Waandishi na wabunge mnamuogopa Rashid Othman?

Hoja ya Mzee Mwanakijiji inachanganya mambo mengi lakini inaonekana wazi kwamba haifahamu TISS na majukumu yake chini ya uongozi wa RASHID OTHMAN kama Mkurugenzi Mkuu. Sina uhakika kama Mzee Mwanakijiji ana maana gani anapomfananisha RASHID OTHMAN na mpelelezi ambaye ameshindwa kuwakamata wezi wa BOT, wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi – albino, kumkamata mtoto aliyerusha chupa ya mafuta ya taa ili kulipua magari kwenye Ubalozi wa Marekani na kuwazuia wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wasifanye maandamano mwaka 2000.

Mzee Mwanakijiji anasema RASHID OTHMAN na vijana wake wa TISS wanaacha kutimiza majukumu yao kwa sababu wanapata mgao unaotokana na uhalifu. Nafikiri Mzee Mwanakijiji anatafuta habari kwa njia za uchokozi na hajafanya utafiti wa kile anachotaka kukisema. Ana bahati mbaya sana kwa sababu hajakadiria uharibifu anaofanya kwa kuelezea TISS na Mkurugenzi wake Mkuu kwamba imedorora.

Pamoja na kwamba Mzee Mwanakijiji hajataja tukio lolote ovu ambalo linahatarisha Usalama wa Taifa ni vizuri afahamu kwamba Idara ya Usalama inayoongozwa na RASHID OTHMAN, kwa sisi tunaoishi mitaani, TISS kama ‘Central Intelligence Agency’ ya Marekani inayoongozwa na LEONS’ PANNETA zina kazi ya kutoa ushauri juu ya makadirio ya hali ya kiusalama na sio kutoa sera, kufanya kazi za kipolisi au Jeshi la Wananchi. Sisi tulio mitaani tunakuwa na wasi wasi kama kweli Mzee Mwanakijiji anafahamu majukumu ya kazi za vyombo vya Usalama akianzia na TISS na hutumia mtandao huu kutoa somo kwa wananchi. Inabidi afanye utafiti wa kutosha na hata awaulize Wabunge kama wanaionaje TISS chini ya RASHID OTHMAN.

Mzee Mwanakijiji anatakiwa afahamu kwamba TISS, kama ina upungufu, upungufu huo unaweza kuonekana pia kwenye vyombo vingine vya Kimataifa vinavyofanana nacho kama CIA ya Marekani, KGB ya Shirikisho la Urusi au hata MOSSAD ya Israel. CIA ni chombo kikubwa cha Marekani kinachofanya kazi kama TISS, lakini chombo hicho kina mafanikio na mapungufu yake. Chombo hicho kikubwa kimekuwa na kile kinachoitwa ‘Intelligence Failure’ kuanzia vita vya Korea, miaka ya 50, Vietnam miaka ya 70, Iraq miaka ya 90 hadi sasa, na Cuba – Bay of Pigs na Afghanistan. Mzee Mwanakijiji anaombwa asome juu ya hilo kabla ya kuishambulia TISS ambayo sisi tulio mitaani tunasikia ikisifiwa kwa weledi, ujasiri na umakini wa watendaji wake chini ya RASHID OTHMAN.

Mkuu,

Natofautiana kidogo na wewe unaposema kuwa taasisi kama CIA haifanyi kazi za kipolisi.....!Huu ni uongo!Taasisi hizi zinafanya kazi za kipelelezi na ikibidi kuchukua hatua inapobidi.Unataka kuniambia mpelelezi wa Usalama wa Taifa akiona mtu anataka kulipua jengo atapiga simu polisi?Get real!
 
Hoja ya Mzee Mwanakijiji inachanganya mambo mengi lakini inaonekana wazi kwamba haifahamu TISS na majukumu yake chini ya uongozi wa RASHID OTHMAN kama Mkurugenzi Mkuu. Sina uhakika kama Mzee Mwanakijiji ana maana gani anapomfananisha RASHID OTHMAN na mpelelezi ambaye ameshindwa kuwakamata wezi wa BOT, wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi – albino, kumkamata mtoto aliyerusha chupa ya mafuta ya taa ili kulipua magari kwenye Ubalozi wa Marekani na kuwazuia wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wasifanye maandamano mwaka 2000.

Mzee Mwanakijiji anasema RASHID OTHMAN na vijana wake wa TISS wanaacha kutimiza majukumu yao kwa sababu wanapata mgao unaotokana na uhalifu. Nafikiri Mzee Mwanakijiji anatafuta habari kwa njia za uchokozi na hajafanya utafiti wa kile anachotaka kukisema. Ana bahati mbaya sana kwa sababu hajakadiria uharibifu anaofanya kwa kuelezea TISS na Mkurugenzi wake Mkuu kwamba imedorora.

Pamoja na kwamba Mzee Mwanakijiji hajataja tukio lolote ovu ambalo linahatarisha Usalama wa Taifa ni vizuri afahamu kwamba Idara ya Usalama inayoongozwa na RASHID OTHMAN, kwa sisi tunaoishi mitaani, TISS kama ‘Central Intelligence Agency’ ya Marekani inayoongozwa na LEONS’ PANNETA zina kazi ya kutoa ushauri juu ya makadirio ya hali ya kiusalama na sio kutoa sera, kufanya kazi za kipolisi au Jeshi la Wananchi. Sisi tulio mitaani tunakuwa na wasi wasi kama kweli Mzee Mwanakijiji anafahamu majukumu ya kazi za vyombo vya Usalama akianzia na TISS na hutumia mtandao huu kutoa somo kwa wananchi. Inabidi afanye utafiti wa kutosha na hata awaulize Wabunge kama wanaionaje TISS chini ya RASHID OTHMAN.

Mzee Mwanakijiji anatakiwa afahamu kwamba TISS, kama ina upungufu, upungufu huo unaweza kuonekana pia kwenye vyombo vingine vya Kimataifa vinavyofanana nacho kama CIA ya Marekani, KGB ya Shirikisho la Urusi au hata MOSSAD ya Israel. CIA ni chombo kikubwa cha Marekani kinachofanya kazi kama TISS, lakini chombo hicho kina mafanikio na mapungufu yake. Chombo hicho kikubwa kimekuwa na kile kinachoitwa ‘Intelligence Failure’ kuanzia vita vya Korea, miaka ya 50, Vietnam miaka ya 70, Iraq miaka ya 90 hadi sasa, na Cuba – Bay of Pigs na Afghanistan. Mzee Mwanakijiji anaombwa asome juu ya hilo kabla ya kuishambulia TISS ambayo sisi tulio mitaani tunasikia ikisifiwa kwa weledi, ujasiri na umakini wa watendaji wake chini ya RASHID OTHMAN.

Mkuu with due respect, kama sikosei ni Magezi ndo aliye chambua hivi!!! Au ulimaanisha Magezi na si Mzee Mwanakijiji?
 
Back
Top Bottom