Wabunge akiwemo 'Ndesa pesa' na Madiwani wa Chadema Moshi wameweza Mikoa Mingine je..?

Mkuu, ada za shule za kata ni 1500 kwa mwaka! Kwani Moshi kuna mayatima wangapi?

moshi pako bomba watu wameenda shule,ada kwa sasa navyolipa mimi ni 20,000 plus mavitu mengine jumla 35,000 hapo bado dawati ,pesa ya mlinzi nk
 
Mkuu, ada za shule za kata ni 1500 kwa mwaka! Kwani Moshi kuna mayatima wangapi?
Wakazi wa Dar mjifunze kutoka Moshi, hizo wilaya zenu zina matajiri wangapi?

Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala hazina watu wanazozijali kama ilivyo kwa Moshi?

Hapo utaona utofauti, Moshi huwezi fananisha na Dar.
 
Wakazi wa Dar mjifunze kutoka Moshi, hizo wilaya zenu zina matajiri wangapi?

Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala hazina watu wanazozijali kama ilivyo kwa Moshi?

Hapo utaona utofauti, Moshi huwezi fananisha na Dar.
Dar kweli dampo.....mpaka yatokee mabalaa kama haya ya mafuriko ndio watu wanatafakari jinsi mji wa dar ulivyo hovyo.......alafu mbaya zaidi ni kwamba shughuli zooote za utawala wa nchi.....yaani mawizara na taasisi zoote nyeti eti ziko dar.....watawala wameshindwa kabisa baada ya miaka 50 angalau kusambaza hizi huduma nchi nzima......mpaka pale mji utakapodondoka jumla (collapse) siku moja ndipo vichwa vya watawala vitaamka.....we angalia tu juzi vidaraja kadhaa vimeshindwa kupitika....watu wameshindwa kuingia mjini makazini........yaani shughuli za kuendesha nchi ziliingia matatani.....kwasababu kila kitu nchini kiko kwenye kasehemu tu kadogo ka mji ambao nao ni feki......it takes disasters in tz yaani ili watu waamke,wafikiri na wachukue maamuzi.......what a f****ng banana republic we have eh!!!!!!
 
Kama Moshi wameweza kwanini sisi Dar tushindwe, kinachotakiwa ni mikakati tu. Mimi binafsi naamini kuwa tunaweza tukaboresha hali ya usafi. Kwa kuanza zingetungwa sheria ndogo za usafi na kutolewa elimu ya kutosha kwa wananchi kwa kipindi cha miezi 3 hivi, dustbin ziweke kila mahali, vyoo vya kulipia vijengwe kwa wingi, Kwa kuanzia tungeanza na eneo la mjini (maeneo ya posta), K'koo tuiache kwanza, tuendelee kwa kupanua kidogo kidogo. Nina imani tunaweza kabisa.
 
Back
Top Bottom