Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,008
wadau Michigan wafurahia Summer huko Cedar Point
Ankal,
Jumamosi Jumuiya ya Watanzania michigan TAMI iliandaa siku ya kujumuika pamoja katika kutemebelea viwanja vya maonesho ya bembea za aina mbalimbali na burudani huko Cedar Point kwenye Jimbo la Ohio.
Wanachama na familia zao pamoja na Watanzania wengine ambao walipenda kushirikiana nasi tukiwa na marafiki zetu wengine kutoka England, na Congo tuliweza kujumuika katika kufurahia majira haya ya joto kwenye viwanja hivi maarufu ambapo wenye kuthubutu waliweza kupanda bembea ziendazo kasi na kushuhudia burudani nyingine mbalimbali. Mjumuiko huu ni wa kwanza kwa mwaka ambapo TAMI imelipa gharama nusu ya tiketi na kukodisha usafiri wa kwenda huko.
TAMI imeandaa shughuli nyingine za kutuunganisha Watanzania pamoja katika furaha, umoja, upendano na udugu ambao msingi wake ni kuheshimiana, kushirikiana na kuwa pamoja katika shida na raha. Wiki ijayo TAMI inashirikiana na jumuiya za Wana Afrika Mashariki wenzetu katika kuandaa sherehe ya Siku Kuu ya Uhuru wa Marekani, Julai 4. Mwishoni mwa mwezi wa saba TAMI imeandaa vile vile burudani ya muziki wa "kukata na shoka" katika tarehe, muda na mahali ambapo tutathibitisha baadaye.
Zifuatazo ni baadhi tu ya picha za baadhi ya wanachama wakiburudika Cedar Point. Unaweza kuona picha zaidi kwenye tovuti yetu ya: