Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 17,457
- 21,161
Rais wa WBC Mauricio Suleiman atoa pendekezo kuwe na V.A.R kwenye pambano la wababe kati ya Tyson Fury (Gypsy King) na Oleksandr Usyk (The cat).
Mauricio hakuishia hapo apendekeza pia kuwe na majaji watano kwenye hilo pambano la wababe litakalofanyika May 18 Riyadh Saudi Arabia.
Sababu kuu ya kufanya hivyo ni kuondoa lawama au dosari zozote zile za upendeleo ili mtu akipigwa apigwe kihalali kusitokee malalamiko ya aina yoyote ile kama malalamiko yaliyotokea kwenye pambano la mwisho la Tyson Fury dhidi ya Francis Nganou.
Ikumbukwe pambano hili ni kubwa sana kwa kuwa wanaunganisha mikanda yote minne mikubwa kidunia kupata undisputed champion katika uzito wa juu zaidi
(heavyweight division).
Wote wawili hawana historia ya kupigwa .
Tyson Fury ana jumla ya mapambano 35 ameshinda 34 ,24 kwa K.O na moja ametoa sare.
Usyk anajumla ya mapambano 21 ameshinda yote ,14 kwa K.O.
Ikumbukwe Usyk alikuwa Undisputed champion kwenye uzito wa cruiserweight na baada ya kuona hana tena mpinzani baada ya kumchapa swahiba wa Anthony Joshua anaitwa Anthony Bellew ambaye angalau kidogo alikuwa anaonekana Bora kwenye uzito huo ndipo akapanda uzito mpaka heavyweight kupata challenge mpya.
Usyk ameendeleza ubabe kwenye heavyweight na kufanikiwa kuchukua mikanda mbalimbali ikiwemo mikanda mitatu mikubwa ya kidunia ambayo ni WBA,WBO na IBF amebakisha mkanda mkubwa mmoja ambao ni WBC unaoshikiliwa na Tyson Fury.
Hakika hili pambano la wababe na rais hataki kabisa kuona mbeleko ya aina yoyote atakayeshinda basi ashinde kihalali.
#ENJOY THE SWEET SCIENCE OF BOXING#.
Save the date May 18 2024.
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥