Wabunge waridhia ongezeko la gharama za mawasiliano ya simu!

Hivi hawa watu wanafikiria Kuongeza Kodi kwa mtumiaji wa simu ili tuende sawa na kenya na Uganda? Mimi nafikiri tungeanza kwa kuboresha kwanza maisha ya mtanzania ili yaendane na maisha ya Wana afrika Mashariki wengine kwanza. Ili basi tulingane kwa kila kitu. Hivi hii jeuri ya kukaidi na kuhisi kila mnachofikiri ni sahihi mmeitoa wapi?
 
Wana JF naomba kukumbushwa hivi kwenye hoja ya wenje walioshinda ni wanaotaka tubaki 10% au magamba wanaotaka tuwachangie 12%, tafadhali na msaada wenu
 
Samahani kwa maneno niliyoyasema mwanzo kwa kweli sikujua kama umri wako ni huu.

Nadhani kila atakayesoma hii post yako atajua umri wako na ata kuonea huruma
yan kweli ukikua utabadilika ngoja tukupe muda, mada ina kuzidi uzito!
you still minor

Mkuu watoto wa fb hao.. Mie niligundua mapema ndo maana cikutaka kumjibu.. Kila kitu wanachukulia easy kwa sababu "dad" yupo.. Credit ananunuliwa kama anavyonunuliwa nguo za kuvaa na kulishwa..

Sent from Tora Bora..
 
Umepost kishabiki mno.wenje alikuwa anatafuta umaarufu usiokuwa na maana na wewe hujaelewa kilichofanyika kwa kuwa ulijiandaa kupotosha.

hebu elezea kilichofanyika ili na sisi wa mbali tuelewe la sivyo nakubaliana na mtoa hoja.
 
Kwa hiyo, zile mbwembwe kuwa Mkongo wa Taifa utaleta unafuu kwa nchi yetu katika teknolojia ya mawasiliano ndiyo sefuri! (e-learning kwenye shule zetu za sekondari vijijini, e-government n.k)

Tatizo kila kitu wanatanguliza siasa,angekuwa mbunge wa ccm nahic spika angesema waliotaka asilimia 10 wameshinda lkn kwa kuwa aliyetoa hoja ni WENJE,Spika mishipa ilimtoka kulazimisha hoja kupita ,ukweli wabunge wengi walipinga
 
Kama watumiaji wa mawasiliano watapunguza kutumia mawasiliano, mapato ya serikali yatapungua au yataongezeka? sijui ni hesabu gani zinatumika hapa ili ku justify kwamba ukiongeza gharama then mapato yanaongezeka pia.
 
Simu ni nyenzo muhimu ya mawasiliano na pia inaokoa muda ni makosa kuihusisha simu na maswala ya mapenzi lakini hiyo imechangiwa zaidi na makampuni ya simu ambayo matangazo yao mengi yanahusu biashara. Hakuna asiyejua kuwa makampuni ya simu ni wakwepaji wakubwa wa kodi badala ya serikali kuangalia namna gani wangeyabana ili walipe kodi wamekimbilia kuwaongezea wananchi mizigo lakini hii imechangiwa na wanahisa wake wakubwa kuwa wanasiasa nani asiyejua takrima walizotoa vodacom kabla ya kuanza bunge, swala la mtu kuwa na line tofauti ni sahihi kwani ukipiga simu toka mtandao mmoja hadi mwingine gharama yake ni heri ungempigia mtu wa ulaya kuliko kuongea Tanzania. Mwisho nawaunga mkono wale wote wanaosema wabunge walijifikiria wao binafsi
 
Sababu zilizotolewa kupunguza umri wa magari kwa kweli hazikuwa na mshiko kabisa. Unamlindaje mwananchi kwa kumlazimisha kununua gari ya bei ghali wakati unajua hata hiyo ya bei nafuu hataiweza? Mimi nadhani sababu ya msingi ili kuwa ni kuongeza mapato kutoka kwa wanyonge na kuwakandamiza zaidi.

Hii itasabisha gharama ya ukusanyaji wa kuodi kuwa kubwa kwa kuwa itawatia moyo (encourage) watu kukwepa kodi na kuongeza rushwa kwa maafisa wa TRA.
 
Acha uongo wewe Gadafi wengi tumetazama sasa pale umaarufu alokua anatafuta Wenje ni upi zaidi ya kutetea walalahoi wengi. Nadhani wewe ndio umechangia kishabiki zaidi shame on you. Tatizo ni bibi ndio kapitisha na siyo wabunge

Mwanasiasa akutetee wewe? utampa nini wewe? anakujali siku ya kukuomba kura tu. Slaa huyo anakopa chama. Nenda wewe uone kama utakopeshwa hata nauli ya kwenda kwenu.
 
Insanity is doing the same thing in the same way (kama kuchagua ccm) while expecting different results!!
 
Mwanasiasa akutetee wewe? utampa nini wewe? anakujali siku ya kukuomba kura tu. Slaa huyo anakopa chama. Nenda wewe uone kama utakopeshwa hata nauli ya kwenda kwenu.

we ukilala ukiamka unamuwaz slaa mkumbuke baba na mama yako wapo bush wanashndia uji na ugoro upo mjini unalea kitambi.
 
Ninaloweza kusema kwa mtu mzima au kijana mwenye uwezo wa kupambanua mambo ni uwendawazimu kushabikia maigizo ya wabunge wa ccm hasa hoja ya utetezi kwa wananchi inapotolewa na wapinzani
 
Jioni hii wabunge wa CCM ambao ndio wengi wamekataa pendekezo la Mbunge wa upinzani Wenje la kukataa ongezeko la gharama za simu kwa vile limetoka kwa mpinzani.

Serikali ya CCM inataka tutoboke zaidi tutumiapo simu?
Je, hawa wabunge waliosema 'Ndiyoooo' dhidi ya maumivu kwa wananchi wanamwakilisha nani Bungeni?

Mi naona gharama za simu ziongezwe lakini cha juu kiingizwe kwenye source of income ya serikali. Na kwa sababu watumiaji wa simu ni wengi sana serikali itakusanya fedha mingi sana, au wakuu?
 
Umepost kishabiki mno.wenje alikuwa anatafuta umaarufu usiokuwa na maana na wewe hujaelewa kilichofanyika kwa kuwa ulijiandaa kupotosha...............

Ha!ha!hah! hivi watu kama nyie mnakuwa ni watu au mizimu? bado sijawaelewa na mwenzio rejao.
 
Tusubiri tuone maigizo haya yatatupeleka wapi. Wameshusha bei ya nguzo na kuunganishiwa umeme wakasahau tatizo si kuunganishiwa tu, hata bei ya umeme wenyewe.
 
Back
Top Bottom