Sakata hilo, lilibuka juzi usiku, katika kikao cha Wabunge wa CCM, ambacho kilikuwa kinajadili tatizo la umeme, hali iliyomfanya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), kuibuka na na hoja ya kutaka viongozi wa wizara hiyo wawajibishwe.
Hoja ya Sendeka, ilimlenga Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, wawajibishwe kwa kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kilisema kuwa hoja hiyo ya Ole Sendeka, ilionekana ni mwiba kwake, hali iliyomfanya Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kunyanyuka na kumuumbua ole Sendeka.
Lugola, alisema alifuatwa na Ole Sendeka, huku akiahidi kumhonga fedha ili aweze kumuunga mkono hoja yake ya kutaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliachim Maswi, wawajibishwe na Bunge.
"Hoja ya Ole Sendeka, ilimfanya Kangi Lugola kunyanyuka na kuanza kutoa maelezo ambayo kulikuwa na lengo la kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Alipinga wazi kuwawajibisha viongozi wa wizara hiyo, huku akifananisha kinachotaka kufanywa ni sawa na lililomtokea Lowasa.
"Alisema katika ripoti ile ya kamati teule ya Bunge, ilipelekea kumwajibisha Lowassa na baada ya muda iligundulika ilijaa upotoshaji mwingi na kusisitiza katu wabunge hawapo tayari kurudia makosa ya mwaka 2008, ambapo vilitolewa vielelezo vya mitaani," alisema mtoa habari huyo.
Baada ya maelezo ya Lugola, naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), aliunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa mwaka 2008, Bunge liliaminishwa Lowassa, alikuwa mhusika na Richmond, kutokana na jambo hilo kukosa ushahidi alitahadharisha kutorudiwa kwa makosa tena.
"Kilango, alisema wabunge waliamini alikula fedha kwa kulipwa na Richmond, lakini hakuna ukweli, hivyo hakuna sababu ya kumwajibisha Waziri wa Nishati wala Katibu Mkuu wake.
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI GUMZO LA JIJI