Wabunge Vijana waishambulia serikali

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Mdee1(4).jpg

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee


Wabunge vijana jana waliishambulia serikali wakisema imeweka vikwazo kwa vijana kupata ajira na kutoa upendeleo kwa wazee katika ajira nyingi za umma hasa nafasi za uongozi.
Wakichangia kwa hisia kali mjadala wa Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Vijana wa Afrika wa mwaka 2006 bungeni jana, wabunge wengi vijana walisema tatizo la ajira kwa vijana linazidi kuwa kubwa nchini kutokanaa na vikwazo mbalimbali vinavyowazuia kupata ajira za serikali na kutotengenezewa mazingira mazuri ya vijana kujiajiri.
Katika mjadala huo, wabunge hao walisema Serikali imekuwa haiwaamini vijana kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa yatakayosaidia taifa na wananchi, hivyo kuwaweka pembeni na kuonekana watu wasiofaa.
Walisema kigezo cha uzoefu wa kazi kwa muda mrefu katika matangazo ya ajira za umma, kimekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana hasa wanaomaliza elimu ya juu kupata ajira ili waweze kutoa mchango wao kwa taifa lao na kutaka kigezo hicho kiondolewe.
Wa kwanza kuwasha moto alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Bulaya, ambaye aliwashambulia wazee kuwa ni tatizo kwa vijana kupata ajira kutokana na kuweka vikwazo vinavyosababisha kuwa vigumu vijana kupenya.
Alisema vijana wanapotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi au ubunge, hupata wakati mgumu na kuonya kuwa hali hiyo ikiendelea uvumilivu utawashinda vijana na kupambana na wazee kwa njia zozote.
Mbunge wa Mbozi Mgharibi (Chadema), David Silinde, alisema nafasi nyingi za juu serikalini zinashikwa na wazee, huku vijana wanaoweza kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi wakiwekwa pembeni.
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, aliitaka serikali kujifunza kwa yanayotokea katika nchi za Afrika Kaskazini, ambako alisema makundi ya vijana waliokata tamaa na kuingia mitaani na kusababisha ghasia.
“Ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji. Serikali ijifunze kwa yanayotokea katika nchi za Afrika Kaskazini, matatizo haya ya vijana yasiposhughulikiwa haraka ni bomu litakalokuja kutuchoma wenyewe,” alisema.
Aliitaka serikali kuweka mazingira mazuri kwa vijana kusoma na kuacha kufukuzwa hovyo wanafunzi wa elimu ya juu hasa wale wanaoonekana kuwa na mapenzi na vyama vya upinzani.
Naye Mbunge wa Viti Maaluum (CCM), Zainab Kawawa, aliitaka serikali kutatua haraka tatizo la ajira kwa vijana kwani linaweza kuiyumbisha nchi.
“Vijana wengi wanaingia katika maandamano kutokana na kutokuwa na la kufanya, msiwachukie watafutieni ajira maana mtu akiwa na kazi ya kufanya hawezi kupoteza muda wake kwenye maandamano.
Hata hivyo, aliwataka vijana kuacha kuilalamikia serikali kwa kila kitu, badala yake wajishughulishe na mambo mbalimbali ya maendeleo.
“Vijana wanatakiwa kufanya jitihada kufanya shughuli mbalimbali badala ya kusubiri kufanyiwa kila kitu, Ester Bulaya ni kijana amefika hapa kwa jitihada zake. Mdee amefika hapa kwa jitihada zake. Hata mimi nimefika hapa kwa jitihada zangu ingawa kuna maneno huko mitaani eti ni kwa sababu ni mtoto wa Kawawa. Tumefika hapa kwa jitihada zetu hivyo vijana wengine nao waongeze jitihada bila kukata tama,” alisema.
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, alisema vijana wamechoka kupuuzwa na sasa wameanza kujipanga kuhakikisha wanakamata ngazi mbalimbali za uongozi.
“Nafasi zote za uongozi wanapewa wazee. Angalia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, mabalozi, wakurugenzi wote utakuta ni wazee waliostaafu. Tunataka serikali ituamini kuwa vijana tuna uwezo, tuna busara, tuna nguvu ya kufanya kazi” alisema.
Awali, akitoa maoni ya Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jenister Mhagama, aliishukuru serikali kwa kuridhia azimio hilo, akisema litasaidia vijana kujiendelea na kushiriki katika masuala mbalimbali ya kielimu, uongozi, siasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Alisema vijana ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote, hivyo watumike vizuri kwa kushirikishwa katika masuala mbalimbali.
Akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Msemaji wa Kambi hiyo, Joseph Mbilinyi, aliitaka serikali kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa vijana, wakiwamo waliopo vijijini.
Alitaka vijana wanaojiajiri kwa kufanya biashara ndogondogo, kutonyanyasa kwa kuondolewa katika maeneo yao na kuharibiwa mali zao bali wasaidiwe na kutafutiwa maeneo ya kuendesha biashara zao kwa kuwashirikisha.



CHANZO: NIPASHE
 
Mtazamo wa kupanua ajira nchini ni vyema ukalenga zaidi kusaidia utengenezaji wa ajira binafsi na kwa hili sera na sheria mbalimbali za tozo za mapato (kodi) hususani ya VAT ya 1997, Stamp Duty 2002, Mapato 2004 n.k, Ufllisi ya 1996, Uwekezaji 1997 na pamoja na mpango mzima wa kurasimisha rasilimali za wanyonge (MKURABITA) ni sharti zipitiwe upya ili ziweze kusaidia kutengeneza mazingira ya watu kuweza kujiajiri wenyewe na kuwa katika sekta rasmi. Ni vyema serikali kuu na zile za mitaa zikawa zinazungumza kauli moja kwenye suala la kusaidia ajira za vijana na wanyonge kwa ujumla na sio mara ooh MKURABITA huku halmashauri zikitoza viwango vya kuumiza wanyonge kama kodi.
 
Waziri Mponda ndio anasoma tamko la serikali juu ya mgogoro wa madaktari hivi sasa... fuatilia TBC au Star Tv
 
Back
Top Bottom