Naomba kujuzwa tofauti ya huduma katika madaraja (classes) za ndege

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,821
Wakuu mimi sijawahi kupanda ndege ila nasikia kwenye ndege hizi mfano za kwetu kutoka dar to mwanza safari ya Lisaa limoja kuna madaraja nayasikia kuna economy class,business class na first class.Je tofauti yake ni huduma gani za ziada unazopata ukiwa class ya bei kubwa na zipi huzipati ukilipia nauli ndogo hasa kwa safari za ndege zetu za hapa nchini.
 
Kiufupi kadri class inapanda kuna utofauti wa vyakula, vinywaji, privacy, customer care, utaratibu wa kupanda na kushushwa kwenye ndege, n.k.

Ukipanda economy class utaitamani business class

Ukipanda business class utaitamani first class

Ukipanda first class utatamani ukodishe private jet

Ukikodi private jet utatamani uimiliki upige nayo Misele.
 
Wakuu mimi sijawahi kupanda ndege ila nasikia kwenye ndege hizi mfano za kwetu kutoka dar to mwanza safari ya Lisaa limoja kuna madaraja nayasikia kuna economy class,business class na first class.Je tofauti yake ni huduma gani za ziada unazopata ukiwa class ya bei kubwa na zipi huzipati ukilipia nauli ndogo hasa kwa safari za ndege zetu za hapa nchini.
1.Seat za kukaa na nafasi kati ya seat na seat zinatofautiana.
2.Wingi wa vyakula na vinywaji na kipaumbele cha kuvipata
3.Nani aanze kupanda ndege na kuteremka kwanza
4.Ubora wa sehemu ya kusubiri kabla ya kupanda ndege
5.Urahisi wa kubadisha siku ya kusafiria kwa gharama nafuu
6. Wingi na uzito wa mizigo unayoweza kusafiri nayo
NB: Siyo kila ndege zina first class hasa za masafa mafupi.
 
Hata waliokufa wengi Titanic walikua class za kawaida.
So hata jambo likitikea rescue huanza na Hawa first class.
Siyo kwamba walikuwa wengi kwa sababu ndiyo class inayochukuwa watu wengi? Halafu kwenye meli kama hizi cruise ship mara nyingi first class zinakuwa sehemu ya juu ya meli hivyo kwenye ajali inaweza ku-play positively au negatively Kuhusu rescue, hawachagui. Kwenye dhararu mtu yoyote anayewahi kufikiwa anaokolewa.
 
Hata waliokufa wengi Titanic walikua class za kawaida.
So hata jambo likitikea rescue huanza na Hawa first class.
Nope !!! Kuna uwezekano wa kuwa na vyombo vya kuokoka ambavyo havitagombaniwa na wingi wa watu lakini linapokuja suala la kuokoa mara nyingi wanaoanza kuokolewa ni wanawake na watoto..... (Nadhani kiubinadamu wewe baba mzima kama ni kwenye boti unagagania kupanda boti wakati kuna watoto hata ukipona Jamii haitakuelewa)
 
Back
Top Bottom