Wachambuzi wa mchongo hawajafurahiswa na ushindi wa Taifa Stars

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Tanzania nakupenda nchi yangu hongereni sana vijana wetu hakika leo mmejitoa kila mtu kafanya majukumu yake, hongera sana benchi zima la ufundi hongereni mashabiki mliojitokeza kuipa joto Taifa Stars ukubwa wa ligi yetu hakika unaanza kuonekana mpaka timu ya Taifa.

Uganda Cranes ni kati ya timu zinazotusumbua sana ukanda wetu, kwa kifupi ndio wakali wa soka kwa ukanda huu hatuna historia nzuri sana tunapokutana nao wametufunga michezo mingi zaidi yetu.

Hakika huu ni mwanzo mzuri wa benchi la ufundi chini ya kocha mpya japo baada ya kutangaza kikosi kama kawaida kuna wapiga kelele waliibuka na kuanza kujifanya nao ni makocha wa Pro UEFA, wapo waliotaka kuona wachezaji wao wanaitwa na kuzusha taarifa zao za kimbeya mitandaoni ila kocha alibaki na misimamo yake.

Yupo mchambuzi mmoja kwa asilimia kubwa leo siku nzuri baada ya Taifa Stars kushinda kwa kifupi alikuwa anataka Stars ifungwe ili aibuke na hoja zake zisizo na mashiko, huyu ndio mchambuzi aliyewaaminisha Watanzania kocha kakosea kutowaita Shomari na Tshabalala hata kufikia kusema kocha ametaka hao jamaa waitwe haraka Taifa stars baada ya picha kusambaa kocha akiwa na vijana hao.

My point is, hawa wachambuzi mimi nawaita wapiga kelele habari zao tuwe tunazisoma kama magazeti ya udaku tu hawawezi kukupa sababu yoyote ya kiufundi na kuishia kuandika udaku tu, mbaya zaidi huyo mchambuzi sio kwamba yupo kwa maslahi ya taifa bali ni mapenzi yake kwa timu wanayotoka hao wachezaji.

Hakika siyo siku nzuri kwake.
 
Kinachonishangaza mimi ni kwa nini sisi huku kwetu tunashindwa kutunza viwanja? Ona ule uwanja waliochezea Uganda na Tanzania leo ile pitch ilivyo halafu linganisha na haya majaluba ya kwetu.

Ccm nao wamejidai kunyakua viwanja vyetu halafu wamevigeuza kuwa maboma ya malisho ya kondoo. Bure kabisa.
 
Timu kupata matokeo chanya haku justify wachezaji wazuri kutoitwa timu ya taifa kua ni sahihi,bado mahitaji ya wachezaji hao wazuri ni makubwa Kutokana na ukubwa wa mashindano yenyewe.

Lazima watu tuelewe kua Mwalimu ametake risk kuwachezesha Job na Novatus out of their natural position,positive thing ni kua imemlipa,siku nyingine yakitokea majanga amini nakuambia atakua kwenye kiti moto kikali sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom