Wachungaji/mapadre hamwogopi mungu kufungisha ndoa zikiwa na mimba makanisani

Ndoa ziwe za wenye mimba au la..ni ishu ya wahusika na Mungu wao.Hao wanaoshangaa kitendo hicho, ina maana wao wako na haki asilimia 100? Utakuta wao ndio wa kwanza kuzini na kushiriki utoaji mimba mradi waonekane kwa nje kuwa hawana dhambi kwa vile matumbo yako flat!
ACHENI HIZO....MNA DHAMBI KUBWA ZAIDI YA KUPATA MIMBA NA KUFUNGA NDOA!

Ujue dada Veracity dhambi ni dhambi mbele za Mungu, hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Kinachohitajika kwa watu hawa ni kitubio kabla ya ndoa, mimi kama RC najua kuna kipengele cha kitubio kabla ya ndoa.
 
Tatizo ni kwamba the whole enterprise is a fraudulent monopoly. The bigger problem here is the fact that god does not exist and therefore the bible cannot be the word of god, and from there everything based on the bible as "the word of god" is confusingly incosinstent and naturally it falls short of godlike wisdom.Huku tunaambiwa anayezini apigwe mawe, kule tunaambiwa asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe, kitabu hicho hicho.
Mkuu B, nimekuwa sambamba na wewe tangu awali lakini hii post yako hapa imenipa kizunguzungu. Ckujua msimamo wako ndo hivyo.
 
Hili naona sasa limekuwa ni ukosefu wa adabu ama maadili katika jamii..jamani zamani mimi nijuavyo ni mafuruku kufungisha ndoa zikiwa na mimba ndani yake...nakumbuka kuna siku mchunganji mmoja wa lutherano mwaka jana alikataa kufungisha ndoa ya mtoto wa aliekuwa askofu mkuu mmoja moshi uko akisema kama mtaniruhusu kubariki nitabariki ndoa yenu lakini hivi mkiwa na mimba sifungishi ndoa...hakika kuliwaka moto lakini jambo ambalo sikuamini ile ndoa ilichelewa na akaja mchungaji mmoja akafungish na yeye akiwa anaona aibu akaamua kupasua adharani kama si heshima ya askofu babako kwa kweli tuingefungisha hii ndoa

sasa hivi jambo hili limekuwa ni aibu kila makanisa sasa yamekuwa yakifungisha ndoa zikiwa na mimba ndani yake....majuzi nilihudhuria harusi moja pale st joseph kati ya harusi tano tatu wanawake walikuwa wamevimba matumbo yao kama wako theartre wanasubiri kupasuliwa ilikuwa jambo la aibu sana lakini hatimae ilifungishwa huku mapadre wakipiga makelel ya kutorudia tena watu wengine...bado najiuliza hawa watu huwa wanahonga ndoa kufungishwa hivi ama wanawafanya upofu hawa watumishi wa MUNGU....nafikiri makanisa yanaitaji kuwa mstari wa mbele kukemea na kutaa hali hizi.....wazazi imefika wakati wa kuheshimu ndoa takatifu msiwaruhusu vijana zenu kujazana matumbo na kuwatia aibu mbele ya madhabahu....imagine majana nimeenda shuguli moja nikakuta jamaa anaonyesha zile picha za mwanamke za zamani he gafla anamwonyesha yule mwanamke akiwa na bwanaharusi mtarajiwa wamekumbatiana wanalishana sasa nkajiuliza kama mmeshamaliza kila kitu tumeiwa kufanaynini???/

Kazi kwenu mnaotarajia kuoa kuna starehe ukiwa na mtoto ndani ya ndoa...

Mheshimiwa!, Nina mtazamo tofauti na "The head of Thread" yako hapo juu.
Nijuavyo mimi, Padre/Mapadre kwa upande wa imani yangu hawafungishi NdOA.
NDOA, inafungishwa au kufungwa na wahusika wenyewe.i.e David na Betty, ila sasa Mapadre/padre anakuwa amesimama kama shahidi wa kanisa na jamhuri/Serikali.
 
Lakini kuna vimimba vingine havionekani 1-4 month mchungaji atajuaje huyu ni mjamzito ..hii dhambi itakuwa ya wahusika na si mchungaji

labda ile ambayo akitoka kanisani anafikia leba
 
Kuna dimension nyingine haijazungumziwa japo haihusiani na kuwa na dhambi or not katika kufunga ndoa mtu akiwa mjamzito.

1.Kufuatana na sheria za TZ mtoto anayezaliwa nje ya ndoa hata kama baadae wazazi wataoana, kisheria anahesabika kuwa ni mtoto illegitimate! Hivyo basi wazazi huona ni bora kufunga ndoa kabla mtoto hajazaliwa ili wawe ndani ya wigo wa sheria linapokuja swala la uhalali wa mtoto.Vinginevyo mtoto anayezaliwa ilhali wazazi hawajafunga ndoa atalazimika kisheria kuasiliwa ( adopt) na wazazi wake hao ili kumpa uhalali.Watu wengi wanakuwa hawalijui hili.

2.Ukiachilia mbali kisheria, nadhani wanandoa wengi siku hizi hawajali tena kusubiri kujuana hadi ndoa ifungwe.Wengi huwa tayari wanafahamiana kila kitu na hivyo ndoa ni formality tu.Kwa kifupi, bila kuingia into the moral and ethical side of things nadhani dunia sasa imegubikwa na dhambi, ukengeufu, msongo na kila aina ya matatizo kiasi kwamba ni kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano kutegemea kuwa kuna watu wako 100 % wanyoofu kwenye mienendo yao.Mjadala huu umenikumbusha wimbo wa Banana Zorro - ZOBA ambapo Banana anaimba " subira yangu ndio ilonipoonza, ngoja ngoja naonekana mjinga.... nilisubiri nisifanye kitu nawe hadi umalize masomo...kumbe ukampenda rafiki yangu...." sasa ndio tuone kuwa hata kama mmoja atataka kweli kusubiri..mwenzie mara nyingi hatasubiri ataona huyo mwenzie ni Zoba tu.....mradi ni vurugu tupu.

3.Kwa wenye kulalama na kulaani wajue kuwa ndoa za watu watatu ( bwana, bibi na katoto tumboni) zitaendelea tu.Labda itokee divine intervention.

NB : Mchango wangu unaonyesha tu hali halisi na haimaanishi kuwa naunga mkono vitendo husika.
 
Mheshimiwa!, Nina mtazamo tofauti na "The head of Thread" yako hapo juu.
Nijuavyo mimi, Padre/Mapadre kwa upande wa imani yangu hawafungishi NdOA.
NDOA, inafungishwa au kufungwa na wahusika wenyewe.i.e David na Betty, ila sasa Mapadre/padre anakuwa amesimama kama shahidi wa kanisa na jamhuri/Serikali.

mkuu uko sawa kabisa ...

btw ni ngumu sana ku-reach concesus katika hili coz kila dini/dhehebu lina tafsiri yake juu ya jambo hili and wanaamini according to mapokeo yao. Hujiulizi kama Biblia ni moja, why then kuwe na Wakatoliki, Walutheri, Waanglikana, Wapentekoste ...?? why kuwe na mafundisho tofauti ya ubatizo, ndoa, kifo e.t.c?? Na kama Quran iliyoshushwa na Mwenyezi Mungu na according to mafundisho ya Mtume Muhammad S.A.W juu ya kufunga na kufungua ramadhani, e.t.c. , why then kuwe na tofauti za kufungua ramadhani?? why kuwe na wa-Sunni, wa-Shia ...??

"kiingiacho mdomoni sio najisi bali kimtokacho mtu moyoni ndiyo najisi", tuache kufikiria kwa nadharia ya maumbile bali tuende zaidi ya hapo! .... nadharia ya nafsi ina majibu mengi juu ya hili na yanafahamika lkn kama nilivyowisha highlight hapo juu ... tatizo ni tafsiri na mapokeo ya dini/madhebu yetu ... that's it!
 
Lakini kuna vimimba vingine havionekani 1-4 month mchungaji atajuaje huyu ni mjamzito ..hii dhambi itakuwa ya wahusika na si mchungaji

labda ile ambayo akitoka kanisani anafikia leba

Vimimba au vijimimba? Lol! Mi naona poa tu kuliko kuja kufunga ndoa na mitoto inashuhudia, kama nilivyofanya mimi.
 
hawawezi kuogopa kwa sababu pengine wahusika wanakuwa tayari wametubu.....hata hivyo kama physical appearance haineshi ujauzito hilo sio kosa la mchungaji bali ni kosa la mhusika/wahusika...........yote kwa yote mungu wa kikristo anaangalia zaidi roho ya mtu ilivyo pondekapondeka mbele zake na si mwili ulivyo........
 
kama nimemwelewa pdidy anachosisitiza hapa ni kuwa kufunga ndoa na mimba ni ishara kwamba maharusi wamekuwa wakizini kabla ya ndoa, kimsingi dini zote zinakataza hayo ila kwa wale ambao hawana mimba huwezi kuwasemea kuwa wamekuwa wakizini, hapa ni ule usemi wa 'aliyekutwa na ngozi ndie aliekula nyama' kwa upande wangu pia huwa sifurahishwi na kitendo cha mtu ana mimba ya miezi 8 ndio anaingia kanisani kufunga ndoa.
 
Mkuu B, nimekuwa sambamba na wewe tangu awali lakini hii post yako hapa imenipa kizunguzungu. Ckujua msimamo wako ndo hivyo.
__________________
MI NILISHAMWONA TOKA ROHONI HAYUPO;ULICHELEWA KUSOMA NYAKATYI

.Kwa wenye kulalama na kulaani wajue kuwa ndoa za watu watatu ( bwana, bibi na katoto tumboni) zitaendelea tu.Labda itokee divine intervention.


DIVINE INTERVENTION HII NDIO TULIOILETA HAPA NDUGU...NA IPO WEWE BINAFSI KUIKUBALI...ABARIKIWE ALIEANDIKA POST HII....
 
Back
Top Bottom