Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,669
- 4,920
Ni katika pambano la Masumbwi lililofanyika jana usiku katika ukumbi wa Boulevard Hall, katika jiji la Riyadh nchini Saudi Arabia.
Watu wengi Duniani katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii wameonekana kuuzunishwa na matokeo ya pambano hilo la Boxing ambapo Bingwa mtetezi wa Masumbwi uzito wa juu "WBC Heavyweight Champion" Tyson Fury ambaye alifuana na Bingwa aliyepita wa pambano la UFC "UFC Heavyweight Champion" Fransic Ngannou, ambapo walishinda katika pambano la Heavyweight Professional Crossover Boxing.
Yani hili ni pambano ambalo mfano wanachukua bingwa wa Dunia Boxing na Bingwa wa Dunia wa UFC (MMA-Mixed Martial Arts), au tu mabingwa kutoka tasnia tofauti tofauti ya michezo na burudani, wanaweka kwenye ulingo wanapambana boxing.
Katika pambano hilo lililofanyika jana huko Uarabuni katika ya Muafrika kutoka Cameroon "Fransic Ngannou" na Mzungu kutoka Uingereza "Tyson Fury", majaji walimamiza pambano kwa "Split" kuwaachanisha na kisha kugawa point kama zifuatavyo;
JAJI
1. Alan Krebs: Fury 95 - Ngannou 94
2. Carlos Pelayo: Fury 96 - Ngannou 93
3. Ed Garner: Fury 95 - Ngannou 94
View: https://x.com/MichaelBensonn/status/1718432217544700365?s=20
Ukitizama Pambano vizuri mwanzo mpaka mwisho utagundua kabisa, raia kutoka Cameroon, bwana Fransic Ngannou yeye ndiye aliyetawala mchezo, kwa kifupi alipaswa kupata point nyingi kulingana na namna alivyopeleka kichapo kizito kwa Tyson. Hata hivyo Fransic Ngannou alionekana kuuzunishwa na matokeo hayo baada ya kunyanganywa ushindi huo mnono dhidi ya muingereza katika ardhi ya waarabu.
View: https://youtu.be/tHFdnJsz9Uc?si=GyiQ4XG2a1HJyhQb
Pambano hilo liliudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Mike Tyson, Eminem, Christiano Ronaldo, Kanye West, na Lil Baby.