Wabunge nao walipwe pension kwa kikokotoo cha asilimia 33%. Kama Rais Samia unaona hicho ndio kinachofaa, basi kifae kwa wote!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,039
Kuna mambo mengine huwa yanakera sana!! Kama Rais Samia anaamini kwa dhati IMANI ya CCM kuwa binadamu wote ni sawa na kuwa kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, inakuwaje akaona kuwa watumishi wengine wanastahili mafao kwa kikokotoo cha asilimia 33% wakati wabunge wao wanakomba zote kwa kikokotoo cha asilimia 100%.

Hapo imani yake kama mwana CCM iko wapi? Utaaminije kuwa wanadamu wote ni sawa wakati mmoja unampa mafao asilimia 100% wakati mwingine unampa asilimia 33%, halafu utarajie kuwa huyu uliyempa asilimia 33% ataona unathamini utu wake sawa na huyu uliyempa asilimia 100%? Tuambizane ukweli hapo hakuna cha usawa wala nini zaidi ya upendeleo wa wazi! Suluhu ni moja tu, wote wapate asilimia 33% au wote wapate asilimia 100%.

Vinginevyo mama atuambie hawa wanaopata asilimia 100% wana ziada gani katika utu wao? na hawa wanaopata asilimia 33% wana upungufu gani katika utu wao??. Kama kikokotoo cha asilimia 33% kinafaa basi kifae kwa wote! na kama hakifai kisifae kwa wote!!

Poleni sana watumishi wa umma ambao mliokuwa PPF na NSSF kabla ya wote kuhamishiwa PSSSF maana MPAKA LEO mkistaafu mmekuwa mkipewa mafao kwa kikokotoo cha asilimia 25% wakati wenzenu waliokuwa LAPF na PSPF wanapata mafao kwa kikokotoo cha asilimia 50%, na serikali ilifumbia macho double standard hii!!

Hebu kwa wasiozijua imani na ahadi za wana ccm (ambao ndio waliounda serikali iliyoko madarakani) niwatupie hapa muone kama wenyewe wanazitekeleza au ni kiini macho:

IMANI YA CCM​

  • Binadamu wote ni Sawa
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
  • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Karibuni kwa mjadala (bila matusi)!
 
Wewe unataka kuwapokonya wabunge tonge mdomoni. mbingunikwetu unafikiri ukiwa na njaa unatunga sheria nzuri, waache wabunge wale kwa urefu wa kamba zao
 
Lakini tuambizane ukweli na siyo kudanganyana kuwa ccm inaamini kuwa binadamu wote ni sawa, wakati vitendo ni kinyume chake!
 
Ukiwa kiongozi wa CCM lazima uwe tapeli,muongo.
CCM hawajali usawa.
CCM hawajali Watanzania wadogo.
CCM inajali maslahi ya kakikundi chao tawala tuu.
 
Kuna gari moja nililiona limeandiokwa: "Ubinadamu kazi", nimeamini kabisa, tena ni kazi ambayo watawala wengi hawaiwezi!
 
Wazo zuri ingawa umeandika kwa kurudia rudia sana, ila umesahau kuwa binadamu wote ni sawa kimaumbile ila sio haki sawa,

haki sawa tumeahidiwa kwenye vitabu vitakatifu ndo tutaipata huko
 
Kuna mambo mengine huwa yanakera sana!! Kama Rais Samia anaamini kwa dhati IMANI ya CCM kuwa binadamu wote ni sawa na kuwa kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, inakuwaje akaona kuwa watumishi wengine wanastahili mafao kwa kikokotoo cha asilimia 33% wakati wabunge wao wanakomba zote kwa kikokotoo cha asilimia 100%.

Hapo imani yake kama mwana CCM iko wapi? Utaaminije kuwa wanadamu wote ni sawa wakati mmoja unampa mafao asilimia 100% wakati mwingine unampa asilimia 33%, halafu utarajie kuwa huyu uliyempa asilimia 33% ataona unathamini utu wake sawa na huyu uliyempa asilimia 100%? Tuambizane ukweli hapo hakuna cha usawa wala nini zaidi ya upendeleo wa wazi! Suluhu ni moja tu, wote wapate asilimia 33% au wote wapate asilimia 100%.

Vinginevyo mama atuambie hawa wanaopata asilimia 100% wana ziada gani katika utu wao? na hawa wanaopata asilimia 33% wana upungufu gani katika utu wao??. Kama kikokotoo cha asilimia 33% kinafaa basi kifae kwa wote! na kama hakifai kisifae kwa wote!!

Poleni sana watumishi wa umma ambao mliokuwa PPF na NSSF kabla ya wote kuhamishiwa PSSSF maana MPAKA LEO mkistaafu mmekuwa mkipewa mafao kwa kikokotoo cha asilimia 25% wakati wenzenu waliokuwa LAPF na PSPF wanapata mafao kwa kikokotoo cha asilimia 50%, na serikali ilifumbia macho double standard hii!!

Hebu kwa wasiozijua imani na ahadi za wana ccm (ambao ndio waliounda serikali iliyoko madarakani) niwatupie hapa muone kama wenyewe wanazitekeleza au ni kiini macho:

IMANI YA CCM​

  • Binadamu wote ni Sawa
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
  • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Karibuni kwa mjadala (bila matusi)!
Kuna vitu vya msingi huelewi tunapozingatia usawa wa binadamu.
Kwa usawa unaozungumzia wewe unadhani kila mtu anaweza kuwa Rais au Jaji Mkuu au Askofu au Shekh Mkuu.
Hujui kama kuna mwanamke na mwanaume au vijana na wazee au watoto na watu wazima hawa kuna mambo ya msingi kabisa ambayo hawawezi kuwa sawa hata iweje....
Aidha utu wa binadamu una madaraja ya asili na ya kutengenezwa.
Ukienda mahakamani na dhana ya defamation ndio utagundua wengine wana utu, hadhi na heshima ya mabilioni ilihali wengine ni tumilioni kulingana na jinsi walivyoutengeneza utu wao.
Aidha utu hautumiki kila eneo.. Chukulia ajira hatuajiriwi kwa utu bali uwezo na sifa. Hata miujiza ya mitume na manabii au maombi mbele ya Muumba yana mipaka.
 
Mafao ya uzeni ni kwaajili ya maisha baada ya kustaafu na si kwajili ya unapostafu tu- wazee wengi siku hizi wanaishi maisha marefu miaka zaidi ya 15 baada ya kustaafu (watakula nini kama utawapa kila kitu wanapostafu - kumbuka hawa posho yao haibadiliki mpaka watakapo iaga dunia) Wabunge wapo tofauti - mbunge hana uhakika wa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wabunge wengine walishafanya kazi za kuajiliwa na wapo kwenye mifuko ya pensheni kama wafanyakazi wengine. hapo sijui wanalipwaje pensheni hizo mbili? Mifuko ya pensheni haiwezi kulipa asilimia 100 kila mtu anayestaafu, vile vile mifuko iliyokuwa inalipa asilimia 50 yote ilikuwa taabani- ilishindwa kulipa waastafu kwa wakati muafaka. Hata hii asilimia 33 ni kubwa - mifuko itaanza kuyumba. Mifuko yetu imewekeza kwenye miradi mingi ambayo haina tija yoyote- imepoteza pesa za wateja wao, ipo kwenye hatari ya kufilisika kabisa kama itaendeshwa kisiasa badala ya kufuata wataalamu wa Fedha.
 
Wazo zuri ingawa umeandika kwa kurudia rudia sana, ila umesahau kuwa binadamu wote ni sawa kimaumbile ila sio haki sawa,

haki sawa tumeahidiwa kwenye vitabu vitakatifu ndo tutaipata huko
Kurudia rudia ni staili ya kusisitiza!!
 
Mafao ya uzeni ni kwaajili ya maisha baada ya kustaafu na si kwajili ya unapostafu tu- wazee wengi siku hizi wanaishi maisha marefu miaka zaidi ya 15 baada ya kustaafu (watakula nini kama utawapa kila kitu wanapostafu - kumbuka hawa posho yao haibadiliki mpaka watakapo iaga dunia) Wabunge wapo tofauti - mbunge hana uhakika wa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wabunge wengine walishafanya kazi za kuajiliwa na wapo kwenye mifuko ya pensheni kama wafanyakazi wengine. hapo sijui wanalipwaje pensheni hizo mbili? Mifuko ya pensheni haiwezi kulipa asilimia 100 kila mtu anayestaafu, vile vile mifuko iliyokuwa inalipa asilimia 50 yote ilikuwa taabani- ilishindwa kulipa waastafu kwa wakati muafaka. Hata hii asilimia 33 ni kubwa - mifuko itaanza kuyumba. Mifuko yetu imewekeza kwenye miradi mingi ambayo haina tija yoyote- imepoteza pesa za wateja wao, ipo kwenye hatari ya kufilisika kabisa kama itaendeshwa kisiasa badala ya kufuata wataalamu wa Fedha.
Tunachotaka ni usawa kwa kiwango chochote kitakachokubalika!! Huu ubaguzi ndio unaleta kichefu chefu!!
 
Ukisoma mambo ya CCM, kuanzia katiba, itikadi na ahadi, zisome kisha uzigeuze uone kinyume chake kinavyokuwa.
 
Sheria wanatunga wao kwa maslahi ya watanzania wote,hata mimi nilikuwa na wazo kama hilo
 
Kuna vitu vya msingi huelewi tunapozingatia usawa wa binadamu.
Kwa usawa unaozungumzia wewe unadhani kila mtu anaweza kuwa Rais au Jaji Mkuu au Askofu au Shekh Mkuu.
Hujui kama kuna mwanamke na mwanaume au vijana na wazee au watoto na watu wazima hawa kuna mambo ya msingi kabisa ambayo hawawezi kuwa sawa hata iweje....
Aidha utu wa binadamu una madaraja ya asili na ya kutengenezwa.
Ukienda mahakamani na dhana ya defamation ndio utagundua wengine wana utu, hadhi na heshima ya mabilioni ilihali wengine ni tumilioni kulingana na jinsi walivyoutengeneza utu wao.
Aidha utu hautumiki kila eneo.. Chukulia ajira hatuajiriwi kwa utu bali uwezo na sifa. Hata miujiza ya mitume na manabii au maombi mbele ya Muumba yana mipaka.
Hakuna aliyesema kila mtu anaweza kuwa rais!! lakini utu wa rais na utu wa askari haupishani!! Wote ni sawa kama binadamu!! Kumbuka hata mafao siyo kuwa tunasema tupate pesa sawa maana kipato kinatofautiana!! Ila asilimia iwe sawa!! Tupishane tu kwa kiasi cha pesa kwa kuwa tulitofautiana kiasi cha mshahara!! Don't get me wrong!!
 
Lakini tuambizane ukweli na siyo kudanganyana kuwa ccm inaamini kuwa binadamu wote ni sawa, wakati vitendo ni kinyume chake!
Shida kubwa watu hawana hofu ya Mungu
Japan ukikosea umedhalilisha familia. Yani ukiharibu unatengwa kwanza na familia yako na ukoo kwa ujumla. Mtu yuko kulinda legacy, heshima na dhamana anayopewa ila shida huku kwetu watu wanalamba asali. Naamini kabisa uongozi unatoka kwa Mungu, ukiharibu huna cha kuwajibu watanzania, iko siku moja hutakuwa la kujibu kwa mola wako. .
 
Hakuna aliyesema kila mtu anaweza kuwa rais!! lakini utu wa rais na utu wa askari haupishani!! Wote ni sawa kama binadamu!! Kumbuka hata mafao siyo kuwa tunasema tupate pesa sawa maana kipato kinatofautiana!! Ila asilimia iwe sawa!! Tupishane tu kwa kiasi cha pesa kwa kuwa tulitofautiana kiasi cha mshahara!! Don't get me wrong!!
Kaka utu wa mtu kama Rais hauwezi kuwa sawa abadan na utu wa mtu kama askari milele
 
Back
Top Bottom