CriticalThinker
Member
- May 27, 2009
- 7
- 0
Hivi ni kwanini tusianzishe mjadala kupambana na uandishi uchwara??? Fani ya uandishi hapa nchini imepoteza sana heshima yake kutokana na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa waandishi wenye taaluma ya juu (elimu ya chuo kikuu angalau), malipo hafifu na mengine mengi lakini cha kusikitisha zaidi ni juu ya habari zenyewe zinazoandikwa kutokuwa na credibility maana siku hizi waandishi badala ya kufatilia mambo kwa kina wana-download habari kutoka kwenye blogs na forums kama hii. Huu ni ujinga kwakweli, mambo kama haya yanahitaji kurekebishwa haraka ili kunusuru fani hii.