nyingine za kibiashara na hivyo kuchangia kwenye pato la taifa. Baadhi ya huduma ambazo inabidi waongeze gharama ni pamoja na hospitali, kliniki, mashule na vyuo mbalimbali.

c. Wafunge baadhi ya huduma zao ambazo ni ngumu kujiendesha na kuziunganisha baadhi ya huduma zao kama wafanyavyavyo wafanyabiashara wengine na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

d. Huduma zile za misaada (charity works) zisitishwe na kuacha serikali ifanye shughuli hizo kwa ufanisi vinginevyo wataweza vipi kutoa misaada ambayo wanaigharimia kama bidhaa nyingine. Nani ata offset gharama ya kuingiza, kutunza na kusambaza misaada hiyo. Of course, serikali ina uwezo huo! Sudan walijaribu!!


Upande mwingine ni kuwa serikali isilegeze uzi bali ing'ang'anie msimamo wake tuone hawa wachungaji na mashehe watafanya nini zaidi ya kupiga mikwara. Najua jambo moja msitarajie Pengo kuandamana mitaani!!! Hata kina Kilaini msifikirie wanaweza kusimama na mabango!

I know however, rafiki yangu Khalifa Khamisi wa Kwamtoro na wengine wanaweza kuonekana mitaani! Hawa kina Rev. Whoever hawana ujasiri wa kufanya hivyo!

===========================================

Habari Leo
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini ameishauri serikali kupitia upya uamuzi wa kuyafutia msamaha mashirika ya dini na asasi za kiraia. Akizungumza jana na gazeti dada la Daily News, alisema taasisi hizo hazitengenezi faida na badala yake, zipo kwa ajili ya kuwainua watu wa kawaida ambao ni masikini. Alitoa mfano wa huduma za afya zinazotolewa hususan maeneo ya vijijini, ambazo nyingi hutolewa na taasisi za dini.

"Serikali ilipaswa kukaa na wadau kwa ajili kupata ushauri juu ya hasara na faida ya kuondoa msamaha huo kabla ya kutangaza bajeti yake," alisema Kilaini. Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu (masuala ya dini) wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Mohamed Khamis alisema uamuzi huo unakwamisha sera ya Taifa ya kuwapa maisha bora wananchi.

Alisema taasisi za dini hazitengenezi faida na nyingi zinategemea wafadhili. Alisema inapaswa itoe ruzuku kwa taasisi hizo, ili kuziwezesha kuendesha shughuli zake za kila siku. Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Dk peter Mwamasika, alisema maaskofu wako tayari kuandamana kupinga hatua ya serikali ya kuziondolea taasisi za dini misamaha ya kodi.

Akizungumza jana Dodoma, Askofu Mwamasika alisema hatua hiyo ya Serikali ni ya hatari na inaweza kuleta mtafaruku usio na sababu za msingi na kuendelea kuwapa ugumu wa maisha wananchi wanaopata huduma kupitia shule na hospitali zinazomilikiwa na mashirika hayo ya kidini.

Aliishangaa Serikali ya CCM inavyoanza kubadilisha mwelekeo wa utawala wake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana nayo kuhudumia Watanzania. Aliongeza kuwa KKKT ikiwa sehemu jumuiya ya Kikristo Tanzania, inatambua wajibu wake wa kuhudumia mtu mzima yenye maana ya kiroho na kimwili na ndiyo maana inahudumia kwenye elimu, afya, vituo vya watoto yatima, walemavu na walioko katika mazingira magumu.

Askofu huyo alisema wabunge na mawaziri na hata marais waliotangulia, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, watambue kwamba elimu waliyo nayo na afya walizonazo, zimetokana na vituo vya mashirika ya kidini, hivyo si vyema kudai kuwa ndio wanaochangia kuyumba kwa uchumi wa nchi.

Alihoji: "Iweje leo kwenye karne ya 21 ionekane kwamba mashirika ya dini ndiyo yanayosababisha upungufu wa bajeti ya Serikali wakati mashirika ya dini yanachangia sehemu kubwa ya afya, elimu na huduma zote za jamii?" Alisema kupuuza mchango huo wa mashirika ya dini ni kuanzisha mtafaruku, "kwa hiyo tunawasihi wabunge, mawaziri, wanasheria, Rais watafakari kwa makini jambo hilo."

Askofu Mwamasika alisema serikali kabla ya kutoa uamuzi kama huo ilistahili kwanza kukutana na viongozi wa dini na wazee kama ambavyo alivyokuwa akifanya Rais Julius Nyerere wakati alipotaka kufanya uamuzi mkubwa kama huo. Hata hivyo alisema hotuba ya Rais Jumatano wiki hii alipozungumza na wazee wa Dodoma, ililenga kuwaondolea shida Watanzania na kuinua uchumi wa nchi.

Alisema Taifa liliipokea hotuba ya Rais kwa furaha, kwani ililenga kumkomboa mwananchi wa chini; lakini ya Waziri wa Fedha na Uchumi, iliona namna ya kunusuru uchumi ni kufuta msamaha wa kodi uliokuwa unatolewa kwa mashirika ya dini. "Kwa kweli Waziri wa Fedha amevuruga." Alisema KKKT inapinga hatua hiyo.

"Nasema tunapinga na sisi maaskofu tumekubaliana kuwa kama Serikali haitabatilisha uamuzi wake tutaandamana hadi kwa Rais Kikwete, kwani hatuwezi kukubali watu wetu waendelee kupata shida wakati kaulimbiu ya Rais ni Maisha Bora kwa kila Mtanzania." KKKT ina hospitali 23, zahanati 139 na vituo vya udiakonia 19.

Askofu Mwamasika alisema iwapo serikali itaendelea na uamuzi wake wa kutotoa msamaha wa kodi kwa mashirika ya kidini ina maana hospitali hizo zinaweza kufungwa. Naye Msaidizi wa Katibu wa Jumuiya ya Kikristo (CCT), John Mapesa, alisema alipokea simu nyingi kutoka kwa maaskofu wa madhehebu yanayounda jumuiya hiyo, wakitaka kujua kama jumuiya ifanye nini kuhusu bajeti iliyosomwa na Waziri.

Mapesa alisema kitendo cha serikali kufuta msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini kinarudisha nyumba juhudi zinazofanywa na mashirika hayo kuisaidia jamii wajibu ambao unastahili kufanywa na serikali.

"Madhehebu ya kidini yanachofanya ni kuisaidia serikali, kwa hiyo ni lazima ikubali kuwa taasisi hizi za kidini ni wadau wakubwa wa maendeleo, hivyo ni lazima waendelee kuzilea," alisema Mapesa.

Alisema anaamini serikali itafikiria upya uamuzi huo kwani unalenga kuvunja moyo hata wahisani ambao wamekuwa wanatoa fedha na vifaa vyao kwa ajili ya kuzisaidia taasisi za kidini ili ziweze kutoa huduma mbalimbali kama afya na elimu kwa jamii.

Aliongeza kuwa huduma nyingi za makanisa zina mafanikio makubwa kuliko hata ambazo zinasimamiwa na Serikali, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuzipa taasisi hizo misamaha ili ziendelee kutoa huduma zao kikamilifu.

Alisema haamini kuwa misamaha inayotolewa kwa mashirika ya dini ndio imesababisha uchumi wa nchi kuyumba au mapato kushuka, bali yawezekana kuna mahali ambako misamaha hiyo inatolewa kwa wingi na sasa kusingizia taasisi za kidini.

"Nawaomba wabunge waliangalie jambo hili pale wanapokuwa wanajadili hotuba hiyo ya bajeti, kama wao wanajua na wanaona huduma zinazotolewa na zahanati au hospitali za kidini katika maeneo yao nadhani watapinga jambo hili," alisema.

Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, alisema yeye aliwahi kuwa kiongozi wa dini na anajua kuwa sehemu ambako kuna hospitali ya misheni, serikali haina huduma katika eneo hilo, hivyo kitendo cha kuzifutia misamaha taasisi za kidini ni kuleta umasikini kwa Watanzania.

"Nchi hii ni kubwa, lakini kuna taasisi za kidini zimepeleka huduma kila kona, leo hii unazifutia misamaha ya kodi, si unataka zitoze fedha zaidi kwenye matibabu na kwenye shule, kwa hili hatukubali," alisema Dk Slaa. Juzi akiwasilisha bajeti ya Serikali, Mkulo alisema Serikali inapendekeza kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Ila alisema vifaa ambavyo vinaagizwa kwa ajili ya huduma za kiroho vitaendelea kupata msamaha wa kodi. Hata hivyo maaskofu wanasema mambo ya kiroho ni elimu, afya na akili, hivyo serikali inapaswa kufafanua vifaa vya kiroho inavyojua, "yawezekana wanasema Kurani na Biblia tu."


Sina utaalamu sana wa mambo ya budget za nchi na sina utaalamu sana wa misamaha ya kodi kwa nchi mbali mbali , Lakini kwa nchi ninayo ishi kwa sasa, ninatambua kabisa kabisa kwamba misamaha katika kodi mbali mbali ipo hasa kwa mashirika ya kidini na hizo Non Goverment Organization ( NGo´s)

Nadhani wenzetu waliliona hili lina nafasi kubwa katika jumuiya zao..Ndugu zangu wa Tanzania, Ukitaka kusikia vyanzo vya machafuko ndani ya nchi kimoja wapo ni hiki ambacho Tanzania inataka kukipitisha. Kuzifutia misamaha taasisi zisizo za Kiserikali na mashirika ya kidini maana yake ni kuwapokonya ama kuwanyima huduma za muhimu wananchi walio wengi..!

Ni asilimia kubwa sana ya watanzania wanategemea mashirika na taasisi zisizo za kiserikali katika kujiendeleza na kupata huduma zilizo muhimu kwa maisha yetu ya kila siku. Mashule, Hospital,vyuo,sehemu za kutunzia watoto yatima ,vituo vya kupambana na maambukizi ya virus vya ukimwi na mengine mengi. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo Serikali yetu ya Kitanzania haiwezi kuvifanyia mdhaha hata kidogo.

Ndio serikali inaweza kuwa na vituo kama hivyo lakini, huwezi kulinganisha huduma zitolewazo na Serikali na huduma zitolewazo ktk mashirika ya kidini au taasisi zisizo za kiserikali. Nimesomea kwenye shule za serikali na za Kidini, nimeshafanya kazi serikalini na kwenye taasisi/ mashirika yasiyo ya Kiserikali. Tofauti ni kubwa sana.

Sitopenda kuingilia Budget ya nchi, Bali kwa ushauri wangu kwa faida ya Taifa langu haya Mashirika ya Kidini na Taasisi zisizo za kiserikali zipeni misamaha ya kodi. Msipo fanya hivyo maana yake mnalirudisha taifa kwenye Kipindi cha miaka ya 70`s

Serikali ya CCM inaweza kuja kujutia faida hiyo inayotegemea kuja kuipata kwa kukusanya Kodi katika hayo mashirika/ asasi.

Sitegemei aliyetoa ushauri wa kuyafutia msamaha wa kodi mashirika ya kidini pamoja na NGO´s alitokea NIGHT CLUB au Bar kwa wakati huo,siwezi jua kwani ni kawaida yetu watanzania kutoa maamuzi mazito hasa pale tunapo kuwa walevi. na Ulevi pia waweza kuwa wa madaraka, au pia nafasi ile ya kutoa maamuzi uliipata kwa njia zisizo sahihi.....Kupeana, INATIA SHAKA...!

Amkeni viongozi wetu, Tupo kwenye Karne nyingine kabisa, Ujanja ujanja mnao taka kuufanya katika kukusanya mapato ya nchi zauwezi kuwa na nafasi kabisa kwa wakati tulionao..PATO LA NCHI LINAKUSANYWA PALE KWENYE FAIDA.

I weje mjifutie kodi kwa miaka miwili pale mnapo kwenda kuchimba madini yenye faida kubwa ktk ardhi yetu kwa kisingizio cha kujiweka sawa?? Una uhakika gani madini yaliyopo ardhini yanaweza kuchimbwa zaidi ya miaka miwili unayo tegemea kulipwa kodi ??

Rais mstaafu B. Mkapa alitumia nyia na mbinu mbali mbali katika kukusanya na kuongeza pato la nchi, na alifanikiwa japo alikuwa na udhaifu wake, Na hakukuwa na malalamiko makubwa japo wananchi waliguswa kwa njia moja au nyingine.

Nina uhakika kama kiongozi hatoweza kupata nafasi ya kudadisi na kuchunguza kwa umakini shughuli na wajibu wake ndani ya nchi hata maamuzi yake hayatokuwa ya busara na faida kwa wale wanaomzunguka.

Utakapo mwachia fisi kazi ya kupanga budget ya kondoo atakwambia ni kumkamata kondoo na kumkamua chakula alichokwisha kula kisha ukigawe tena. Na hili ndilo linaloendelea kwa sasa ndani ya nchi yetu.

Mtawakamuwa wananchi mpaka lini ?

Mungu anamakusudi kabisa ndani ya Taifa letu, Na kilio cha watanzania kimemfikia,"Bwana yu karibu na waliopondeka roho huwaokoa" (Zaburi 34:1 Na pia imeandikwa: Simama ukaitende maana shughuli hii ya kuhusu wewe, uwe na moyo mkuu nami ni pamoja nawe..!

Basi watanzania wenzangu Tusimameni tukaitende shughulii hii ya kulikomboa Taifa letu la Kitanzania lililopo nimodomi mwa mbwa mwitu maana shughulii hii inatuhusu sisi na Mungu yu pamoja nasi..!! Mungu Ibariki Tanzania ..!!!
 
Kwa muda mrefu tumetaka kuwasha moto wa mapambano ya kweli.

Kuni zimekusanywa lundo kutoka misitu ya huko Lindi,Mtwara, Mlimba na Mufindi.
Kuna Petroli,Dizeli na Kerosine zilizochumbuliwa Zanzibar, Makaa ya Mawe kutoka Mgodi wa Kiwirana wa Benjamin Mkapa na Anna, Gas ya Songosongo tele.
Zaidi kuna midomo ya Watanzania zaidi ya Milioni 40 ikiwa kwenye mode ya kupuliza moto endapo kutakuwa na jitihada zozote za moto huo kutaka kuzima pindi ukiwashwa.

Tatizo, wapi kiberiti?

Kwa mtaji huu wa kuramba ushuru wapiga sala, hatuhitaji kibiriti tena moto huu utaanza wenyewe kwa Cheche za Kifikra zitakazo zaliwa kutokana na msuguano wa ndani kwa ndani kati ya Imani na undava wa serikali.
Hatumhitaji nabii Isaya kuja kutoa utambuzi wa nani atalala ngoma.

Ni rahisi ni vema na ni bora kwa serikali kuamua kupapasa kende za simba 7000 wenye njaa kali ya kwenda bila mlo kwa wiki 2 kuliko kugusa na kuchezea hisia za wanadini. Huu si mchezo wa hatari tu kwa serikali ni mchezo wa kutekeleza kifo chake.

Serikali zote katika kipindi fulani cha uhai wake zimewahi kulazimika kusalimu amri mbele ya vyombo vya kidini na kuangamia au kumezwa kiaina.

Je serikali ya CCM itapona kwenye hili??

Mkuu hapa Serikali imeangukia Pabaya...!! Wasipo badirisha hii Budget kiama chao kitakuwa kimefika..!! No one will stand !!!!
 
Hivi kama Kenya na Ug. wameweza kutoa misamaha ya kodi kwa % kubwa kwa nini Tz tunaogopa??

Huu woga unatoka wapi?
 
Wana JF wanafki sana,

kwa hiyo unataka kusema Chadema wakipata kuongoza nchi watatoa misamaha ya kodi kwa taasisi zote zisizo za serikali?

Hizi tax exemptions ndio loop holes za kukwepa kulipa kodi. Imefika wakati taasisi za serikali nazo zilipe kodi. Hii kitu inaitwa tax exemption ifutwe kabisa kwenye sheria za kodi za Tanzania. Hata mshahara wa Rais nao uwe unakatwa kodi kama haukatwi

Wakatabahu.


Taxi exemption zipo dunia nzima sio Tanzania tu..!! loop holes zinakuwepo endapo hakuna utawala bora..!!
 
Taxi exemption zipo dunia nzima sio Tanzania tu..!! loop holes zinakuwepo endapo hakuna utawala bora..!!

Tufanye tu kwa sababu ipo dunia nzima???!!!

Kwani lazima tudese kila kitu kinachofanyika duniani? Kuiga tembo kunya mwishowe ni kupasuka msamba.

Kama umeguswa na hili pole sana lakini habari ndio hiyoooo, mmekwepa vya kutosha...
 
kodi na zilipwe sio na taasisi za dini tu ......na waanze wabunge, wafuatiwe na kuongezwa kwa kodi kwa mawaziri.
 
kodi na zilipwe sio na taasisi za dini tu ......na waanze wabunge, wafuatiwe na kuongezwa kwa kodi kwa mawaziri.

Naogopa kuchangia thread hii!! inatisha! labda kama watu hawajui ukweli! inatisha, kwangu naona faraja!

Kwanza sioni tatizo la hili swala;

(1) Kwanza itawapa discipline wachungaji watumie mapato ya kanisa kikamilifu
(2) Tutawapata wachungaji wa kweli!
(3) Makanisa yatabuni mirai na njia mbadala ya kupata fedha,
(4) Itapunguza ombaomba na hivyo kulitimiza lile neno afadhali kutoa kuliko kupokea, wengi wataanza kutoa then watabarikiwa (Acts 20:35)
(5) In long term; itasaidia watu wajue umuhimu wa kuwa serious kuchagua viongozi wa serikali, ambao watatumia vyema kodi wanazotoa
 
Over 30% ya total budget ilikuwa misamaha ya kodi??????????????

Uwii??????????????

Sasa ni kitu gani hapo hakieleweki??

Nchi zingine, masheik na wachungaji hulipwa salari kama wafanyakazi wengine..na kuna ministries of Church Affairs!

Kama kuna ukata waombe serikali iwasidie pesa kidogo ya mishahara!!

Ila kodi lazima ilipwe!

Think once again..30% exemption???????? This is too much!
 
Wanabodi,
Kwanza wakuu ni muhimu tufahamu kwa nini hizi NGO zimekuwepo dunaini na zimeweza vipi kuchangia ktk ustawishaji wa jamii. Tukianza ku question matatizo yanayosababiushwa na watu binafsi kuweza kuvihukumu vyombo hivi basi nasi tunakuwa hatuna hoja..
Kusema kweli sikubaliani kabisa na maelezo ya Mwanakijiji wala mapendekezo yake kwa sababu hayakuzingatia kazi ya vyombo hizi ktk jamii..Na ndiuo maana vimekuwa katikati ya misukumo miwili ya Kiutawala ktk social and economic issues.

Huwezi kuwaweka ktk Biashara kwa sababu wanachukua nafasi ya sehemu ambazo biashara imeshindwa kutoa huduma hizo kwa maskini na huwezi kuipa serikali majukumu ya hizi NGO kwa sababu NGO hujikita ktk sehemu (huduma) ambazo serikali imeshindwa kuzitekeleza..
Maisha bora kwa wananchi wote ni mbiu ya kitaifa na haiwezi kutekelezwa kwa kutegemea aina mbili tu za usambazaji huduma kwa jamii yaani Biashara au serikali..Tunahitaji sana NGO pale serikali na wafanyabiashara wanaposhindwa kutoa huduma hizo kikamilifu hasa kwa nchi maskini kama yetu. Matatizo ya wahalifu yashughulikiwe kisheria kama raia wengine wanapovunja sheria..
Kibaya zaidi kinachojitokeza hapa ni kwamba hukumu inayotolewa na serikali imetazama upande mmoja tu wakati wawekezaji (wafanyabiashara) wanaepuka kodi mara 20 zaidi ya hizi NGO kupitia hii misamaha ya kodi..Na Viongozi wetu nchini wanaepuka kodi mara 10 zaidi ya hizi NGO lakini utaona bajeti imetazama upande mmoja kuweka sheria ngumu kitaifa..

Kisha mkuu Mwanakijiji kawaita Masheikh na Machungaji WANAFIKI... kwa kile walichosimamia kupinga serikali, lakini wanapolia na kuandamana inakuwa Unafiki..kumbuka wanaoandamana sii wale walioiba wala wanaopenda Ufisadi isipokuwa wapo wanaochukua majukumu zaidi ya dini kuliko kujiingiza ktk siasa za Bongo. Wanajua athari za kujitosa kichwa kichwa ktk maswala ya Ufisadi na pengine makanisa au misikiti yao imewahi pokea michango toka kwa mafisadi haohao wanaoshutumiwa leo...It's a Catch 22.

Mapungufu ya taratibu za utekelezaji ktk taasisi za serikali husika ndio chanzo kikubwa cha ukiukaji wa sheria hizi zilizofukiwa makabatini.. Ukitazam kodi zetu inakuwaje kweli mfanyabiashara afanyiwe estmate ya kodi yake kutokana na biashara inayokusudiwa hata kabla hajaanza uzalishaji?.. Utakuta mtu analipa kodi ya mwaka iliyokisiwa wakati serikali haifahamu pato la mhusika kwa mwaka mzima. Hizi tax exemptions zipo kwa kila diplomatic, mashirika ya nje ambayo toka yaingie nchini ni zaidi ya miaka 10 hawajalipa hata ndululu na wanatajirika kichizi.. lakini utakuta serikali ipo kuwatetea hawa watu, leo vyombo vinavyowasaidia wananchi moja kwa moja vinahukumiwa kwa makosa ya waajiriwa wake..kisha basi hata wasifikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo tayari bunge linakaa kupitisha mswada ambao hauna ushahidi zaidi ya utafirti ambao wanashindwa kuufikisha mahakamani..

Sheria zipo na kama kuna mtu kakiuka sheria hiyo kwa kutumia vyombo hivi afikishwe mahakamani, kesho utaona utendaji mzuri wa kazi na sii kutunga sheria ambayo inaathiri huduma zinazowafikia wananchi moja kwa moja na kila siku ya maisha yao...

Tunayaona haya ktk Ufisadi, wanaofikishwa mahakamani ni wale samaki wadogo.. mbali na Rostam kukubali Upapa na kumwita Mengi kuwa ni Nyangumi ina maana kwamba Rostam hakatai kuwa yeye ni Papa Fisadi!, lakini kilichofanyika ni kukataa kununua mitambo ya Dowans lakini asifikishwe mahakamani kwa makosa yaliyotangulia hadi tukavunja mkataba na Dowans..

Hatukuvunja mkataba na Dowans kwa sababu walishindwa kufua umeme! wala hatukuvunja mkataba na Dowans kwa sababu nyinginezo zaidi ya kuwa shirika hilo liligundulika kuwa feki na mkataba ulioingiwa haukuwa halali pia (Mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe)..Rostam hakuulizwa, kuitwa wala kuvunja mikataba ovyo..
Na kibaya zaidi ni kwamba gharama ya umeme wa Richmond/Dowans ilikuwa kubwa kuliko mashirika mengine yote yaliyotuuzia umeme kwa kiwango sawa na mashirika hayo..WATU wametajirika kutokana na mikataba mingi mibovu na bunge limeshindwa kuweka sheria wala kutazama upande huo kwa sababu tu wahusika ni wao wenyewe..
 
Kweli unafiki wa viongozi wa dini nao budi ubadilike. Kwa mfano, wamekuwa mstari wa mbele kusifia watu wenye kushukiwa kuwa ni mafisadi. Sasa wanapoanza kubadili msimamo, kama ule wa kanisa katoliki kuanza kuelimisha wapiga kura badala ya kuwaasa kuchagua chama kilichopo madarakani, then hii ndo dawa yao. Nafikiri kuandamana hakuta leta maana yoyote ile mana makusudio yao ni ustawi wa roho na mwili wa watu. Wajipange kushare hizo gharama na hao maskini.Halafu nao wabadilike, maana sio wote wanaosamehewa kodi wanaenda kusaidia walengwa.
 
ukipanda mahindi utavuna mahindi tu wala si maharage..Viongozi wa dini mligeuza migongo na kuona wananchi wanaongea pumbapumba sasa kilio cha nini? Welcome aboard tulie na kuomboleza pamoja.
 
Ndahani,
Mkuu wangu unapotosha hoja yako hapa.. Hakuna Mchungaji wala Sheikh anaye run hizi NGO ila hupokea misaada kutoka ktk hizi NGO.. Sasa kama una ugonvi na Sheikh au mchungaji ktk maswala ya siasa mfuate yeye lakini huyo Sheikh au mchungaji ana jukumu jingine zaidi ya mapenzi yake ktk isasa za Tanzania.. Nalo ni kupokea na kutoa huduma za kikanisa au Msikiti kwa waumini wake..
Ubadhirifu wa kodi za serikali unafanywa na waajiriwa wa hizi NGO na siii Wachungaji wala Masheikh!..Muulize huyo waziri yale mabati 3800 yaliyouzwa mtaani na Mchungaji gani!..Na ikiwa mwizi ni toka NGO moja iweje uyahukumu mashrika yote ya misaada hata kama hayajakiuka sheria!..
 
Ndahani,
Mkuu wangu unakosa hoja hapoa kabisa.. Hakuna Mchungaji wala Sheikh anaye run hizi NGO ila hupokea misaada kutoka hizi NGO.. Sasa kama una ugonvhi na Sheikh au mchungaji ktk maswala ya siasa mfuate lakini huyo Sheikh au mchungaji ana jukumu jingine zaidi ya mapenzi yake ktk isasa za Tanzania.. Nalo ni kutoa huduma za kikanisa au Msikiti kwa waumini wake..
Ubadhirifu wa kodi za serikali unafanywa na waajiriwa wa hizi NGO na siii Wachungaji wala Masheikh!..Muulize huyo waziri yale mabati 3800 yaliyouzwa mtaani na Mchungaji gani!..Na ikiwa mwizi ni toka NGO moja iweje uyahukumu mashrika yote ya misaada hata kama hayajakiuka sheria!..

Mkuu sawa kabisa hapa tupo ukurasa mmoja.

Anavosema Mkullo, kama mtu aliuza mabati au simenti au tuseme chakula cha msaada, alifanya uhalifu na alipaswa ashtakiwe kwa kuvunja mkataba, na siyo kuja na hoja dhaifu ya kuwafutia misamaha ya kodi!

Mi najiuliza, ni lini wataacha kupandisha bei za bia na sigara na soda,, na kuendelea kusamehe kodi mafuta yanayotumika kwenye kuchimba madini, mahoteli, nk? hatuna tatizo kubwa kuliko tunavofikiri kweli?
 
Ndahani,
Mkuu wangu unapotosha hoja yako hapa.. Hakuna Mchungaji wala Sheikh anaye run hizi NGO ila hupokea misaada kutoka ktk hizi NGO.. Sasa kama una ugonvi na Sheikh au mchungaji ktk maswala ya siasa mfuate yeye lakini huyo Sheikh au mchungaji ana jukumu jingine zaidi ya mapenzi yake ktk isasa za Tanzania.. Nalo ni kupokea na kutoa huduma za kikanisa au Msikiti kwa waumini wake..
Ubadhirifu wa kodi za serikali unafanywa na waajiriwa wa hizi NGO na siii Wachungaji wala Masheikh!..Muulize huyo waziri yale mabati 3800 yaliyouzwa mtaani na Mchungaji gani!..Na ikiwa mwizi ni toka NGO moja iweje uyahukumu mashrika yote ya misaada hata kama hayajakiuka sheria!..
Nakubaliana na wewe kuwa si wote wanatumia vibaya misamaha ya kodi ingawa wapo. Kwasababu misamaha inatolewa kwa NGO au mashirika ya dini bila ubaguzi, inawezekana pia kukawa na influence ya baadhi wa viongozi wa juu wa dini wasio waaminifu maana hao pia wapo. Ninachotaka kusema pia ni kuwa kuandamana haitabadili sana mwelekeo na inaweza kuleta picha kuwa wanajaribu kulazimisha mabadiliko. Badala yake imapct ya decision hii ndio inaweza kufanya serikali ibadili nia au la. Pamoja na yote, mwelekeo wa wakuu wa dini kusema waziwazi sasa kuchukia mambo mabaya yanayoendelea inaweza pia ikawa ni msukumo. Na nimechukulia tu kwa jumla kwamba kanisa katoliki inawezekana ndilo lina mashirika mengi yenye kupata misamaha hii ya kodi, ingawa sina data za back up kwa hilo. Ujasiri wao wa kusema tubadilike katika chaguzi za viongozi sio kitu kidogo kisiasa. Kina imapact pia ambayo inaweza kuwa na negative consequences kwa utawala. Tusisahau pia Dini haitakiwi kuwa na double starndard. Kwnye ubaya ni lazima isimame na kusema hapana. Kwa muda mrefu hawa jamaa wamekuwa kama hawaoni au watazamaji tu na wahusika wa mambo yasioeleweka wakawa ni mashujaa wao in some occasions.Hapo nahisi ndipo penye unafiki wenyewe unaozungumziwa
 
Ndahani,
Unajua mkuu wangu kitu kimoja ambacho mimi siku zote sikubaliani nacho ni kutafuta sababu ili kukiuka ukweli na sheria.. na mara zote Tanzania imekuwa ikitumia mifano hi ktk kujenga hoja. Tukizungumzia Ufisadi wa Rostam basi watu wataanza mbona wewe Mkandara unafanya hili au lile ambalo halihusiani kabisa na ufisadi unaozungumziwa..
Kama unakumbuka Mtikila aliwahi kumwita Roistam fisadi.. ikaja kuwa aliwahi kupokea msaada kutoka kwa Rostam, basi issue ya Ufisadi wa Rostam ikafa wakati tunafahamu fika kwamba Mtikila alipokea fedha zile kama msaada wa kanisa lake..Hivyo naye akawa fisadi mpokeaji..Na nyote humu mlimshutumu kwa kupokea fedha za Rostam.
Hivyo kuwashutumu Masheikh ambao kula yao hutokana na misaada kisha ukawaingiza ktk siasa za Bongo ambazo majority wa viongozi, makanisa, misikiti wamewahi pokea misaada hii ni kuwazulia unafiki.. Ex Presidaa Mkapa aliiba ngapi?..Mabillioni, yeye na Mkewe.. haya nambie ni dhehebu gani hawakupata msaada wa Mkapa kwa njia yoyote ile.. leo umtake kiongozi wa msikiti au kanisa atangaze kupinga Ufisadi wa Mkapa wakati anajua wazi kuwa Mkapa ndiye aliyeweka msingi wa jengo la ibada..kweli huyu mnakuja muunga mkono kwa jinsi tunavyoendelea kufikiri!

Ni sisi wananchi tunatakiwa kutenganisha vitu hivi.. Kiongozi wa NGO (sii mchungaji) kaagiza mabati 4,000 kati yake mabati 3,800 kauza na kuwapa kanisa mabati 200 na mchungaji kapokea mabati 200 kaezeka kanisa lake.. iweje leo tunashutumu viongozi wa kanisa waliopokea mabati 200 wakati swala ni yale mabati 3,800 yaliyouzwa mtaani?..
Haya serikali inaondoa msamaha wa kodi kwa mashirika haya wakati wanajua wazi kwamba mabati 3,800 yaliuzwa mtaani na yanahitaji kulipiwa kodi..kwa nini wasifanye hivyo?
Kuweka sheria haiwezi kurudisha kodi ya mabati 3,800 wala kuongeza kodi kwa sababu NGO zote zinapokea misaada pia, hawana cash wala hawa run huduma hizi kwa kutegemea kubnunua vifaa isipokuwa misaada inayotolewa na wafadhili toka nje..
Sasa unapowaondolea msamaha wa kodi ni lazima ufikirie kwamba haitawezekana kwa NGo hizi ku function hata kidogo..Hakuna NGO dunaini inalipa kodi ni mfumo ambao haukutungwa na Masheikh wala Wachungaji. Na mara zote unataka ufuatiliaji wa nyaraka zake kwa ukaribu zaidi kuepuka ukiukaji wa kulipa kodi.. Na ukweli ni kwamba NGOs huwa zinafuatiliwa zaidi ktk utendaji wake wa kazi kuliko hata mashirika ya kawaida kwa sababu kuna loopholes ambazo zinahitaji umakini sana...
Sasa basi ikiwa serikali yetu inashindwa kufuatilia matumizi ya hizi NGOs na huduma wanazozitoa badala yake tunatafuta urahisi wa kutoa maamuzi kuepuka lawama za baadhi za wananchi..
Mkuu utanisamehe kwani nionavyo mimi wanafiki ni sisi... Siku zote tumesimama hapa kusimamia upande wa haki ya wananchi lakini imefika ktk swala hili tunaondoa malengo yetu na kuwaadhibu kwa kosa ambalo halihusiani nao kabisa. Je, ile haki tunayosimamia siku zote imekwenda wapi? kuna tofauti gani kati yako wewe na huyo Sheikh au Mchangaji ikiwa hata wewe ktk swala hili unaona vizuri wananchi au waumini wote waadhibiwe kwa makosa ya Sheikh au Mchangaji!..Kwa nini tusisimamie haki kila siku bila kujali nani mwakilishi wa hoja hiyo..
 
JF members wengine hii imewagusa pabaya!!

Je kuna makontainer mmekuwa mnatuma Tz kwa mgongo wa dini bila kulipia kodi??

Poleni! Anzeni kulipia kodi tangu sasa !
 
Mzalendohalisi,
I know where U come from.... sifanyi hivyo hata siku moja..
Mimi natazama haki ya huduma za makanisa na misikiti pia kuponyesha serikali yetu kuingia ktk matatizo makubwa na jamii yake.
Trust me, hili swala litazua utata ambao CCM haijawahi kuupata! pengine wewe huelewi siasa za NGOs dunaini..
 
Kutoa misaada siyo excuse ya kufutiwa kodi bila vipimo.hapa kuna options mbili tu, ya kwanza ni kodi kurudishwa kama ilivyofanya serikali na ya pili ni kusamehe a fixed amount ya kodi kwa mwaka.hii misamaha ya kodi isiyo na vipimo maalum ndio inaacha mianya ya ufujaji.
 
ZeMarcopolo,
Mkuu huwezi kuweka fixed amount kwa sababu kila kijiji au sehemu inahitaji vitu tofauti.. Swala kubwa ni ufuatiliaji wa hii misaada. kama mtu kaingiza mabati 4,000 project nzima inayohitaji mabati 4,000 inatakiwa kupitishwa na vyombo vya serikali toka huko kunakohitajika. Hatua kwa hatua.
Kama kanisa linajenga shule ya sekondary au Zahanati ni lazima kiongozi wa serikali iwe wilaya au mkoa ana habari kwamba kanisa au Zahanati inahitaji mabati 4,000. Mara zote hizi NGOs huomba misaada kutokana na shida iliyopo na kama wamepewa mabati 4,000 ina maana initial plan waliyowakilisha kwa wadhamini ni ujenzi unaohitaji mabati hayo... Hiyo plan iko wapi na nani kaipitia hadi kupitisha mabati 4,000 ambayo hayahitajiki..
Hivyo kinachotakiwa ni mkono wa kiongozi wa serikali..mara zote misaada inayoingia nchini huwa tayari matatizo yapo na hesabu kamili ya kile kinachohitajika ipo..Huwezi kujenga kanisa linalotaka mabati 200 yakaingizwa 4,000 bila chombo cha serikali kufahamu yalihitajika mabati 200 tu..
Hii inaonyesha uzembe uliopo sii wa NGOs bali serikali yenyewe.. Hivyo kilichotakiwa kufanywa ni kuhakikisha kuna misingi bora ya kupokea misaada kama hii na jinsi ya kuepuka wizi kama huu..Kutolipa kodi ni criminal case na sheria zipo iweje tutafute sababu nje ya kosa la wazi kama hili!.
 
Back
Top Bottom