Wabunge wa CCM wasaliti wa serikali yao?

Kalambo Junior

Senior Member
Jul 15, 2011
127
23
Ingawa wabunge wa CCM,Alhamisi usiku walifanya kikao cha kamati ya chama kuweka mkakati wa kutoipinga bajeti ya wizara ya Nishati na Madini,lakini hali inaonyesha kuwa tofauti kabisa.Tayari, wabunge wengi wakiwamo wa CCM wametoa misimamo mikali dhidi ya bajeti hii tofauti na wizara nyingine ambazo zilipingwa na upinzani pekee.Zimesikika kauli kali za wabunge wa CCM kama vile"Hapa patachimbika" "Nitaunga mkono wapinzani kuwa serikali hii ni legelege","waziri amesema uongo" "waziri anapendelea miradi katika majimbo ya maswahiba wake"na siungi mkono hoja".Je katika hili hawa wabunge wa CCM wanamaanisha wanacho kiongea? kama ndio,je watakuwa ni wasaliti kwa serikali yao?.
 
Huo ni mchezo wa kisiasa, kujadili kwa koponda ili wananchi wafurahi, sote tunajua baadae bajeti itapita tu. Hii yote ni calculated move.
 
Kuchangia ni tofauti na kupitisha,subiri bunge litakapokaa kama kamati kifungu kwa kifungu ndo utawajua undani wao
 
Kuchangia ni tofauti na kupitisha,subiri bunge litakapokaa kama kamati kifungu kwa kifungu ndo utawajua undani wao
 
wananifurahishaga pale wanaposimama na kutoa mamalamiko yao juu ya bajeti wakimaliza utasikia NAUNGA MKONO HOJA KWA ASILIMIA 100
 
wanaoafiki waseme ndio................... Magamba wote ndiooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo! F****ck
 
Nyerere aliwahi kusema kazi ya bunge ni kuipa serikali misukosuko.nitawashangaa wakipitisha hii bajeti halafu tuendelee kukaa gizani.
 
Ingawa wabunge wa CCM,Alhamisi usiku walifanya kikao cha kamati ya chama kuweka mkakati wa kutoipinga bajeti ya wizara ya Nishati na Madini,lakini hali inaonyesha kuwa tofauti kabisa.Tayari, wabunge wengi wakiwamo wa CCM wametoa misimamo mikali dhidi ya bajeti hii tofauti na wizara nyingine ambazo zilipingwa na upinzani pekee.Zimesikika kauli kali za wabunge wa CCM kama vile"Hapa patachimbika" "Nitaunga mkono wapinzani kuwa serikali hii ni legelege","waziri amesema uongo" "waziri anapendelea miradi katika majimbo ya maswahiba wake"na siungi mkono hoja".Je katika hili hawa wabunge wa CCM wanamaanisha wanacho kiongea? kama ndio,je watakuwa ni wasaliti kwa serikali yao?.
si wasaliti kazi ya wabunge ni kusimamia masilai ya wanannchi si serikali sema siku zote wabunge wanatusaliti wanannchi tusubili kupinga ni hatuwa ya 1 jee? Kupitisha ndiyooooooooo kama wamenawa uso na kukumbuka kuwajibika kwa wanannchi
 
Huo ndio mkakati mpya waliobuni ili kukabiliana na nguvu ya kambi ya upinzani. Wanapangiana nani apinge au ahoji kipi wakati wa mjadala ili wananchi waanze kuwa na matumaini ya kuwakilishwa ipaswafyo. Lakini ikifika wakati wa kupitisha bajeti, wote wataunga hoja hiyo hiyo waliyokuwa wanapinga kwa asilimia mia na moja!!! Janja ya nyani kula hindi bichi - lakini wananchi wameishapata semina elimishi ya kutosha na wanaijua hii janja.
 
si wasaliti kazi ya wabunge ni kusimamia masilai ya wanannchi si serikali sema siku zote wabunge wanatusaliti wanannchi tusubili kupinga ni hatuwa ya 1 jee? Kupitisha ndiyooooooooo kama wamenawa uso na kukumbuka kuwajibika kwa wanannchi
Ni kweli mkuu,hawa wabunge wanatakiwa wawajibike kwa sisi wanainchi lakini sikuzote hawa wamagamba wamekuwa wakiwajibika kwa serikali yao.Hivyo kama wataipinga kwa dhati bajeti hii ni dhahiri kuwa itakuwa sawa na kuisaliti serikali yao.
 
Mbona bajeti ilishapitishwa! Sasa ni fomalite basi. Bila katiba mpya hakuna kitu wala maendeleo.
 
Back
Top Bottom