Wabunge CCM Wasema Mukama anachemka

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Nimeshangaa sana kuona wabunge wa CCM kumchoka mapema katibu wao Mukama, wanamwambia awe makini kusuluisha migogoro kabla haijawa mikubwa vinginevyo atakuwa ni kiongozi wa kutatua migogoro, ukiwemo ule wa Chatanda
Naye akajibu kwa kujitutumua kwamba tatizo ni baadhi ya wanachama wanaojifanya wako zaidi ya chama ,"nasema tutawafukuza wote" Swali je anao ubavu wa kuwafukuza ? tunaweza jadili zaidi walitumia kigezo gani kumpata mpaka wanamchoka mapema hivi

Source : Tanzania Daima ya Juni 12, 2011
 
Nakubali ni anguko ambalo hawana namna ya kuinuka, kwisha habari !
 
Kawaida ya magamba ni vipande vidogo vidogo vigumu visivyo na uhai vilivyojishikiza kwenye ngozi! Vikibanduka mnyama atakosa ulinzi atakufa tu! Jaribu kuparua samaki kisha umrudishe majini uta-prove what I'm saying.
 
Kaka mukama, jiji ni tofauti na siasa. Rudi zako kwenye fani. Siasa waachie wanaoijua
 
CCM wanawaza kwa kutumia makamasi akili wamezifungia kabatini
 
huwa najiuliza ikitokea jambo je mukama anaweza kubishana kwa hoja na mtu kama Dk Slaa?mana naona ccm hawana jembe wamemtoa makamba wakaweka Mukama na Nape,
0+0=0
 
Nimeshangaa sana kuona wabunge wa CCM kumchoka mapema katibu wao Mukama, wanamwambia awe makini kusuluisha migogoro kabla haijawa mikubwa vinginevyo atakuwa ni kiongozi wa kutatua migogoro, ukiwemo ule wa Chatanda
Naye akajibu kwa kujitutumua kwamba tatizo ni baadhi ya wanachama wanaojifanya wako zaidi ya chama ,"nasema tutawafukuza wote" Swali je anao ubavu wa kuwafukuza ? tunaweza jadili zaidi walitumia kigezo gani kumpata mpaka wanamchoka mapema hivi

Source : Tanzania Daima ya Juni 12, 2011
Ndugu Mukama inabidi awe makini sana wakati huu.
Ni wakati wa kujenga au kubomoa jina lake.
Kwa sisi wana CCM tunajua kuwa ndani ya chama kuna matatizo mengi ya kimfumo kuanzia ngazi za juu.
Kuna watu wamejipenyeza huko na wankiharibia sana chama hasa ngazi ya wakereketwa.
Mukama akijua kuwa kama ana supoort ya Mwenyekiti wake na wajumbe wenye dhamira njema katika chama , huu ndio wakati wa kuita kijiko ni kijiko na si chepeo.
Akishindwa kufanya hivyo ataangukia ile njia ya Makamba.
Inaelekea sasa hivi Nape yuko peke yake kama sauti ya mtu aliaye nyikani.
So far Mukama bado hajaonyesha uelekeo wa chama kama ambavyo wanachama wangetaka kiwe.
 
CCM na hawa wen gine wanao ongea hapo kwa kumpa tahadhari hawajui kwa nini Mukama kapewa nafasi hiyo . Kaanzia mbali hadi kuwa KM wao CCM. Ana malengo na karudia maneno ya kuwafukuza ngojeeni muone .Kaeni macho yeye anajua anacho fanya .CCM kweli ni zigo .Kale kamgogoro ka Arusha kanawashinda ?
 
Naye Nape ni kama hamna kitu amezidi sana kuropoka ropokan ovyo !
 
CCM na hawa wen gine wanao ongea hapo kwa kumpa tahadhari hawajui kwa nini Mukama kapewa nafasi hiyo . Kaanzia mbali hadi kuwa KM wao CCM. Ana malengo na karudia maneno ya kuwafukuza ngojeeni muone .Kaeni macho yeye anajua anacho fanya .CCM kweli ni zigo .Kale kamgogoro ka Arusha kanawashinda ?

CCm itakufa gafra wakiendekeza kulindana hasa 2015, ccm wanaweza survive kama nao wataamua ngoja na liwe hatufukazani humu lakini Mgombea wetu 2015 ni Magufuri na waziri mkuu ni mwakyembe/mwandosya nk.

CCM wanaweza regain reputation yao kwa kufanya vitu rahisi sana. Lakini wakiendeleza race zao wanazotaka kuna mawili tu 2015 yanaweza tokea either upinzani wa sasa kushinda uchaguzi or baada ya uchaguzi watu kushika mapanga.
 
Watu wanapaswa kujua kwamba CCM ni sawa na meli mbovu, hata ikiendeshwa na nahodha mwenye ustadi namna gani hawezi kuiokoa.
 
hayo unayoyasema wafanye hivi au iwe hivi unafikiri yatawasaidia ccm ni "sikio la kufa"
 
hakuna marefu yasiokuwa na ncha, tukitaka kweli maendeleo na mabadiliko ktt nchi, ni wakati wa kufanya maamuzi mazito... kwa 50yrs ya dependence!! bado tukumbatie hali hiyo?
 
Kifo cha nyani miti yote uteleza! Itakua ni tiba chungu lakini ili CCM ijisafishe itabidi iondolewe madarakani. Wakiwa nje ya dola wataweza vuana vizuri magamba!
 
Makamba alisema naenda kuwaandalia makao, kama yeye alivyopumzishwa na wao chama chote watapumzishwa.
 
Nimeshangaa sana kuona wabunge wa CCM kumchoka mapema katibu wao Mukama, wanamwambia awe makini kusuluisha migogoro kabla haijawa mikubwa vinginevyo atakuwa ni kiongozi wa kutatua migogoro, ukiwemo ule wa Chatanda
Naye akajibu kwa kujitutumua kwamba tatizo ni baadhi ya wanachama wanaojifanya wako zaidi ya chama ,"nasema tutawafukuza wote" Swali je anao ubavu wa kuwafukuza ? tunaweza jadili zaidi walitumia kigezo gani kumpata mpaka wanamchoka mapema hivi

Source : Tanzania Daima ya Juni 12, 2011
hatimaye wamefanikiwa kumng'oa
 
Back
Top Bottom