Waandishi wa Habari acheni kulalamika. Tamaa zenu na kukosa maadili ndio anguko lenu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Waandishi wa habari acheni kulalamika; mnavuna mlichopanda. Thamani yenu imeshuka sana kwenye jamii na miongoni mwa watawala. Hakuna kazi mnayofanywa inayopendwa kwenye jamii.

Tumeruhusu nchi imebaki na vyombo vya habari vya michezo, vipindi vya michezo vimekuwa kipaombele vya Taifa. Mambo ya msingi hakuna anayetaka kuyajadili wala kuyachambua, hapa ndipo dharau ilipo.

Leo wachekeshaji wote wamegeuka waandishi wa habari, mnategemea nana ataheshimu taaluma? Mkishindwa kulinda taaluma hakuna mtu atakuja kuwasaidia kuilinda. Endeleeni kuamini kwenye comedy mkidhani mnakuza taaluma, kumbe mnaiua

Wasanii wamekuwa maarufu hadi viongozi wa kisiasa wanaamini agenda zao zipo salama kwa wasanii kuliko waandishi wa habari!

Bado hamjasema?
 
Waandishi wa habari acheni kulalamika; mnavuna mlichopanda. Thamani yenu imeshuka sana kwenye jamii na miongoni mwa watawala. Hakuna kazi inayopendwa jamii mnayofanya.

Tumeruhusu nchi imebaki na vyombo vya habari vya michezo; vipindi vya michezo vimekuwa kipaombele vya Taifa: mambo ya msingi hakuna anayetaka kuyajadili wala kuyachambua ; hapa ndipo dharau ilipo.

Leo wachekeshaji wote wamegeuka waandishi wa habari mnategemea nana ataheshimu taaluma? Mkishindwa kulinda taaluma hakuna mtu atakuja kuwasaidia kuilinda. Endeleeni kuamini kwenye comedy mkidhani mnakuza taaluma kumbe mnaiua

Wasanii wamekuwa maarufu hadi viongozi wa kisiasa wanaamini agenda zao zipo salama kwa wasanii kuliko waandishi wa habari.

Bado amjasemaaaaaa
Well said!
1. Kwanza hatuna waandishi wa habari... ni makanjanja wa academic failures.....f4 &6 failures...Nape and team
2. Njaa za bahasha ,kuhongwa akina Balile and team.....
 
Waandishi wa habari wengi ni wajinga, waliofeli huko walikotoka, wakakimbilia uhandishi wa habari kwasababu ndio ilikuwa cheap option kwao.

Bahati mbaya baada ya kufika hapo, hawajiendelezi kielimu, wameridhika, wanafanya kazi kwa mazoea, ndio maana hata ukisikiliza maswali wanayowauliza wale wanaowahoji, utaona wazi ni maswali mepesi, yanayoonesha vichwa vyao havina kitu ndani.
 
Tunapoelekea hata bahasha zitaondolewa kwa waandishi wa habari na kupelekwa zaidi kwa wasanii.......njaa itazidi zaidi na hapo ndipo taaluma itazikwa rasmi.

Waandishi wa habari wamezalisha ubaguzi wa habari awakujua nao watabaguliwa.......wamebaguliwa na wananchi sasa wanabaguliwa na watawala.


Bado awajasemaaaaaa
 
Mimi NAVYOJUA mwandishi wa habari especially Hawa wa tv ni wale tunawaona kwenye news kila siku au interview kubwa kama dk 45 itv tatizo vyombo vya habari siku hizi wanaajiri Sana presenters (watangazaji) lakini unakuta ana ELIMU ya habari ,ana ethics na confedintiality ya habari .....Hapo ndio shida inapoaanzia kwa bongo hapa ITV ndio ina WAANDISHI WA HABARI WENGI KULIKO PRESENTERS
 
Kukosa msimamo kwa wanahabari ni tabu sana Aliandika jamaa mmoja

 
Jamaa fulani anaitwa Neville naona analalamika kweli kweli kudhalilishwa na Dr. Tax kwa kuwaitwa hao wasanii waandishi wa kisasa.

Sasa huyu huyu Neville ndiye angepaswa kulalamika pale wananchi wanavyopiga kelele kuhusu issue ya bandari ila kakaa kimya akijua atakosa mkate kwa kujikomba.

Nowadays teknolojia imeibua waandishi wengi na wengine wamekuwa maarufu kuliko hata wao, ila anabweka utadhani ananyang'anywa roho.

Viongozi wanajua na wanataka kuonwa na Wananchi katika njia yoyote pasipo kujali wewe no mhariri wa jarida au uliwahi kwenda fungate la wahariri Tanga na mkalipwa na NCAA.

Mwandishi unaegemea upande mmoja au ukibalance story upande ambao haukupi mkate unaubinya kwa kujibalance mwenyewe na storyline yako!.

Dr. Tax kagongwa penyewe na ule ndiyo ukweli hasa!.
 
Vyombo vya habari kama clouds, EFM na Wasafi angalia wana waandishi wa habari wangapi na wasanii wangapi

Angalia kwenye vyombo hivyo vipindi vya michezo vinachukua asilimia ngapi ya muda wa vipindi vyote kwa jumla......nenda Duniani kote katafute nchi ambayo michezo ni kiapo mbele kwenye vyombo vya habari kama utapata.

Lakini hata hiyo michezo nini kinajadiliwa chenye mrengo chanja wa jamii; hakuna cha maana zaidi ya kubishana jambo lilelile asubuhi, mchana na usiku.....hakuna topic mpya zinazoibuliwa.....mijadala ya michezo kama dozi vile MKUDE/MAYELE/YANGA / SIMBA kutwa mara tatu


Lazima mdhalilike.......


Na bado amjasema
 
Press conference na minister ni 10am,hadi 10:30am waziri hajatokea kwenye mkutano wake, why hawakuondoka pale?,.. jibu rahisi ...brown envelopes, Katabalo atakua anageuka kwenye nyumba yake ya kudumu
 
Tunapoelekea hata bahasha zitaondolewa kwa waandishi wa habari na kupelekwa zaidi kwa wasanii.......njaa itazidi zaidi na hapo ndipo taaluma itazikwa rasmi.

Waandishi wa habari wamezalisha ubaguzi wa habari awakujua nao watabaguliwa.......wamebaguliwa na wananchi sasa wanabaguliwa na watawala.


Bado awajasemaaaaaa
Na watasema
 
Neville Meena; kama unakubaliana na akina chumvi kwanini ufanye ubaguzi kwa wasanii wengine? Hao wasanii mnaowalalamikia kupewa hadhi ndio hao hao akina Masanja mnaowapa hadhi kwenye vyombo vyenu mnavyovisimamia. Ukitaka kulaani anzia kwenye vyumba vya habari.

Angalia usomaji wa magazeti wa siku hizi; wanaume wanavaa kike kusoma magazeti means mmekaa kimya kila kitu kimekuwa comedy bila kujua mnatutengezea kizazi cha watoto wa kiume kuvaa kama joti au Masanja........

Fanyeni self evaluation
 
Baada ya kizazi cha waandishi wakongwe kina Jenerali, Hamza kasongo, Makwaia wa Kuhenga na wengineo wa wakati huo muda wao kusogea, tasnia hii imepwaya kabisa.
 
Inasikitisha sana, huwa nikiangalia TV's za hapo Kenya tu nikalinganisha na za kwetu naumia zaidi. Elimu kwetu haipewi kipaumbele kabisa!
 
Hizi ndizo nguzo kuu na tano utambuzi wa yeyete anayetaka heshima ya kuitwa Mwandishi wa Habari: 1. Accuracy, yaani ukweli wa kile anachokiandika bila kujali bila kujali maumivu ya ukweli wenyewe. (1) Independence, uhuru wa kutoa taarifa ya ukweli bila kushawishiwa au kutishwa. (3) interest of the public, aweke maslahi mapana ya nchi mbele (4)Empathy, aweze kuvaa viatu vya uhusika (5) integrity, kuaminika kunakotokana na kujiheshimu. Kama mjumbe (messenger) uonekane mtoa ujumbe unayeaminika kutokana na elimu Yako kwenye uandishi, uzoefu wako kwenye tasnia au eneo unayolitolea taarifa, uaminike unapotoa taarifa. Hivi vigezo kama huna basi wewe ama si Mwandishi au Umehongwa. Sio jukumu la mwandishi kutushawishi kuhusu jambo lolote Bali kutupa taarifa sahihi ili sisi wananchi tuweze kufanya maamuzi sahihi yakiwemo ya uzuri au ubaya 2a mkataba wa Bandari. Mwandishi au chombo chochote Cha habari kinachoonekana kufanya ushawishi basi ama si chombo Cha habari au kimehongwa. Tuwe macho kuwatambua Kwa matunda Yao. Nachelea kuamini kuwa Wizara inayolalamikiwa kama mlaji, Ina Haki ya kuchagua wanachotaka. Ni jukumu la wanaotaka kutambulika na kuheshimika kama waandishi kujiongeza.
 
Back
Top Bottom