BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,379
- 8,123
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema ofisi yake tayari imepokea majina ya Wabunge waliofanya safari za nje ya Nchi na kukiuka maelekezo ya madaraja waliyopaswa kutumia hivyo wataandikwa barua ili walipe gharama hizo.
Kwa mujibu wa Spika, Wabunge wanastahili kupewa tiketi za 'Business Class' na huduma zilizopo chumba cha daraja hilo hilo na sio VIP ambayo ina gharama za ziada na Ofisi ya Katibu wa Bunge imekuwa ikitoa maelekezo kuhusu matumizi ya madaraja hayo.