Wabunge CCM wamempitisha Ndugai kugombea Uspika

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
Mh. Job Ndugai ameteuliwa kuwa mgombea rasmi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM.

Mbunge wa Kongwa na aliyekuwa naibu spika bunge la 10 lililoisha, Job Ndugai amepitishwa na kamati kuu ya chama cha mapinduzi kugombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya wagombea wengine wawili waliopitishwa mwanzo kujitoa.

==============

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemteua aliyekuwa naibu Spika wa Bunge la 10 Job Ndugai, kuwa mwakilishi wa chama hicho atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye atapigiwa kura na wabunge wa hapo kesho kuwania nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Dodoma kupitia Katibu wa Itikadi na Unezi, Nape Nauye, amesema Dkt. Tulia Mwansasu na Mbunge wa Afrika Mashariki, Abdulla Ally Mwinyi waliamua kujitoa katika nafasi hiyo hivyo kumpa nafasi Job Ndugai kupita bila kupingwa.

Wakati mchakato wa kumpata mwakilishi atakayewakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kinyang'anyiro cha nafasi ya uspika ukiendelea, imebainika kuwa Goodluck Ole Medeye, ndiye atakayesimama katika nafasi hiyo.

Ole Medeye, aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia CCM aliwahi pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi katika utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete (CCM), imeelezwa ndiye atakayewania nafasi hiyo.

Umoja wa Vyama unaofahamika kama Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

Soma zaidi =>Ndugai ateuliwa kuiwakilisha CCM Uspika




 
Last edited by a moderator:
Muda mfupi uliopita Katibu Mkuu Kinana amemtangaza Job Ndugai kuchaguliwa kuiwakilisha CCM katika uchaguzi wa Spika Kesho.
 
Mbona Ngugai ni team Lowassa? Lowassa kamweka mtu wake unachezea pesa wewe?
 
Muda mfupi uliopita Katibu Mkuu Kinana amemtangaza Job Ndugai kuchaguliwa kuiwakilisha CCM katika uchaguzi wa Spika Kesho.

My Take: Magufuli has lost his First Battle.

Kwanini uko concerned sana battle badala ya kuongea mambo ya maana zaidi?
 
Ndugai kama ni yule yule, bunge litamshinda...Kuna wakati alikuwa anazidisha hasira kwenye maamuzi (tolarance limit yake iko chini sana) hekima na busara ipo chini pia...
 
Duh hii kali kwani Ndugai na Magufuli haziivi ?.

Yeah,habari zipo muda sana humu na mitandao mingine Ukitaka soma hapa:-

Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Pombe Magufuli leo ameshusha lundo la tuhuma kwa naibu spika wa bunge na mgombea ubunge wa jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM ndugu Job Ndugai, imethibitishwa.

Magufuli amemtuhumu Job Ndugai kwa kitendo chake cha kueleza hadharani kuwa anaiunga mkono kauli ya Edward Lowassa ya kuunda tume maalum kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji jimboni humo.

Magufuli amesema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi ambavyo Job Ndugai asivyo na imani naye kama mgombea wa urais kupitia chama chake na wala asisingizie migogoro.

Aidha habari za ndani zilizopatikana jimboni humo ni kuwa Job Ndugai alikuwa miongoni mwa wana CCM walio na imani kubwa na Edward Lowassa ingawa kwa sasa hajaeleza msimamo wake baada ya Lowassa kuitosa CCM.
..................
Mimi nipo na timu ya watu wa ndani kabisa wa John Magufuli mikoani.

Link ya JF hii hapa: https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania/943612-magufuli-amshushia-tuhuma-job-ndugai-amtahadharisha-kuunga-mkono-kauli-za-lowassa.html
 
Ndugai nilimwona kwenye kura za Maoni ccm akimpiga mwenzie na rungu sijuwi yaliishia wapi, mnaona kwa hasira alizonazo hataweza kuendesha bunge la safari hii, nashangaa kinana kumtangaza mtu kama huyo,
 
Mbona Ngugai ni team Lowassa? Lowassa kamweka mtu wake unachezea pesa wewe?
Huu mwingine upuuzi tu. lowassa has nothing with this. hao ni wana ccm, mfuasi wa lowassa ni yule aliyejitoa hadharani na kuhama naye hao wengine maisha yao bila ccm hayawezekani
 
Muda mfupi uliopita Katibu Mkuu Kinana amemtangaza Job Ndugai kuchaguliwa kuiwakilisha CCM katika uchaguzi wa Spika Kesho.

My Take: Magufuli has lost his First Battle.

Duuu....team tulia watakuwa wana gugumia tu kwikwi.

Ila mkuu Job Ndugai punguza zile hasira zako maana kina Lissu
wanaweza chezea bakora bunge hili.
9k=

ukawa mkinizengua mjue kuwa
njia nyeupeeeee...mkapigie
kelele zenu huko nje na sio humu mjengoni.
sasa azengue mtu...

NB:(naibu spika niletee kile kibakora cha kwenye kampeni nikae nacho karibu)
1.jpg
 
Last edited by a moderator:
Yametimia. Nasubiri kwa shauku kubwa kusikia Tulia Akson akitangazwa kuwa Naibu Spika
 
UKAWA mpooooo hesabuni maumivu!

Maumivu gani jinsi ambavyo bunge lunaendeshwa bila ya kuzingatia haki na usawa ndivyo ambavyo mnazid ipaisha ukawa msijidanganye mkamjaza sifa akaenda ibeba ccm kma alivyofanya makinda mtajuta tena
 
Tunataka kaz sisi CCm sasa haina mtandao atakae shiNda ndio mshindi lOwasa kashindwa coz of mitandao....Ndugai atosha
 
Back
Top Bottom