Wabunge waridhia ongezeko la gharama za mawasiliano ya simu!

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Jioni hii wabunge wa CCM ambao ndio wengi wamekataa pendekezo la Mbunge wa upinzani Wenje la kukataa ongezeko la gharama za simu kwa vile limetoka kwa mpinzani.

Serikali ya CCM inataka tutoboke zaidi tutumiapo simu?
Je, hawa wabunge waliosema 'Ndiyoooo' dhidi ya maumivu kwa wananchi wanamwakilisha nani Bungeni?
 
Umepost kishabiki mno.wenje alikuwa anatafuta umaarufu usiokuwa na maana na wewe hujaelewa kilichofanyika kwa kuwa ulijiandaa kupotosha.
 
Acha uongo wewe Gadafi wengi tumetazama sasa pale umaarufu alokua anatafuta Wenje ni upi zaidi ya kutetea walalahoi wengi. Nadhani wewe ndio umechangia kishabiki zaidi shame on you. Tatizo ni bibi ndio kapitisha na siyo wabunge
 
hii hoja imepitishwa kwa nguvu na spika lakini wengi sana walimuunga mkona Wenje!
 
Pale wabunge wanapokuwa si watetezi wa wanaowawakilisha, wanamfaidisha nani???
 
Jioni hii wabunge wa CCM ambao ndio wengi wamekataa pendekezo la Mbunge wa upinzani Wenje la kukataa ongezeko la gharama za simu kwa vile limetoka kwa mpinzani. Serikali ya CCM inataka tutoboke zaidi tutumiapo simu. Jee hawa wabunge walio sema Ndiyoooo dhidi ya maumivu kwa wananchi wanamwakilisha nani Bungeni?
Wanajiwakilisha wenyewe na familia zao tu. Utaki unaacha
 
Acha uongo wewe Gadafi wengi tumetazama sasa pale umaarufu alokua anatafuta Wenje ni upi zaidi ya kutetea walalahoi wengi. Nadhani wewe ndio umechangia kishabiki zaidi shame on you. Tatizo ni bibi ndio kapitisha na siyo wabunge
Huyu ghadafi ni gamba eeh! Yaani ameshindwa kuona kilichofanyika pale?Lakini pia wabunge wa ccmagamba kwanini wasikomae na huyu bi kidude maana wao lazima wajue hii inaeffect kwao kwa wingi na ukizingatia hoja imetoka upinzani hivyo ilikua advantage kwa ccmagamba kuweka uzito hoja ya zito but wao wamenyamaza tuu!hapa hawawezi kuepuka lawama hata kama ni makinda ndo aliyelazimisha
 
Matumizi ya simu hapa nchini mengi ni kuhusu mapenzi na anasa na story za ajabu ajabu ndio mana imekuwa sio kipaumbele
 
Finance Bill 2012 ishapita muda huu huu, maumivu kwa akina kabwela katika mawasiliano sasa kuongezeka hadi 12%. Pamoja na Zitto kuomba kura zihesabiwe baina ya wabunge wetu waliokubali ongezeko hilo kutoka 10% na wale waliopinga, madam Makinda kamaliza mzozo kwamba wanyonge waendelee kulipia gharama mpya, 12%. Vituko vingine vilivyojili jioni hii bungeni ni kauli ya waziri wa fedha kwamba ati serikali ilipendekeza magari yawe na umri wa miaka 8 badala ya 10 kuepuka uchakavu, kodi kubwa, kwamba ati serikali ililenga kumkomboa Mtanzania na uchafuzi wa mazingira, matengenezo, na kwamba magari ya above 10 yrs yanakula sana mafuta ilhali Watanzania hawana uwezo wa kununua mafuta kila mara, nimecheka sana hii maneno.
 
Utamkuta mtu ana simu nne line line tano,voda mbili tgo mbili airtel moja na zantel.ukiangalia majina ya watu ali save ni mahawara zake tuu,kwa hali hiyo lazima alalamikie gharama za mawasiliano.
 
Acha uongo wewe Gadafi wengi tumetazama sasa pale umaarufu alokua anatafuta Wenje ni upi zaidi ya kutetea walalahoi wengi. Nadhani wewe ndio umechangia kishabiki zaidi shame on you. Tatizo ni bibi ndio kapitisha na siyo wabunge

i see,wenje amenenepa kweli wakuu,shavu dodo,naona posho za pale mjengoni miezi mitatu hii zimesaidia sana wabunge
 
Hata kama wapo wa CCM waliomuunga mkono Wenje na Makinda kakandamiza kura,swali ni wale waliosema ndio wanamwakilisha nani?maana kama wana tuwakilisha sisi na hakuna hata mmoja aliyesema ndio halafu Makinda aseme waliosema ndiyo wameshinda kingekuwa kichaa cha karne.
 
Jioni hii wabunge wa CCM ambao ndio wengi wamekataa pendekezo la Mbunge wa upinzani Wenje la kukataa ongezeko la gharama za simu kwa vile limetoka kwa mpinzani. Serikali ya CCM inataka tutoboke zaidi tutumiapo simu. Jee hawa wabunge walio sema Ndiyoooo dhidi ya maumivu kwa wananchi wanamwakilisha nani Bungeni?

We ulitegemea nini? Acha umajinuni. Watu kama Lusinde' Mimi mwenyewe nina simu moja tu hapa lakini kuna wananchi wanasimu zaidi ya mbili hivyo wanaweza kumudu gharama na hivyo kodi iongezwe' Lusinde Mb alitamka Bungeni...Kwa kujiona yupo sawa akashangiliwa...aliongea bila kufanya utafiti ni kwanini wananchi wamekuwa na umiliki wa laini za simu zaidi ya moja na hata simu zaidi ya moja..... Yeye anadhani huyo ndio utajiri, atashindwa kusema NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO had masuburi yanachezacheza...? CDM rudin kwa wananchi, tumeona mchango wenu..tunawakubali tunawaona mlivyo wapigania haki kwetu.....Sijaona mantiki ya kung'ang'ania ongezeko la kodi wakati hili hujaweza ikusanya vilivyo....ati tunajaribu kwenye maisha ya watu?
 
Huyu ghadafi ni gamba eeh! Yaani ameshindwa kuona kilichofanyika pale?Lakini pia wabunge wa ccmagamba kwanini wasikomae na huyu bi kidude maana wao lazima wajue hii inaeffect kwao kwa wingi na ukizingatia hoja imetoka upinzani hivyo ilikua advantage kwa ccmagamba kuweka uzito hoja ya zito but wao wamenyamaza tuu!hapa hawawezi kuepuka lawama hata kama ni makinda ndo aliyelazimisha

gadafi sio gamba sema ana fikra huru,hajabanwa na ndoano za kishabiki za kivyama
 
Ulaji wa mafuta unategemea umri wa gari au cc? Hivi anataka kuniambia vitz ya 2001 cc 990 inakula mafuta sana kuliko Vogue ya 2008 cc4900? Eheeeee imbombo ngafu ndio wataalamu wetu hao!
 
Matumizi ya simu hapa nchini mengi ni kuhusu mapenzi na anasa na story za ajabu ajabu ndio mana imekuwa sio kipaumbele
Ni vema umejionyesha ni mtu wa kundi gani na unaishi kwa mawazo ya wakati gani. Wenzio wa karne hii simu ni kitendea kazi wewe baki na mambo yako ya mapenzi
 
Back
Top Bottom