Wachumi wamshukia Magufuli, watabiri pigo la kiuchumi

Hao wataalamu wapuuzi sana! Miaka yote ya utawala uliopita hawakuwapo kushauri serikali! iweje hata leo tunaburuza mkia kwa umaskini duniani! wataalamu mbona hata uchumi ndani ya nyumba zenu hauimariki! acheni propaganda za kimagazette. nendeni ikulu mkamsaidie ushauri na si jamii forum
 
Kiburi haswa ndo naona kitatugharimu. Yaani serikali kwa makusudi wanashindwa ku comply na terms za MCC na hatimaye tunanyimwa msaada wa Trillion 1 kwa mwaka halafu kuna watanzania wanafikiri eti tutaweza wenyewe. Mnajidanganya sana aisee. Kwa umasikini nnaouona hivi vijiji vya kitanzania nadhani tulikuwa tunahitaji hizi fedha sana.

Nchi yetu masikini sana, sasa unapoanza kugombana na watoa misaada sijui ni ujasiri wa wapi huu.. tutashindwa mapema mno

Kha! Hiyo ID yako utata mtupu.

Ila kwa kuongezea kwenye hoja yako, ni afadhali angalau kiburi chetu kingekuwa kinatokana na kusimamia haki lakini eti suala lenyewe ni issue ya Jecha!!! Haya Jecha afute tena uamuzi wa Mcc tuone.
 
Usikute wewe ni Nape Moses Nauye!

Wasomi wetu ndiyo waliyoiangusha hii nchi na ndiyo maana wengine wanalia kwa kuondolewa ukuu wa mkoa na hiyo inaonyesha kwamba usomi wao umeshindwa kuwasaidia wao binafsi kiasi kwamba sasa wanakimbilia ajira za kisiasa.
 
.....Hao wakubwa wakishafunga fedha zao kazi itayobakia ni KUKAMUANA SISI KWA SISI.
--he should review series port charges...
--create attractive and friendly tax for businessmen/
--review again znz elections of 2015.
--startup new talks over znz .
--etc etc etc.
sikio la kufa halisikii dawa.
hata kama kufunga mikanda, mikandi itafungwa na walalahoi tu.
 
Shida hii nchi uchumi umeshikiliwa na wapigaji madili sasa wakiporomoshwa uchumi lazima utetereke. Ngeshauri washughulikiwe kimahesabu huku tukiwajengea uwezo wao kuendelea na kazi,isiwe kama vita wakati mifumo yetu ndiyo iliwalea mpaka kuwa wapigaji wazuri.
Pia tuanze kufundisha watuwetu kuanzisha viwanda vidogovidogo kama vya viatu,vyombo,simple electronics,nguo,vyakula hasa kwakuifufua Sido na kujitosa kwenye technolojia ya china etc.
Bila kufanya makusudi tutaishia kuwafundisha watotowetu historia teeele na kuwajengea uhodari wa kubishana kisiasa na kulaumu.
 
RAIS MAGUFULI KUPATA PIGO

Rais John Magufuli ametahadharishwa kupata pigo kubwa la kiuchumi linaloweza kuikumba serikali yake wakati wowote kuanzia sasa, jambo linaloweza kuwakatisha tamaa wananchi ambao kwa sasa wanamuunga mkono kwa kiasi kikubwa.

Tahadhari hiyo imetolewa na wachumi waandamizi nchini kufuatia mwenendo mbaya wa sasa wa nchi ktk uzalishaji wa bidhaa za kuuza nje, uhaba wa vyanzo mbadala vya kodi na kutoimarishwa kwa vyanzo vya fedha za kigeni ambavyo vinatajwa kuwa mhimili mkuu katika kuimarisha pato la ndani la taifa (GDP).

Chanzo: Raia Tanzania
hao wachumi ni sawa na kuku doti doti tu!! wanapaswa kupendekeza na kutoa ushauri sio kuvimbisha matumbo na kukosoa tu, kwan TZ ni ya magufuli peke yake...
ikifeli serikali na wao pia wamefel na tutawachamba na vibunzi hadharani
 
Kuwa na wachumi wa aina hii ni bora kutokuwa nao kabisa. Lini Tanzania ilizalisha na kuexport zaidi ya tunavyoimport?

Tatizo kubwa kimekuwa na kupiga madili kuanzia matajiri wakubwa wa nchi hii, hadi machinga wa barabarani, Sasa mirija imezibwa kila mchumiA tumbo anaanza kulalamika.

Nchi ambayo tajiri mkubwa kama MO, MENGI, BAKHRESSA na wengine wengi wanavuna tu lakini hawalipi kodi kuendana na biashara zao. Wenzetu, ili uonekane kweli ni bilionea, lazima utajiri wako uendane na kodi unayolipa kwa serikali.

Uchumi haujengwi kwa siku moja au mwaka, tunapenda moto wa mabua, ndani ya miezi sita maisha yawe mazuri, kila mtu awe na ajira. Uliza kipindi USA ilivyokumbwa na 'the great recession' ikimchukua Obama miaka mingapi kufix uchumi wa marekani. Russian Rouble has tumbled na Putin bado hajaiweka sawa, mwaka umepita na uchumi bado haupo sawa.

Fixing the dead economy sio kazi ya siku moja, mwezi wala mwaka. Ni process ndefu, inahitaji watu makini, wasio walalamikaji kama wa Tanzania walio wengi, washauri wabobezi katika sekta mbalimbali kuanzia teknolojia, sayansi, kilimo, elimu, viwanda, biashara na uchumi. Tuache kulalamika.
 
wachumi uchwara. Miaka yote hii walikuwa wapi wakati uchumi unayumba kwa kutokukusanya kodi?
RAIS MAGUFULI KUPATA PIGO

Rais John Magufuli ametahadharishwa kupata pigo kubwa la kiuchumi linaloweza kuikumba serikali yake wakati wowote kuanzia sasa, jambo linaloweza kuwakatisha tamaa wananchi ambao kwa sasa wanamuunga mkono kwa kiasi kikubwa.

Tahadhari hiyo imetolewa na wachumi waandamizi nchini kufuatia mwenendo mbaya wa sasa wa nchi ktk uzalishaji wa bidhaa za kuuza nje, uhaba wa vyanzo mbadala vya kodi na kutoimarishwa kwa vyanzo vya fedha za kigeni ambavyo vinatajwa kuwa mhimili mkuu katika kuimarisha pato la ndani la taifa (GDP).

Chanzo: Raia Tanzania [/QUOT]
Wachumi uchwara
 
mwananchi atakaeshindwa kupata walau mlo mmoja kwa siku na wakat mvua za kutosha zinanyesha atakua ni mvivu na mzembe wa kutupwa
Uko mkoa gani?... Tuanze na hilo kwanza.Sina maana ya kutetea uzembe na uvivu kwani natambua madhara yake.
 
Wasomi wetu ndiyo waliyoiangusha hii nchi na ndiyo maana wengine wanalia kwa kuondolewa ukuu wa mkoa na hiyo inaonyesha kwamba usomi wao umeshindwa kuwasaidia wao binafsi kiasi kwamba sasa wanakimbilia ajira za kisiasa

Hao wanaojiita wasomi wachumi ndio wao hao wanaotumiwa na mashirika ya kimataifa ya World Bank na IMF kufanya tafiti uchwara zinazokubaliana na matakwa ya hayo mashirika!! Hawa wasomi ni vibaraka tu ambao wengi wao huzawadiwa kwenda kufanya kazi kwenye hayo mashirika baada ya kuziuza nchi zao!! Magufuli hana budi kutafuta washauri wachumi ambao ni wazalendo wa kweli na sio hawa waliotumika kutuletea structural adjustment programmes zilizotuingiza kwenye umaskini zaidi. Wasomi wachumi wapo lakini wanabaniwa na hawa ambao mashirika ya nje yanawapendekeza kwa watawala kama walivyofanya enzi ya Mzee wa msoga kumletea gavana wa BOT toka washington na matokeo yake tumeyaona!!
 
Wasomi wetu ndiyo waliyoiangusha hii nchi na ndiyo maana wengine wanalia kwa kuondolewa ukuu wa mkoa na hiyo inaonyesha kwamba usomi wao umeshindwa kuwasaidia wao binafsi kiasi kwamba sasa wanakimbilia ajira za kisiasa.

Serikalini wamejaa wasomi wa vyeti sio ujuzi. Lazima hali hii irekebishwe, tena haraka.
 
Kiburi haswa ndo naona kitatugharimu. Yaani serikali kwa makusudi wanashindwa ku comply na terms za MCC na hatimaye tunanyimwa msaada wa Trillion 1 kwa mwaka halafu kuna watanzania wanafikiri eti tutaweza wenyewe. Mnajidanganya sana aisee. Kwa umasikini nnaouona hivi vijiji vya kitanzania nadhani tulikuwa tunahitaji hizi fedha sana.

Nchi yetu masikini sana, sasa unapoanza kugombana na watoa misaada sijui ni ujasiri wa wapi huu.. tutashindwa mapema mno
Kukubali masharti maana yake ni kukabidhi nchi kwa aliyeshinda kweli kitu ambacho watawala hawapo tayari kuona kinatokea.

Kila mchuma janga ula na wakwao tujipange tu kukabiliana na kitakachofuata hatuna cha kubadili muda huu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom