Wabunge viti Maalumu Katavi watoa Milion 6 Maendeleo ya Chama na UWT

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Wabunge viti Maalumu Katavi watoa Milion 6 Maendeleo ya Chama na UWT.

WABUNGE wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi wametoa shilingi Milioni 6 Kwaajili ya kusaidia Maendeleo ya Chama na Jumuiya ya UWT ili kuhakikisha Chama na Jumuiya ya UWT zinaendelea kuimalika.

Wabunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi wametoa shilingi Milioni 6 Kwaajili ya kusaidia Maendeleo ya Chama na Jumuiya ya UWT ili kuhakikisha Chama na Jumuiya ya UWT zinaendelea kuimalika

Wakiwa katika Kikao Cha Baraza la UWT Mkoa wa Katavi wabunge hao Martha Mariki,na Taska Mbogo wamesema kuwa wanafanya hivyo Kwa maslahi Makubwa ya Chama na Jumuiya ya UWT Kwakuwa wametokana na Jumuiya hiyo

Marth Mariki Mbunge wa Viti maaalum Mkoa wa Katavi ametoa Shilingi Milioni 2 kwaajili ya kudaidia Ukarabati wa ofsisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda nakubainisha kuwa anatoa mchango huo Kwa kutambua umuhimu wa chama Cha Mapinduzi Kwa nafasi aliyonayo.

"Ndugu wanachama wenzangu wa UWT natoa shilingi Milioni 2 Ili kusaidia Ukarabati wa ofisi ya chama Cha mapinduzi Wilaya ya Mpanda"amesema Mbunge Martha Mariki

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalimu mkoa wa Katavi Taska Mbogo ametoa ametoa Shilingi Milioni 4 ,Milioni3 kwaajili ya kusaidia Ujenzi wa nyumba za watumishiUWT Kwa Wilaya za Mpanda,Mlele na Tanganyika na shilingi Milioni 1 kwaajili ya ukarabati wa Ofisi ya chama Cha mapinduzi [CCM] mkoa wa Katavi.

‘’Mimi kama Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa nachangia Milioni nne Milioni Moja Moja Kwa Kila wilaya Kwaajili ya kusaaidia Ujenzi wa nyumba ya UWT Kwenye wilaya ya Mlele,Tanganyika na Mpanda na Milioni Moja kwaajili ya kuendeleza ukarabati wa ofisi ya Chama chetu Mkoa wa Katavi’’amesema Taska.

Pamoja na hayo wabunge hao wamebainisha mikakati mbalimbali ya kuwatumikia wananchi na UWT Kwa ujumla Kwa lengo la kuisadia jumuiya Hiyo kiuchumi kupitia miradi mbalimbali kuanzia ngazi ya Kata Hadi Mkoa.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Idd Kimanta ambae alikuwa mgeni Rasimi katika Baeaza hilo amaewashukuru wabunge hao kwa kuguswa na kuona umuhimu wa kuendelea kukisaidia chama na jumuiya ya UWT kwa Ujumla.
 

Attachments

  • 1.JPG
    1.JPG
    37.8 KB · Views: 6
  • 2.JPG
    2.JPG
    42.3 KB · Views: 5
  • 3.JPG
    3.JPG
    26.5 KB · Views: 5
  • 4.JPG
    4.JPG
    21.9 KB · Views: 5
  • 5.JPG
    5.JPG
    38.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom