Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
lazima tutafute sifa kwa udi na uvumba kujisafishia njia urais 2015
Naona shutuma zote za upungufu ulioibuliwa na CAG unaelekezwa kwa mtoto wa mkulima. Siyo haki. Tusome katiba ya JMT. Waziri Mkuu kama walivyo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Mashirika ya Umma na wenyeviti wa Mabodi wote ni wateule wa Rais hata kama anashauriwa na WM. Baada ya uteuzi kufanyika mwenye mamlaka ya kikatiba kuwajibisha wateule wake ni Rais. Pengine tuna kumbukumbu fupi lakini wakati wa kipindi cha kwanza cha serikali hii, Waziri wa Utalii aliamua kumwajibisha Mkurugenzi wa Wanyama Pori. Jamaa yule alikataa na kukumbusha Waziri wake kuwa wote walikuwa wateule wa mamlaka moja na hivyo hakuwa na mamlaka juu yake. Cha kushangaza Waziri aliondoka kwenye wizara hiyo na kumwacha Mkurugenzi akidunda. Kwa hiyo tusimbebeshe mzigo usistahili mtoto wa mkulima. Msingi wa matatizo tunayoshuhudia ni Katiba yetu mbovu. Tukikubali hivyo tutaacha kukimbizan ana kivuli.
Kwa hiyo ina maana CUF wananunuliwa kwa bei ya Mbunge mmoja sio? siamini kaka duh kama ni hivyo basi tumekwisha si ajabu wanachama wake wakaendelea kujitoa...!usitegemee kitu toka CCM B juzi hapa wamepewa nafasi moja EALA kwa kupigiwa kura na wabunge woote wa CCM A; sasa kwa mantiki hiyo watarudisha fadhila ila itakuwa mbaya kwao haswa kuhusu swala zima la imani ya jamii kwao! we si umeona Prof. Mapumba na Mtatiro walivyo kimya hawajasema lolote mpaka sasa! Natabiri 2015 CUF hawapati hata kiti kimoja bara!
wabunge wa ccm majasiri kama kina Filikunjombe watatoa na watawashawishi wenzao weeengi! sahihi 70 zitatosha!
Naomba kuuliza swali hapa, Great Thinkers. Hivi kweli tatizo ni Pinda au tatizo ni Kikwete? Nauliza hivi kwa sababu wakati wa sakata la Jairo, Pinda alishaashiria kwamba Jairo atajiuzulu lakini baada ya kuzungumza na Kikwete akaambiwa asubiri mpaka Kikwete arejee nchini. Sote tunajua yaliyotokea. Marehemu Sokoine na Kawawa waliwahi kuwa mawaziri wakuu chini ya utawala wa Mwalimu. Kuna baadhi ya maamuzi ambayo walichukua bila kushauriana na Mwalimu na hata kama Mwalimu hakukubaliana nao lakini alikuwa na uungwana wa kutosha kuyaacha yaendelee. Mawaziri wanaotuhumiwa ubadhirifu wamewekwa pale na Kikwete, sidhani kama Pinda ana mamlaka yoyote ya kuwafukuza kazi bila idhini ya rais. Sasa Pinda akijiuzulu ndiyo iweje? Imwachie mlango Kikwete kukwepa lawama na kumchagua swahiba wake Asha Rose Migiro? Nasikia anasubiria sana kiti hicho.