Waandishi wa habiri wa tz ni wavivu kutafuta habari

Zhu

Senior Member
Sep 26, 2010
184
24
Kumekuwepo na kasumba kwa waandishi kusubiri viongozi waaite waandishi na kutoa taarifa za 'akiongea na waandishi...' Iwe Tv iwe gazeti. Badala ya kutafuta chanzo cha habari kwa kina wanategemea group thinking badala ya mwandishi binafsi kuwa mdadisi wa jambo. Kwa sasa waandishi wajali biashara baadala ya kuangalia athari kwa msomaji. Kwa mfano tukio la arusha. Vifo habari zilianza watu 10, halafu 6 na mwisho 3. Waache uvivu wa kufuatilia jambo mpaka ujiridhishe kuwa habari hii ni sahihi. Mambo ya kwenda Habari maelezo tu haitoshi. Tupeni habari zenye uthibisho.
 
matatizo makubwa ya Tanzania katika sekta ya habari ni kuwa hao waandishi hawajaspecialize, utashangaa mwandishi huyohuyo anaandika siasa mara kesho uchumi mara kesho michezo na vyote vinakuwa shallow,
Jerry Muro alionesha angalau yeye alikuwa kwenye uandishi wa kiuchunguzi na kipelelezi na alikuwa anaelekea vizuri, lakini kazi yake haikupendwa na wakubwa wengi
Ukimpata msomi wa uchumi hata level ya degree na akasomea uandishi wa habari basi kazi yake akiandiak kuhusu uchumi itakuwa na uchambuzi wa kina

hata hili tatizo la dowans, kama kungekuwa na mwandishi mzuri wa habari ambaye pia ni mwanasheria basi angekuwa anaandika habari zenye uzito na uchambuzi wa kina
 
Bahati mbaya wengi wetu leo ni maslahi kwanza! As long as mwandishi anashiba, hajisumbui zaidi! Madhara ya uvivu hauwasumbui akili kwani maslahi yao yanazingatiwa!
 
kweli zhu...., sio habari tu hapa bongo kila industry mwendo ni kubahatisha tu..... hakuna wachapakazi bali wasanii
 
kweli zhu...., sio habari tu hapa bongo kila industry mwendo ni kubahatisha tu..... hakuna wachapakazi bali wasanii

hapo mkuu nakuunga mkono kabisa, ukiangalia madudu wanayoyafanya Mwanasheria mkuu na yule mwendesha mashtaka wa serikali hapo ndio utajua kweli tumeoza kila sehemu,
 
wengi wao hawana misimamo ktk uandishi wa habari za kina, kwa kuhofia kuwaudhi baadhi ya vigogo walio madarakani.
 
Back
Top Bottom