Wabadhirifu wa fedha za umma wafilisiwe mali zao

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,148
7,724
Kwanza kabisa natoa pongezi kwa waziri Mkuu kwa moto alio uwasha kwa kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi yote ya Serikali inayo endelea kwenye kila Mkoa nchini.

nafuatilia kwa karibu kila ziara za ukaguzi Mkoa wa Iringa, Katavi, Tabora, Pwani n.k, imebainika karibu kila mradi kuna wizi/ubadhirifu wa fedha za umma!

Lakini jambo la kushangaza zaidi hakuna hatua za kiuchunguzi ambazo zimefanywa na vyombo husika!

Jamani eeeeeee, nchi yetu haiwezi kusonga kwa mtindo huu, yaani kweli kabisa Afisa anachoma nyaraka kupoteza ushahidi kisha anaangaliwa tu!

Nashauri wale wote wanao tuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za umma wafilisiwe mali zao.

Lakini pia inashangaza viongozi wa mikoa kwa nini hawasimamii na kukagua miradi ya Serikali ili kujiridhisha?

Pongezi tena kwa waziri Mkuu kwa jitihada za kushughulikia kero hizi, hakika mambo haya ndio yanarudisha maendeleo ya wananchi nyuma.

Hakuna kuchoka tupanmbane kwa masilahi ya wananchi.
 
Afanye ufuatiliaji kwenye miradi mikubwa hasa ujenzi wa barabara atajionea mengi huko kazi haziendi na rushwa zake ni kubwa kubwa TANROADS na TARURA ni kichaka
 
Back
Top Bottom