Wachina waenzi na kuendeleza moyo wa “Baba wa Mpunga Chotara” wa kuwanufaisha watu wote duniani kwa chakula

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111438851499.jpeg


Kilimo ni uti wa mgongo wa maisha na pia ni sehemu muhimu sana hasa katika jamii yetu ya kisasa, ambapo kinaathiri chakula tunachokula, ardhi tunayoishi, na mambo mengine mengi ya jamii yetu. Mamilioni ya watu wanaweza kujikwamua na umaskini duniani endapo watawekeza kwenye sekta ya kilimo, lakini bila ya kuwa na utaalamu ama teknolojia husika za za kisasa ambazo zitahakikisha mavuno yanakuwa bora na mengi, kilimo hiki hakitakuwa na manufaa makubwa sana.

Hivi karibuni wanasayansi wa China wamegundua code ambayo itarahisisha zaidi upatikanaji wa zao la mpunga. Tunafahamu kwamba Wachina ndio watu ambao hutumia kiasi kikubwa cha mchele duniani, hivyo wamekuwa wakijitahidi kutafuta njia za kuongeza uzalishaji wa mpunga. Kulima aina za mpunga zenye mavuno mengi na ubora wa juu sio tu ni suala muhimu na linalotiliwa maanani zaidi katika uwanja wa utafiti wa kisayansi, lakini pia linahusiana na usalama wa chakula.

Katika juhudi za kuhakikisha mchele unapatikana kwa wingi na kukidhi mahitaji ya watu wa China na duniani kwa ujumla, timu ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Huazhong cha China imefaulu kutambua code muhimu ya kijenetiki ambayo itaimarisha mavuno ya nafaka ya mpunga kwa asilimia 7 hadi 15.

Hii ni hatua nzuri sana hasa ikizingatiwa kwamba juhudi hizi hazikuanzia hapo tu, bali zimeanza kitambo sana. Tunapozungumzia ‘mpunga’ na ‘China’ wengi watakuwa wanamkumbuka baba wa ‘Mpunga Chotara’ Yuan Longping, ambaye alifariki Mei 22 mwaka 2021. Katika enzi za uhai wake Bw. Yuan Longping aliwahi kusema kwamba“Kuwanufaisha watu wote wa dunia ni moja ya matumaini yangu maishani.”

Moyo wa kuendeleza kuwanufaisha watu kupitia chakula unaonekana kutoishia kwa baba wa mpunga chotara tu, bali moyo huu unaenziwa na kuendelezwa na Wachina wengine, na ndio maana hivi sasa tafiti mbalimbali zinafanyika hapa China juu ya zao hili la mpunga pamoja na nafaka nyingine.

Kimsingi China hulima mpunga wenye punje nyembamba na ndefu yaani indica, na wa kitumbo yaani, mpunga wa japonica. Katika utafiti wao, watafiti hawa wameonesha tofauti katika sifa za mwonekano na muundo wa kijeni baada ya kuchagua ule uliozalishwa kwa muda mrefu. Baada ya miaka 12 ya utafiti na uchanganuzi, timu iligundua kuwa aina nyingi za mpunga wa indica hazijabeba locus GY3 hivyo aina zilizoboreshwa kwa kuwekewa GY3 zikaonesha ongezeko la asilimia 9.1 hadi 16.3 la mavuno.

Ujuzi na utaalamu kama huu wa kutafiti namna ya kuongeza mavuno ya nafaka hasa mpunga, unahitajika zaidi katika nchi za Afrika, ambazo nyingi zao zinakuwa na uhaba wa chakula hasa yanapotokea majanga ya ukame, ama migogoro ya vita duniani kama vile vinavyoendelea huko Ukraine. Na kwa kuwa Afrika inaagiza vyakula vya nafaka vikiwemo mchele na ngano kutoka nje ya Afrika, ujuzi huu wa China unaweza kuwakwamua katika dimbwi la kutegemea kuagiza chakula nje na badala yake itakuwa inazalisha yenyewe tena kwa kiasi kikubwa.

Katika mkutano wa kwanza wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mwaka 2006, China iliahidi kujenga vituo 10 vya vielelezo vya kilimo barani Afrika. Mwaka huohuo, kwa mara ya kwanza Yuan Longping akiwa baba wa mpunga chotara na mtaalamu aliyetafiti mpunga alikwenda na timu yake nchini Madagascar, na kuanza juhudi zake za kusaidia kilimo barani Afrika kwa miaka 15.

Kwa maana hiyo juhudi kama hizi zikiendelezwa basi katika siku za mbele, Afrika itakuwa na soko lake la nafaka ambalo litakidhi mahitaji ya Waafrika na hatimaye kuondoa hali ya taharuki na kuombewa misaada na mashirika ya Umoja wa Mataifa pale yanapotokea majanga makubwa hasa ya uhaba wa chakula.
 
Back
Top Bottom