Wabunge wagoma kupunguza Ushuru

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
BUNGE limekataa kupitisha Azimio la
Serikali la kutaka kupunguza ushuru wa
maji kwa madai kuwa kiwango
kilichopunguzwa hakimgusi mlaji wa
chini.
Azimio hilo lilitaka Bunge hilo kupitisha punguzo la ushuru wa maji ya chupa,
kutoka Sh 69 hadi Sh 12 kwa lita. Kwa
mujibu wa Azimio hilo, Serikali
ingepungukiwa mapato kwa Sh bilioni
7.7 ambayo ilipanga kufidia upungufu
huo kwa kupunguza posho, fedha za makongamano, ununuzi wa magari na
safari za ndani na nje ya nchi.
Uamuzi wa kukataa kupitisha Azimio
hilo, ulifikiwa bungeni jana na Naibu
Spika Job Ndugai, baada ya kuhoji
wabunge na kundi la waliolikataa Azimio kushinda la waliotaka lipitishwe.
Kabla ya Ndugai kuhoji wabunge hao,
Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba
(CCM) aliomba Mwongozo akitumia
kanuni ya 58 ya Bunge na kutaka hoja
hiyo iondolewe na kurejeshwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi, kwa
kuwa haijazingatia maslahi ya
mwananchi wa chini.
“Kwa kanuni ya 58 naomba wabunge
wenzangu mniunge mkono hoja hii
iondolewe na kurejeshwa serikalini kufanyiwa kazi zaidi, kwa kuwa hilo
punguzo la Sh 57 katika ushuru wa maji,
kamwe halitamfikia mlaji wa kawaida
zaidi ya kunufaisha wenye viwanda,”
alisema.
Hata hivyo, Ndugai alikataa kutoa Mwongozo kuhusu hoja hiyo kwa kuwa
Mbunge huyo alitumia kanuni tofauti na
inayotakiwa. “Kanuni uliyopaswa
kutumia ni ya 69 inayosema Mbunge
anaweza kuomba hoja iondolewe na
kutoa sababu zake, lakini kanuni ya 58 inasema Mbunge anaweza kupendekeza
mabadiliko katika hoja,” alisema Ndugai
Alisema kutokana na Mbunge huyo
kukosea kanuni, kwa mamlaka aliyonayo
kupitia kanuni hizo za Bunge, ataendelea
kuhoji, jambo ambalo hata hivyo, walishinda waliokataa baada ya
kuhojiwa. Akiwasilisha Azimio hilo,
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, alisema
kupitia Sheria ya Fedha na Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa katika bajeti ya
mwaka huu, Serikali iliweka ushuru wa Sh 69 kwa lita ya maji ya chupa.
Hata hivyo, alisema kutokana na
malalamiko kuhusu ongezeko hilo la
ushuru, Serikali ilifanya tathmini na
kubaini kuwa bei ya maji ya chupa
ilipanda kwa kiasi kikubwa na kuwafanya watumiaji wengi kushindwa
kumudu na hivyo kutumia maji yasiyo
salama.
Alisema tathmini hiyo pia ilibaini
kwamba ongezeko la ushuru huo
lilisababisha bei za maji yanayozalishwa katika viwanda vya nchini, kuwiana na
bei za maji yanayoagizwa nje na hivyo
kuondoa ushindani, jambo ambalo
limeathiri uzalishaji wa viwanda nchini
na kupunguza mapato ya ndani na ajira.
“Sheria ya Ushuru wa Bidhaa inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana na
fedha kupitia amri itakayochapishwa
kwenye Gazeti la Serikali, kufanya
marekebisho kwa lengo la kupunguza au
kuongeza ushuru ulioainishwa,” alisema
Mkulo. Alisema tangazo la kupunguza ushuru
huo na kufikia Sh 12 sawa na asilimia 10
ya wastani wa bei ya kiwandani ya
uzalishaji ambayo ni Sh 120 kwa lita,
lilitolewa Septemba mwaka jana, ili
kuwawezesha wananchi wa kawaida wasiopata maji safi na salama, kumudu
gharama za ununuzi wa bidhaa hiyo.
Mkulo alisema baada ya kurekebisha
ushuru wa bidhaa hiyo, matokeo ya
mapato yanayotarajiwa kwa kipindi cha
Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu ni Sh bilioni 2.7 wakati kupitia ushuru
wa Sh 69 yangekuwa Sh bilioni 15.5.
Alisema mapendekezo ya kupunguza
ushuru huo kutoka Sh 69 hadi Sh 12 kwa
lita ya maji ya chupa, yataleta upungufu
wa mapato kwa Sh bilioni 12.8 na kupitia ushuru huo, Serikali inatarajia
kukusanya Sh bilioni 2.7 yaani kila
mwezi itatakiwa kukusanya Sh milioni
225.
Alisema kutokana na upungufu huo,
Serikali inapendekeza kuziba nakisi hiyo kwa kupunguza matumizi yake katika
maeneo ya posho, fedha za
makongamano, ununuzi wa magari,
samani, gharama za uendeshaji ofisi,
mafunzo ya ndani na nje, safari za ndani
na nje na ukarabati wa majengo. Kamati ya Bunge
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na
Uchumi, Dk Abdallah Kigoda, akichangia
maoni ya kamati hiyo kuhusu Azimio
hilo, alipongeza hatua hiyo ya kupunguza
ushuru wa maji na kuitaka Serikali kuhakikisha inachukua hatua madhubuti
za kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za
ndani.
Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha,
Christina Mughwai, akiwasilisha maoni
ya Kamati ya Kambi ya Upinzani, alisema Kamati yake inaishauri Serikali
kuangalia pia maeneo mengine ya
kupunguza ushuru kama vile dizeli hali
ambayo itasaidia kupunguza mfumuko
wa bei.
Wakichangia kwa nyakati tofauti, wabunge walitofautiana kuhusu Azimio
hilo ambapo baadhi yao akiwamo
Mbunge wa Viti Maalum, Zarina Madabida
(CCM) na Tizeba, walikataa kuliunga
mkono na kutaka lifanyiwe
marekebisho, kwa kuwa punguzo hilo la ushuru halijamgusa mwananchi.
Mbunge wa Wawi Hamad Rashid
Mohamed (CUF), Mbunge wa Lushoto
Henry Shekifu (CCM), Mbunge wa Kalenga,
William Mgema (CCM) na wa Kisarawe,
Selemani Jaffo (CCM) walisema kwa nyakati tofauti kuwa ni aibu kwa
Serikali kuagiza maji nje na kutaka
ushuru uongezwe kwa maji hayo.
Hamad alitaka Serikali kuhakikisha
inakabiliana na mfumuko wa bei ikiwa
ni pamoja na kuzingatia maeneo ya kupunguzia matumizi kwa kuwa
mengine bado ni muhimu hoja
iliyoungwa mkono na Mbunge wa Viti
Maalumu, Leticia Nyerere (Chadema).
Source: Habari Leo
 
kuna maajabu mengi sana yanasubiri zamu yeo kutokea nchini TZ, ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom