Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,552
- 2,360
We Hofstede umetuchambua sana watu wa tbr, mengi ni ya ukweli ila hilo la mlo mmoja na barabara haujatutendea haki. Kama umekwenda Tbr. hivi karibuni utakubaliana na mimi kwa upande wa barabara hasa za ndani tunafanya vizuri sana. Nadhani baada ya Dsm sisi ndio tunafuatia kwa urefu wabarabara za lami zinazo zunguka mjini, tatizo letu ni barabara za kutuunganisha na mikoa na mwaka huu tumepigana sana tumewekewa fedha angalau za kuunganisha na manyoni.