Wachungaji/mapadre hamwogopi mungu kufungisha ndoa zikiwa na mimba makanisani

Kama unakimbilia hilo la kupigwa mawe na hili chini

maana mshahara wa dhambi ni """mauti""""' inakuwaje hiyo??
 
Unajua tatizo tunalolalamikia hapa ni si haki kufungisha ndoa za wenye mimba na wasio na mimba at the same tyme lazima tuwaheshimu hawa wanaokuja kanisani hawajakutana kimwili......ukisoma kwenye biblia
 
Kama unakimbilia hilo la kupigwa mawe na hili chini

maana mshahara wa dhambi ni """mauti""""' inakuwaje hiyo??

Hata kama mshahara wa dhambi ni mauti, haijasemwa wenye dhambi asiozwe maana mwishowe hakuna atakayeozwa.

Huku kujifanya holier than thou ni ufarisayo tu.Kila mtu ana skeleton kwenye closet lake, kama si mimba basi watu wamejuana kimwili bila kupata mimba, wengine wamekuwa na affairs na watu wengine, wengine wamekuwa na affairs na waume/ wake za watu.

Ukisema wenye mimba wasiozwe what's next? Utaenda kupima bikira? Maana basically kama unaongelea suala la kutojuana kimwili kabla ya ndoa issue ni ile ile, mwenye mimba na asiye bikira lao moja.Na kama unasema bikira inaweza kutoka yenyewe, hata mimba inaweza kupatikana bila kujuana kimwili kwa mujibu wa biblia.

Kwa hiyo huu ufarisayo wa kujifanya sisi wasafi sana na wenzetu wana dhambi sana hauko katika doctrine ya Kristo.Kwa mujibu wa wakristo Kristo hakuja ku judge, alikuja ku redeem, na siku ya judgement itakuja. Who are we to judge in such a cruel way?

This is akin to the spirit of the Spanish Inquisition and similar witchhunts. Halafu wale wanaojifanya kuwa staunch opposers wa haya mambo ndio worst offenders.

Kama yule senator Larry Page alivyokuwa anamrushia mawe Bill Clinton kwa sababu ya infidelity, baadaye akaja kukutwa ana solicit gay sex kwenye public restroom.Ditto Kwa yule gavana wa South Carolina. Kwa hiyo hujafa hujaumbika, acha ku judge, especially kwa mambo ambayo hayana biblical ground.
 
Unajua tatizo tunalolalamikia hapa ni si haki kufungisha ndoa za wenye mimba na wasio na mimba at the same tyme lazima tuwaheshimu hawa wanaokuja kanisani hawajakutana kimwili......ukisoma kwenye biblia

Utajuaje hawajakutana kimwili?
 
Ninamaanisha hata wale wanaoenda kanisani kufunga ndoa wakati wameshakutana kimwili kabla bila kujali mimba nao ni dhambi.....,na kama wanaenda kanisani kufunga ndoa wajue wanabariki....ndoa

nafikiri hili wakiwa makni watumishi wa mungu litapunguza sana uzinzi katika jamii
 
Kwa msingi wa "mwenye dhambi hafungi ndoa" basi hakuna anayefunga ndoa, nani kati yetu asiye na dhambi?
 
Swala muhimu mkuu B ni kujitahidi kufunga ndoa takatifu ambayo wawili mnakuwa hamjawahi kukutana kimwili hata siku moja...hakuna haja ya kutest kama vijana wa sikuhizi wanavyosema unaweza test ukatest kasa.....ndio maana ukiwa unaingia ndoani usijidanganye ati akiwa kwenye ndoa atabadilika...weeeeee kama unaingia ingia kama alivyo ubadilika unamwachia mungu matokea....zingine hazibadilikiki
 
Hivi niulize Wakiristu mnafahamu kuwa ikiwa biharusi atakutwa sio bikila adhabu yake ni kifo ?
Kill Women Who Are Not Virgins On Their Wedding Night - Deuteronomy 22:20-21 NAB , Sasa hii ya kuozeshana wakiwa na mimba sijui wamefikaje? Au kuna ile aya wanayoifuata ya raped to be married by rapist forever .Hawa wataumbuka tu we wacha !!
 
Hebu nikuulize ndugu, mwanamme mtu mzima anayefanya ngono na binti wa miaka 8 ni pedofile au sio pedofile.

NB: Twende taratibu usikimbie.

Kabla sijakujibu japo hujaniuliza mimi ningependa unielezee maana ya hiyo au hilo neno linaloonekana ni la kimombo "pedofile ",ili nielewe umeifahamu vipi tafsiri ya neno hilo au maana yake kwako ni ipi ? Na nikiendelea na kuichambua huo mstari wako ...anaefanya ngono...hapa panahitajika uhalali wa hiyo ngono ,je kuna makubaliano ya ndoa yalipita na hako kabinti ka miaka minane ? Au kalibakwa ,ilikuwaje kuwaje inafaa uweke picha ili sheria ichukue mkondo wake ? ,Halafu pia sijui kama unaufahamu au ndio jazba tu ili nawe uonekane umo , hivi katika ukiristo mwanamke anaeolewa inabidi awe na miaka mingapi ? Ningependa ushaidi kama upo au unapatikana ndani ya bible ? Kama hamna nafikiri huyo atakuwa si pedofile maana ndani ya dini amna kiwango maalum kilichowekwa. Nategemea hao wahusika watakuwa watu wanaofuata mrengo fulani wa dini.

NP:Tuende taratibu tusikimbizane .
 
mkisha oana na baada ya hapo mtoto hapatikani inakuwaje??? Hili ndo limepelekea, lakini mimi kwa ushauri ningesema watu kama wana wasiwasi basi wazae kwanza pamoja ndo wabariki ndoa yao.......ni ushauri tu.
 
Kabla sijakujibu japo hujaniuliza mimi ningependa unielezee maana ya hiyo au hilo neno linaloonekana ni la kimombo "pedofile ",ili nielewe umeifahamu vipi tafsiri ya neno hilo au maana yake kwako ni ipi ? Na nikiendelea na kuichambua huo mstari wako ...anaefanya ngono...hapa panahitajika uhalali wa hiyo ngono ,je kuna makubaliano ya ndoa yalipita na hako kabinti ka miaka minane ? Au kalibakwa ,ilikuwaje kuwaje inafaa uweke picha ili sheria ichukue mkondo wake ? ,Halafu pia sijui kama unaufahamu au ndio jazba tu ili nawe uonekane umo , hivi katika ukiristo mwanamke anaeolewa inabidi awe na miaka mingapi ? Ningependa ushaidi kama upo au unapatikana ndani ya bible ? Kama hamna nafikiri huyo atakuwa si pedofile maana ndani ya dini amna kiwango maalum kilichowekwa. Nategemea hao wahusika watakuwa watu wanaofuata mrengo fulani wa dini.

NP:Tuende taratibu tusikimbizane .

Kama umechukua dhima ya kujibu swali bila kuulizwa ni vyema tu.

Kwa kifupi sihitaji maelezo, wewe weka tu jibu. Ndio au Hapana? Nadhani sio vigumu kiasi hicho.
 
Kama umechukua dhima ya kujibu swali bila kuulizwa ni vyema tu.

Kwa kifupi sihitaji maelezo, wewe weka tu jibu. Ndio au Hapana? Nadhani sio vigumu kiasi hicho.
Imesemwa tuende taratibu sasa kama unakubaliana na kauli hiyo ya kwenda taratibu ,usiseme weka jibu tu ,kama nikuweka jibu tu ,basi jibu lililowekwa ni kuwa alikwishakukuelewa na hapo ungelinyamaza na kukaa tuli.
Sasa kama umehitajia taratibu itabidi paendwe taratibu,vinginevyo kaa kimya.
 
Kwa ndoa za Kanisa Katoliki hakuna haja ya mjadala. Soma sheria za Kanisa Katoliki Kanuni ya 1055 hadi 1165. Tatizo lililopo hata wakatoliki wengi si kwamba hawazisomi sheria hizo, bali hawajui kwamba zipo.

Ukitaka kuthibitisha tafuta wakatoliki kumi uwaulize halafu urudi hapa mtandaoni unipe majibu yao.
 
Kwa hiyo unataka wenye dhambi wasifungishwe ndoa?

ahaaaaaa
si wenye dhambi kaka;waliozaa nje ya ndoa hawafungishwi ndoa
wanabariki ndoa.tofautisha kati ya kufunga ndoa na kubariki ndoa....

Sasa unabariki vipi "ndoa" ambayo haipo?! Maana hawa watu hawajawahi kuoana kabla, sasa inakuwa vipio iitwe "kubariki ndoa"?!!!! Very confusing!!
 
Imesemwa tuende taratibu sasa kama unakubaliana na kauli hiyo ya kwenda taratibu ,usiseme weka jibu tu ,kama nikuweka jibu tu ,basi jibu lililowekwa ni kuwa alikwishakukuelewa na hapo ungelinyamaza na kukaa tuli.
Sasa kama umehitajia taratibu itabidi paendwe taratibu,vinginevyo kaa kimya.

Kwa hiyo jibu ni pedofile au sio pedofile? Tufupishe mazungumzo tafadhali.
 
Deuteronomy 22:20-21 NAB

LAKINI IKIWA NI KWELI NENO HILI..LA KUTOONEKANA KWAKE YULE KIJANA ALAMA ZA UBIKIRA; NA WAMTOE NJE YULE KIJANA MLANGONI PA NYUMBA YA BABAKE WAMPIGE MAWE MPAKA AFE..KWA ALIVYOFANYA UPUMBAFU WAKE...KWA KUFANYA UKAHABA KATIKA NYUMBA YA BABA YAKE......

SO UKIWA UNAZINI UKIWA BADO KWA WAZAZI WAKO HAKUNA SABABU YA WEWE KUTOPIGWA MAWE...MNALIJUA HILI...SO UTAONA MIMBA NI KAMA MATOKEO TU NA DHANA ZAIDI NI KUZINI .....YAANI UZINZI..MMMHHH TOPIC NJEMA
 
May be we all know not NDOA ni nini! Ndoa hufungwa katika stages kwanza mioyoni mwa wapendanao, and the other successive stages and afterall is fainali madhabahuni as a formality. Mimba haihusiani na kiapo kwani NDOA is mainly kiapo cha kuishi hadi kifo kitakapotenganisha wawili waliokuwa mwili mmoja. Ndio maana si mashahidi wala maaskofu wala mapadre wala mashehe wako answerable kama ikiwa waliofunga ndoa hawatapata mtoto. Hilo haliwahusu ukifikiria kiroho. Mungu tena hubariki nia kabla ya kukiri mbele ya watu na ndio maana huwabariki mtoto kabla ya kuapa kuishi pamoja kwa kuwa huona nia na ndio vile vile utaendelea kuona mimba katika viapo vya ndoa mpaka basi. Anyhow NDOA iheshimike sana. Na hakuna classes za ndoa baada ya kiapo. NDOA is NDOA.
 
Pdidy sio makanisa yote, makanisa ya kiprotestant ndio yako hivi, nayo hutegemea aina ya pastor wa mahali hapo,

Mimba ni alama ya kuwa hawa watu walikutana kimwili, Bible hairuhusu kukutana kimwili kabla ya ndoa, na hatujui namna ya kujua hawa walikutana kimwili au la, Mimba ni moja ya kithibitisho kuwa hawa watu walikiuka maadili ya biblia, kuruhusu watu kuoana na mimba ni kuhalalisha tendo lifanyike kabla ya ndoa!

Huwa nasema kila siku there is no compromise katika kumfuata Mungu,so as there is no compromise kufuata katiba zetu za organisations, taifa, n.k

Kushindwa kulinda na kusimamia kile kinachopaswa kufuatwa kwa gharama yeyote ni ushahidi tosha wa dini za kuletewa na kurithishwa, NDIO tunatka hapo tunaenda CCM,CHADEMA , kwenye makampuni tunayafisadi hili hali tukijua katiba na miiko!

Hii ni makosa, I am pastor though!
 
Pdidy sio makanisa yote, makanisa ya kiprotestant ndio yako hivi, nayo hutegemea aina ya pastor wa mahali hapo

mkuu waberoya nikisoma hapo juu naona jamaa aliona hayo kanisa la st joseph ....nahisi haya matatizo yamemwagika kila makanisa..mungu aturehemu tu...swali linalokuja iweje wanafungisha watu ndoa wakati wanawaona na MITUMBO yao madhabahuni
 
Wakuu kwani tatizo ni Kujamiiana kabla ya Ndoa au Mimba kabla ya Ndoa?
 
Back
Top Bottom