Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Pinda?

Gamba lingine hili, maana yake ndio nini wakati unajua kabisa watu ambao hawapendi mabadiliko ni viongozi kutoka katika chama cha MAGAMBA!

Kwa hiyo dawa ni kuondoa magamba sio eh?
Halafu yakikomaa tena, unaendelea kuyaondoa eh?
Kaaazi kweli. Nimesema Watanzania hatujui tunachokitaka.
 
pinda jaman mtu safi bado tunamhitaji ila hao mawzir wapumzike aletewe vifaa vipya achape kazi

Jamani tanzania yetu hii hata viongozi waseme wanajiuzulu hakuna jipya zaid ya uongo mtupu,nadhani umefika wakati wakuto kubali kudanganywa,Lowasa alijiuzulu nini kilitokea?
 
mimi nimetumhua macho TBC1 nasubiri PM aongee na wazee wa dodoma kumbe kamaliza!
 
Siasa bwana eti pinda anataka kuleta mkanganyiko kati ya kura ya kumtoa ba majibu ya mawaziri wake kujiuzulu siku ya jumatatu ili kuupisha upepo mbaya unaompuliza
 
Naomba kuuliza swali hapa, Great Thinkers.

Hivi kweli tatizo ni Pinda au tatizo ni Kikwete? Nauliza hivi kwa sababu wakati wa sakata la Jairo, Pinda alishaashiria kwamba Jairo atajiuzulu lakini baada ya kuzungumza na Kikwete akaambiwa asubiri mpaka Kikwete arejee nchini. Sote tunajua yaliyotokea. Marehemu Sokoine na Kawawa waliwahi kuwa mawaziri wakuu chini ya utawala wa Mwalimu.

Kuna baadhi ya maamuzi ambayo walichukua bila kushauriana na Mwalimu na hata kama Mwalimu hakukubaliana nao lakini alikuwa na uungwana wa kutosha kuyaacha yaendelee. Mawaziri wanaotuhumiwa ubadhirifu wamewekwa pale na Kikwete, sidhani kama Pinda ana mamlaka yoyote ya kuwafukuza kazi bila idhini ya rais. Sasa Pinda akijiuzulu ndiyo iweje? Imwachie mlango Kikwete kukwepa lawama na kumchagua swahiba wake Asha Rose Migiro? Nasikia anasubiria sana kiti hicho.


Mbona ilipokuja suala la Katibu Wizara ya Afya Mh. Waziri Mkuu mwenyewe alitamka kumsimamisha kazi bila kusibiri simu ya Raisi na suala la Waziri ndio akaliacha kwa Raisi. Waziri Mkuu kama bosi wa Mawaziri wote hawezi kwa namna yoyote kujitoa katika matatizo haya. Yeye alipaswa kumshauri Raisi toka mwanzo sio baada ya tatizo kufikia hatua ya mwisho na kubainika bungeni. Kama W. Mkuu angeona Raisi ni kikwazo angeonekana muajibikaji na makini zaidi kama angejihudhuru kabla ya kusubiri Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani. Vinginevyo, amshauri Raisi awawajibishe au awashauri Mawaziri wajihuhudhuru.
 
Back
Top Bottom