Vita vya Kiuchumi kwenye Sakata la Bandari

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Hii sakata la bandari lina vita kubwa sana za kiuchumi kati ya UAE na nchi ya Belgium katika kuthibiti madini ya DRC.

Hivi karibuni serikali za UAE na DRC waliwekeana mktaba mkubwa wa uchimbaji na ununuzi wa madini ya DRC.

Bandari ya Dar es Salaam kwa kiasi kikubwa itanufaika na hii biashara kwani serikali ya Dubai kupitia kampuni ya DP World baada ya kuchukua sehemu ya uendeshaji wa bandari hiyo inamaanisha sehemu kubwa ya madini yatokayo DRC itapitia Dar es Salaam.

Hii imekuwa pigo kwa serikali ya Belgium kwani kwa zaidi ya miongo mingi nchi hii ilinufaika na madini ya nchi ya DRC.

Hivi karibuni tuliona mwanasiasa mmoja aliitwa Belgium baada ya ya sakata hii la bandari kuanza na aliporudi hapa nchini yeye na chama chake walianzisha mikutano mingi ya kupinga hili suala la bandari tena kwa kufikia kuwatukana marais wastaafu na Rais wa sasa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Serikali isipuuzie hawa wanasiasa mamluki katika mpango wao kutaka kutugawa na kuleta machafuko hapa nchini ni kitu cha kushangaza sana kuruhusu mtu anaishi ubelgiji kama mkimbizi kufanya mikutano ya siasa hapa.

Nchi Kenya wakati wa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilimpiga marufuku Miguna Miguna ambaye alikuwa mkimbizi huko Canada kuingia nchini humo kufanya siasa kwasababu ya kumtolea lugha za kejeli Rais Kenyatta.
 
8d288b62-7346-4610-a9a2-a328517f79cd.jpg
 
Back
Top Bottom